Mkuu, nje ya mada. Hivi kwa nini Mwl. Nyerere hakuwa muumini mkubwa wa demokrasia?
Aliandika kwamba demokrasia zipo za aina nyingi na Afrika kama bara lenye nchi changa nyingi inaweza kuwa na demokrasia yake ya nchi zenye vyama vimoja, na ikafanya kazi vizuri tu.
Baadaye miaka ya 1990s alibadili mawazo na kuwa mtu wa mwanzo kabisa katika CCM kujenga ushawishi kwamba muda wa kufanya demokrasia za vyama vingi umefika, na sababu zilizotufanya tukatae vyama vingi miaka ya 1960s hazipo tena.
Zaidi, Nyerere aliingia katika mtego wa utamu wa madaraka. Muandishi wa ki Martinique aliyeandika sana kuhusu ukoloni, hususan kitabu maarufu cha "The Wretched of The Earth", aliandika kuwa serikali nyingi kandamizi zilirithi mifumo na sheria za kikoloni badala ya kuivunja. Nyerere naye aliingia katika mtego huu. Sheria zile zile zilizokandamiza TANU na Waafrika wakati wa ukoloni, Nyerere alizitumia kukandamiza Watanzania kama kina Christopher Kasanga Tumbo na Joseph Kassela Bantu.
Christopher Kasanga Tumbo alikuwa kiongozi wa vyama vya wafanyakazi machachari aliyempinga vikali Nyerere miaka ya 1960s. Nyerere alijaribu kumuhonga kwa kumpa ubalozi wa Tanzania Uingereza. Kasanga Tunbo alivyorudi Tanzania kutoka ubalozini kwa kujua ubalizi ule ulikuwa ni mtego wa kisiasa kumuweka mbaki na Tanzania, Nyerere alimfunga kifungo cha kutotoka kijijini kwake. Kasanga Tumbo aliishia kuuza gongo ili ku survive. Alikuwa anasema yeye mwenyewe wala hizi si habari za kumpakazia. Wengine waliofungwa hivyo ni kina Chifu Makwaia na Joseph Kassela Bantu.
Jaji Francis Nyalali aliandika kirefu kuhusu sheria 40 kandamizi Tanzania ambazo nyingi bado zinayumika mpaka leo.
Professor Paul Bjerk kaandika vizuri kwa mizania habari hizi katika kitabu chake "Building a Peaceful Nation : Julius Nyerere And The Establishment of Sovereignty in Tanzania 1961- 1964"
Kifupi madaraka matamu na wale mnaowaona wanamapinduzi wa leo, muda wao wa kuwaandikia historia ukufika mtajua madudu yao mengi sana.
Umeona kama umeuliza swali la nje ya mada, lakini ukweli ni kwamba swali lako linaturudisha kwa Ibrahim Traore.
Ibrahim Traore amekataa kufanya uchaguzi mwaka 2024, anaendesha nchi kijeshi tu.
Sasa, kama anapendwa kweli na watu hivyo, kwa nini asifanye uchaguzi tu akawa rais wa kidemokrasia anayetawala kwa kura za watu na si kw amtutu wa bunduki?