UAE ina immigrants wengi, income inequality ipo baina ya Masheikh na wale immigrants, ila Raia wote wa nchi za gulf wanapata benefits ambazo huzipati popote Africa.
Mfano wa Benefits anazopata Raia wa UAE
1. Elimu bure
2. Afya Bure
3. Familia zote ambazo pato lake la mwezi ni chini ya AED 25,000 (Milioni 18 za kitanzania) wanawekwa kundi maalum na kupewa yafuatayo
-allowance ya nyumba ambayo ni AED 2500 (milioni 1. 8 kwa mwezi kupanga nyumba)
-Allowance kwa wenye miaka 45 ama zaidi bila kazi ambayo ni hadi AED 5000 (milioni 3.6 ya kujikimu vitu kama chakula, mavazi etc)
-Allowance kwa wanaotafuta kazi na hawaja pata, hawa pia wanapewa AED 5000 (milioni 3.6) ila kwa miezi 6 tu atafute kazi, kama hataki kazi hapewi hii allowance hadi afike miaka 45
- allowance ya Chakula asilimia 75 serikali inalipa
-Allowance ya Umeme kama unatumia chini ya Unit 4000 (😂) na maji kama unatumia chini ya Mageloni 26,000
- allowance ya Mama wa Nyumbani AED 3500
-Allowance ya watoto, wa kwanza AED 2400, wa pili AED 1600 na AED 800 mtoto wa 3 kuendelea
Source
u.ae
Hao kweli mkuu ulinganishe na nchi zetu hizi?