Kwanini Rais akitaka kufanya jambo anazunguka sana kupata uhalali?

CWR2016

JF-Expert Member
Dec 14, 2017
2,072
2,000
Habari wana JF,

Tangu Mh. Rais ameshika madaraka, ameonekana akitaka kufanya jambo anatafuta "zuga" flani ili aeleweke.

Swali ninalojiuliza kwa nini asiwe anachukua msimamo na kulifanya jambo moja kwa moja?

Mfano:
1. Inafahamika kabisa swala la kuondolewa kwa "machinga" alishalipitisha siku nyingi tu. Na hii itakuwa operation katika majiji yote makubwa. Sasa Mh Rais akaona afunge ziara aende kariakoo, kisutu, n.k akidai eti ameenda kujionea. Hivi pale kariakoo alijionea nini kipya?

Pia ktk mpango huu, wameona ni lazima Halmashauri/jiji wachukue uendeshaji wa masoko yaliyo kwa viongozi au vyama vya masoko (mf. kariakoo shimoni). Sasa hili nalo badala ya kutamka tu, Yeye akasema ameenda, amesikia malalamiko, na akasimamisha uongozi ili soko liendeshwe na jiji. while inafahamika kabisa ni maamuzi walishayapanga.

Swali: Kwani Machinga Complex haipo chini ya Halmashauri?

2. Mfano namba mbili, ni ishu ya kupambana na corona. Inafahamika kabisa Mama alishakubaliana na swala la chanjo. Sasa namna alivyozunguka na kuunda tume utafikiri kweli, TUNAPAMBANA NA CORONA.

Swali la kumuuliza Mama, mbona hafafanyii kazi mapendekezo mengine, ila anafanyia kazi pendekezo moja tu la chanjo? vipi kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni, vipi physical distance, vipi uvaaji barakoa? Mbona si lazima? au uongozi ni kuvaa wewe tu? Kwa nini usingetamka kwamba tunafanya taratibu namna ya kupata chanjo, ukazunguka kuunda tume!!

3. Ishu ya Manji
Inafahamika kabisa ashapata 'clearance' huko juu. Pale TKKR mmempeleka ili asafishwe na kufanya "zuga" flani.
Sasa kwa nini msimuache tu.

Najua ipo "zuga" unayowaandalia CHADEMA. Hahaha...

Binafsi hii style ya 'zunguka-zunguka' ili uamue jambo sioni haja yake. Simamia tu kile unachokiamini moja kwa moja.

Asante.
 

Naipendatz

JF-Expert Member
Jul 27, 2011
2,856
2,000
Unataka awe anaropoka ropoka hovyo kama mkemia? Mama ni mwanasiasa aliyepikwa na kupikika na miamba ya chama kwa muda usiopungua miaka 30! Tabia mojawapo ya wanasiasa ni kuuma na kupuliza, ili waendelee kukubalika angalau na makundi yote katika jamii. Huyo jamaa yako yeye alishasema siyo mwanasiasa (Japo inashangaza mtu siyo mwanasiasa and anagombea posts za kisiasa!!).
 

CWR2016

JF-Expert Member
Dec 14, 2017
2,072
2,000
Unataka awe anaropoka ropoka hovyo kama mkemia? Mama ni mwanasiasa aliyepikwa na kupikika na miamba ya chama kwa muda usiopungua miaka 30! Tabia mojawapo ya wanasiasa ni kuuma na kupuliza, ili waendelee kukubalika angalau na makundi yote katika jamii. Huyo jamaa yako yeye alishasema siyo mwanasiasa (Japo inashangaza mtu siyo mwanasiasa and anagombea posts za kisiasa!!).
Sio kuropoka. Huoni anaingia hadi gharama kwa "zuga" zake. Atamke tu kwa kujiamini. Mbona tunampenda tu na kumwelewa.
 

Bujibuji

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
61,209
2,000
3. Ishu ya Manji
Inafahamika kabisa ashapata 'clearance' huko juu. Pale TKKR mmempeleka ili asafishwe na kufanya "zuga" flani.
Sasa kwa nini msimuache tu...
Hapo nilipo bold panahitaji ufafanuzi wako
 

CWR2016

JF-Expert Member
Dec 14, 2017
2,072
2,000
SSH anajua anachofanya sio sahihi hivyo anaweka zuio hili iki back fire lawama zisifike kwake moja kwa moja, iwe alishauriwa vibaya na kamati, ni ka tabia fulani hivi cha kinafiki na wasiojiamini na misimamo yao.
JK alitumia sana ka utaratibu
 

Midevu

JF-Expert Member
Feb 11, 2012
237
500
Mkuu ulitaka kumpa lawama ukashindwa ndio ukaamua umlaumu kuwa hakupi nafasi ya kumlaumu?😁
 

White party

JF-Expert Member
May 5, 2015
887
1,000
Mbona sisis wajuba tunaona anafanya sawa tu, lazime ahamornize na wananchi wake kabla ya kufanya kitu kitakachowaumiza huo ndio uongozi! So far tuna amani mioyoni hayo mengine ya ziada tu
 

Kalamu1

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
11,042
2,000
3. Ishu ya Manji
Inafahamika kabisa ashapata 'clearance' huko juu. Pale TKKR mmempeleka ili asafishwe na kufanya "zuga" flani.
Sasa kwa nini msimuache tu.
Eeeh Bhwana, unasema kweli?

Mimi bado ninashangaa na lile tukio la Bomba la Mafuta Kigamboni, ni kama halipo kabisa, au ni sinema?

Inawezekana linanyimwa uzito stahiki ikiwa ni mbinu za kulififisha, kutokana na wazito wanaohusika nalo?
 

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
43,755
2,000
Kufa kwa Magufuli imekua nongwa, kila mtu atakufa, sioni sababu ya kusema Magufuli kafa as if yeye ndie mtu pekee wa kwanza na na mwisho kufa.

Sioni hii hoja kama inamhusisha Magufuli hadi atajwe kama kafa.

Tumieni hata akili ndogo mlizonazo basi.


Nyinyi wenye akili nyingi msingetamani Rais
Afanane na Magufuli huku mkijua haiwezekani...
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom