Kwanini picha ya kujaa Maji Bwawa la Nyerere haionekani google wakati huu, nini shida

mwanamabadiliko

JF-Expert Member
Oct 30, 2010
843
1,363
Tangu kuanza kujazwa maji katika bwawa la nyerere ni takribani mwaka mmoja umepita, na maendeleo ya ujenzi wa bwawa la nyerere limefikia asilimia takribani 90. Sasa toka maji yameanza kujazwa disemba 2022 maji yameingia mengi mno, na ujazo umefikia mita takribani 160+, hawa google kwanini hawaliweki hili bwawa kwenye picha za gugo earth, ukienda ile sehemu bwawa lilipojengwa unaona picha za zamani sana kiasi cha kwamba nikafikiri inawezekana serikali ya marekani na CIA kiujumla wameamua kuficha picha za sasa hivi za bwawa letu la nyerere.

Watalamu mbalimbali wa Google map na geography kiujumla wanadai zile picha za google huwa zinakuwa updated kila baada ya muda, lakini ndani ya huo muda mimi nilijenga nyumba zangu , ila naziona gugo, sasa wanajamvini maji ya bwawa la nyerere tunayaonaje gugo kama ilivyo kwenye bwawa la mtera ambalo hata ukicheki kwenye gugo earth satellite unaliona.

Kiufupi picha za sasa zinaonesha hamna maji, hawa google wanatuhujumu, angalia picha au nenda gugo map
 

Attachments

  • Stiglers thumbnail.png
    Stiglers thumbnail.png
    442.8 KB · Views: 5
  • mtera thumbnail.png
    mtera thumbnail.png
    579.4 KB · Views: 4
Ile SATELLITE inayo record picha za ulimwengu ina pita sehemu tofauti kwa nyakati tofauti..especially maeneo ya maporini huwa wanapuuzia sana kwani wanahis maendeleo yake ni uoto asilia yaani miti, hivyo haina haja kupitisha SATELLITE kila mwaka wakati porini miti ni ile ile..
 
Kama tungekuwa na Satellite yetu wenyewe tungeweza ku-update mabadiliko yatokanayo na kujaa kwa maji kwenye bwawa la Mwalimu Nyerere..... Ni kweli bwawa limejaa lakini halionekani kwenye ramani ya Dunia.
 
Ile SATELLITE inayo record picha za ulimwengu ina pita sehemu tofauti kwa nyakati tofauti..especially maeneo ya maporini huwa wanapuuzia sana kwani wanahis maendeleo yake ni uoto asilia yaani miti, hivyo haina haja kupitisha SATELLITE kila mwaka wakati porini miti ni ile ile..
That's the point. Mi ni mnazi mkubwa wa Google Earth tangu 2018. Nimekuwa nikifuatilia mabadiliko wanayoweka kila mwaka. In fact huwa wana-tend kufanya mabadiliko mwezi Aprili ya kila mwaka.
Kama ulivyosema wameweka nguvu zaidi katika maeneo yenye makazi. Na kadri Nchi au eneo lililoendelea ndivyo pia contents zinakuwa highly detailed. Ndiyo maana ukiangalia picha za miji ya Ulaya Magharibi hata small details zinapnekana kwa umaridadi ajabu.
Ila kama mtoa mada alivyoeleza mimi nilikuwa nikichungulia mara kwa mara ujenzi wa Bwawa lakini sikuwahi kuliona kutokana na sababu tajwa hapo juu.
 
Back
Top Bottom