Kwanini Rais akitaka kufanya jambo anazunguka sana kupata uhalali?

careenjibebe

JF-Expert Member
May 28, 2020
900
1,000
Habari wana JF,

Tangu Mh. Rais ameshika madaraka, ameonekana akitaka kufanya jambo anatafuta "zuga" flani ili aeleweke.

Swali ninalojiuliza kwa nini asiwe anachukua msimamo na kulifanya jambo moja kwa moja?

Mfano:
1. Inafahamika kabisa swala la kuondolewa kwa "machinga" alishalipitisha siku nyingi tu. Na hii itakuwa operation katika majiji yote makubwa. Sasa Mh Rais akaona afunge ziara aende kariakoo, kisutu, n.k akidai eti ameenda kujionea. Hivi pale kariakoo alijionea nini kipya?

Pia ktk mpango huu, wameona ni lazima Halmashauri/jiji wachukue uendeshaji wa masoko yaliyo kwa viongozi au vyama vya masoko (mf. kariakoo shimoni). Sasa hili nalo badala ya kutamka tu, Yeye akasema ameenda, amesikia malalamiko, na akasimamisha uongozi ili soko liendeshwe na jiji. while inafahamika kabisa ni maamuzi walishayapanga.

Swali: Kwani Machinga Complex haipo chini ya Halmashauri?

2. Mfano namba mbili, ni ishu ya kupambana na corona. Inafahamika kabisa Mama alishakubaliana na swala la chanjo. Sasa namna alivyozunguka na kuunda tume utafikiri kweli, TUNAPAMBANA NA CORONA.

Swali la kumuuliza Mama, mbona hafafanyii kazi mapendekezo mengine, ila anafanyia kazi pendekezo moja tu la chanjo? vipi kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni, vipi physical distance, vipi uvaaji barakoa? Mbona si lazima? au uongozi ni kuvaa wewe tu? Kwa nini usingetamka kwamba tunafanya taratibu namna ya kupata chanjo, ukazunguka kuunda tume!!

3. Ishu ya Manji
Inafahamika kabisa ashapata 'clearance' huko juu. Pale TKKR mmempeleka ili asafishwe na kufanya "zuga" flani.
Sasa kwa nini msimuache tu.

Najua ipo "zuga" unayowaandalia CHADEMA. Hahaha...

Binafsi hii style ya 'zunguka-zunguka' ili uamue jambo sioni haja yake. Simamia tu kile unachokiamini moja kwa moja.

Asante.
Hii si kaz yako ndo maana huelewi
 
sengobad

JF-Expert Member
Aug 13, 2017
4,417
2,000
Eeeh Bhwana, unasema kweli?

Mimi bado ninashangaa na lile tukio la Bomba la Mafuta Kigamboni, ni kama halipo kabisa, au ni sinema?

Inawezekana linanyimwa uzito stahiki ikiwa ni mbinu za kulififisha, kutokana na wazito wanaohusika nalo?
Kusema kweli inashangaza, kuanzia polisi, waziri mkuu, waziri wa nishati wote wako kimyaaa.
 
sengobad

JF-Expert Member
Aug 13, 2017
4,417
2,000
Kwenye nukta yako namba mbili nikukumbushe tu hayo mengine uloyataja ni mambo ambayo yapo kwa kila mmoja...! Mf.. Suala la kunawa maji churuzika halihitaji serikali ikusimamie, aidha suala la chanjo sio la mtu mmoja mmoja bali serikali ndio mwenye jukumu hilo moja kwa moja.

Aidha kwa kile ulichokiita zuga na mifano iloitoa sijaona muunganiko wake. Nikukumbushe tu kuwa unapotaka kuvuka mtari lazima ujiandae..., kama umevaa kanzu au msuli huna budi kukunja kwanza ili usipate ajali. Ninachokiona kwa Mama yeye hakurupuki kutaka kuruka tu maadamu anaweza kufika ng'ambo ya pili, bali hujiandaa nakuweka mazingira sawa kwanza na huo ndii sisi watu wa pwani tunaita uungwana.
Kwenye korona naona kuna kauzaifu au labda wamegundua kuwa hata hizo hatua tulizoimizwa toka mwanzo tuchukue labda hazisaidii, kama hatua hizo zinasaidia kweli sioni sababu ya kutoimiza watu kunawa mikono kila mahali na kuagiza wakuu wa mikoa wasimamie hilo jambo, sioni sababu ya kutohimiza uvaaji wa barakoa labda tu kama wamegundua kuwa hazina msaada.
 
