Kwanini pamoja na kuwa Land Rover ni kampuni ya kiingereza lakini magari yake sio maarufu Uingereza?

Mukulu wa Bakulu

JF-Expert Member
Aug 12, 2014
4,052
12,906
Land Rover ni kampuni ya Uingereza, Land Rover ndio hutengeneza magari kama Range Rover, Discovery nk lakini kwenye taarifa ya Serikali magari ya kampuni hiyo hayako hata kwenye top 20 ya magari yanayopendwa Uingereza.

Angalia taarifa hii ya Mwezi December 2022, kwenye category zote za Pure Electric, pure Petrol ama hybrid cars Land Rover haipo.

Wataalamu, mnaweza kutusaidia kujua sababu ya waingereza kutokupenda magari yao?
20230107_194001.jpg
20230107_194021.png
 
Land Rover ni kampuni ya Uingereza, Land Rover ndio hutengeneza magari kama Range Rover, Discovery nk lakini kwenye taarifa ya serikali magari ya kampuni hiyo hayako hata kwenye top 20 ya magari yanayopendwa Uingereza.

Angalia taarifa hii ya Mwezi December 2022, kwenye category zote za Pure Electric, pure Petrol ama hybrid cars Land Rover haipo.

Wataalamu, mnaweza kutusaidia kujua sababu ya waingereza kutokupenda magari yao?
View attachment 2472266View attachment 2472267
Waingereza hawapendi hata nchi yao, ndo kisa cha wao kuwa na himaya kubwa ya makoloni duniani. Walikuwa wanafanya kila namna kuondoka nchini Uingereza, wakajikuta wanagundua mengi duniani, ikiwemo uwepo wa jamii zilizo nyuma kimaendeleo kwenye mabara mengine zinazoweza kutwaliwa na kutawaliwa.
 
Waingereza wengi ni watumiaji wa gari ndogo na sio SUV,sasa Landrover gari zake zote ni SUV,kule uingereza kuna gari kama Austin,Jaguar,Vauxhal n.k.ndizo zinazotumika sana...
Watu wanakurupuka kujibu tu. Uko sahihi. Kingine Land rover asilimia kubwa ni gari za gharama. Raia wengi ni tabaka la kati na chini hivyo gari nyingi Uingereza na dunia nzima ni tabaka la chini na kati.
Hakuna nchi duniani ambako Range rover au Land cruiser ni nyingi kuliko magari madogo ya chini.
Gari za Land rover ni hizi
Range rover
Discovery
Evoque
Jaguar aina zote
Discovery
Utaona zote ni tabaka la juu.
Gari za tabaka la chini UK ni Vauxhall, rover, Ford models fulani etc hizi zimejaa kibao mitaani UK
 
Watu wanakurupuka kujibu tu. Uko sahihi. Kingine Land rover asilimia kubwa ni gari za gharama. Raia wengi ni tabaka la kati na chini hivyo gari nyingi Uingereza na dunia nzima ni tabaka la chini na kati.
Hakuna nchi duniani ambako Range rover au Land cruiser ni nyimgi kuliko magari madogo ya chini.
Gari za Land rover ni hizi
Range rover
Discovery
Evoque
Jaguar aina zote
Discovery
Utaona zote ni tabaka la juu.
Gari za tabaka la chini UK ni Vauxhall,rover,Ford models fulani etc hizi zimejaa kibao mitaani UK
Hii hoja haina mashiko.
Mbona SUV ya magari mengine za gharama nyingi tu zinaonekana barabarani hata hapa Tanzania.

Halafu kwa mfano, Evoque sio large suv kama range, ni mid sized suv za daraja a kati, mbona hazionekani mtaani nyingi.
 
Back
Top Bottom