Marathon day

Senior Member
Jan 31, 2020
158
250
Huyu ni Mama lazima abembeleze watoto wote hata watoto wakorofi.

Anaenda nao taratibu..
Huwa nafatilia comments zako, huwa uko makini sana ,hukurupuki na comments zako, uko sawa kwa hili mama huwa anafanya maamuzi kubalance kwa watoto wote alie sahihi na mkosaji.Tumwelewe mama nadhani yuko sahihi.
 
Kalamu1

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
10,485
2,000
Kusema kweli inashangaza, kuanzia polisi, waziri mkuu, waziri wa nishati wote wako kimyaaa.
Kuna jambo zito hapa.

Hata vyombo vya habari havitaki kuligusa!

Halafu tunaambiwa Mbunge wa Sengerema anatishiwa maisha, kwa kuzungumzia mambo yahusuyo eneo hilo hilo la nishati, si maajabu haya?
 
Sheikh23

JF-Expert Member
Jul 11, 2016
861
1,000
Mama yupo sahihi,mambo ya kuropokeana na maamuzi ya kejeri mbele ya kadamnasi yanatweza utu,kila mtu ana style yake ya uongozi,tusilazimishe afanane na wengine
 
CWR2016

JF-Expert Member
Dec 14, 2017
2,039
2,000
Mama yupo sahihi,mambo ya kuropokeana na maamuzi ya kejeri mbele ya kadamnasi yanatweza utu,kila mtu ana style yake ya uongozi,tusilazimishe afanane na wengine
Sasa ni mangapi ameshaamua huko ndani na hatujui?!, au hadi aandae konakona ndio tutakuja kustuka
 
CWR2016

JF-Expert Member
Dec 14, 2017
2,039
2,000
Kuna jambo zito hapa.

Hata vyombo vya habari havitaki kuligusa!

Halafu tunaambiwa Mbunge wa Sengerema anatishiwa maisha, kwa kuzungumzia mambo yahusuyo eneo hilo hilo la nishati, si maajabu haya?
Kuna mengi nchi hii "yamefunguliwa".
 
CWR2016

JF-Expert Member
Dec 14, 2017
2,039
2,000
Kwenye korona naona kuna kauzaifu au labda wamegundua kuwa hata hizo hatua tulizoimizwa toka mwanzo tuchukue labda hazisaidii, kama hatua hizo zinasaidia kweli sioni sababu ya kutoimiza watu kunawa mikono kila mahali na kuagiza wakuu wa mikoa wasimamie hilo jambo, sioni sababu ya kutohimiza uvaaji wa barakoa labda tu kama wamegundua kuwa hazina msaada.
Ni udhaifu mkubwa. Jiulize kwa nini 'CREW' yake tu ndio huwa inavaa barakoa kila mahali! Eti wananchi wanaachwa wajiongoze wenyewe!
Kwa nini isiwe lazima kwa wanachi wote,

Ni uongozi gani huo wa kujijali peke yako...
 
Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
14,673
2,000
Mama yupo sahihi,mambo ya kuropokeana na maamuzi ya kejeri mbele ya kadamnasi yanatweza utu,kila mtu ana style yake ya uongozi,tusilazimishe afanane na wengine
Unakuta Doctor anayefanya kazi usiku kucha akitibu wagonjwa anatukanwa na mwanasiasa mmoja kapata sifuri mtihani wa form four kisa tu ni diwani au mkuu wa wilaya. Ile huwa ni dharau mbaya kwa utu wa mtu.
 
Sheikh23

JF-Expert Member
Jul 11, 2016
861
1,000
Unakuta Doctor anayefanya kazi usiku kucha akitibu wagonjwa anatukanwa na mwanasiasa mmoja kapata sifuri mtihani wa form four kisa tu ni diwani au mkuu wa wilaya. Ile huwa ni dharau mbaya kwa utu wa mtu.
Upo sahihi,japo hupaswi kuwa mnyonge sababu ya cheo cha mtu,ilhali upo kwenye haki Mungu atasimama nawewe
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom