Kwanini Nyerere hakutaifisha seminari za Katoliki?

Kwanini Nyerere hakutaifisha seminari za Katoliki?

Status
Not open for further replies.
Mtoa ameuliza seminari za Kikatoliki (na sio shule za kawaida za kanisa, sijui St. Francis=pugu n.k)
kwasababu seminary ni shule za kufundishia mapadre watarajiwa. Na hazikuwa shule za watu wengine wote kama hizo Pugu, Tabora shools, Rugambwa etc. Malengo ya shule yalikuwa tofauti, labda kama alikuwa anataka kuupiga vita ukristo then na makanisa angefunga.
 
Uswahili ni kama ugonjwa vile...kuanzia asubuhi ni kupiga story na kazi kidogo...halafu kutafuta sifa sana
japo umeandika kwa kiswahili na mama yako alitongozwa kwa kiswahili,akakubali kushika ujauzito wako kwa kiswahili,akakulea kwa kiswahili na wewe umetongozwa kwa kiswahili ukatolewa bikira kwa kiswahili..wacha kunanga uswahili wakat umetawala maisha yako
 
Wao lengo lao lilikua ni kuandaa mapadre na sio washenzi wa tabia. Wewe uliamua tu kuwa mshenzi wa tabia na kama wangejua lengo lako ni kua mshenzi usingepata nafasi hiyo
Kama lengo ni kuandaa mapdre peke yake kwanini wasisome theology kuanzia o level na A level mpaka chuo kikuu ?? Kwanini kuna PCB,PCM,HGL,HKL,EGM na kadhalika ? Bora hata mimi nakubali ni mshenzi wa tabia ,hao ambao wewe unawaona watakatifu ,unajua kashfa zinazo isumbua kanisa sasa hivi ?? Wanaofanya si hao hao mapadri na ma sista ??
 
Sizungumzii tabia nazungumzia kuandaa Mapadre, kama wanavyoandaliwa wataalamu wengine kama walimu, mambo ya tabia sio lengo la muuliza swali.
Ulivyokuja kama nyati aliye jeruhiwa na kusema huzungumzii washenzi kama mimi ulikua na maana gani ??
Kwenye kuandaa hao mapadri tabia unaachaje kuizungumzia ?? Nilivyo sema mimi ni mshenzi wa tabia nilikua na maana yangu ungeuliza kwanini nimesema hivyo
 
Ulivyokuja kama nyati aliye jeruhiwa na kusema huzungumzii washenzi kama mimi ulikua na maana gani ??
Kwenye kuandaa hao mapadri tabia unaachaje kuizungumzia ?? Nilivyo sema mimi ni mshenzi wa tabia nilikua na maana yangu ungeuliza kwanini nimesema hivyo
Asiyejua ushenzi wa tabia ni nn angeuliza,
Siku njema.
 
Kufuatia Azimio la Arusha serikali ilitaifisha taasisi ikiwemo hospitali, vyuo,majengo n.k. vya watu binafsi na mashirika ya kidini. Lakini shule za seminari za Kikatoliki hazikuguswa nini sababu hasa?mwenye kujua naomba msaada.
NB:
Ieleweke si kila shule inayomilikiwa na katoliki ni Seminari (mfano; St. Francis High School = sasa Pugu Sec. hii haikuwa seminari per se).
Chemsheni bongo msitoe majibu laini laini kama kawaida ya watanzania, hii sio kipima joto cha ITV kubwabwaja utumbo hapa ni "pweinti" tu zinatakiwa.
watu wengine sijui akili zenu zikoje. hapa sijui unataka kusema nini. nadhani inatakiwa uelewe seminari ni shule ya aina gani ndio uweke huu uzi. naona kama uzi hauna miguu.
 
We ukiangalia majipu meengi kama hawa kina kitilya tibaijuka chenge the list is long woote ni vibaka kutoka seminary
 
Jamani kusoma seminari sio lazima uwe padri au sista ,eleweni maana yangu,kama lengo ni kuwa padri ,kusingekua na PCB,PCM,HGL,HKL nk watu wangesoma tu theology mwanzo mwisho

Kwa hiyo unataka kuiambiaje jamii kuwa ilikuwa kosa kutokuzitaifisha ????!

Huko kanisani huduma za PCB, HKL zipo na zinahitajika sana tu. Ni sawa na kusema jeshini watu wacheze gwaride na kujifunza silaha tu. Tusiwe na madaktari, mainjinia nk. Kanisa ni taasisi ina mahitaji ya jumla
 
japo umeandika kwa kiswahili na mama yako alitongozwa kwa kiswahili,akakubali kushika ujauzito wako kwa kiswahili,akakulea kwa kiswahili na wewe umetongozwa kwa kiswahili ukatolewa bikira kwa kiswahili..wacha kunanga uswahili wakat umetawala maisha yako

You have summarized well what is in your mind. Uswahili katika ubora wake
 
Hivi hao ma padre wanaokulana ni wazuri wa tabia ??
Mkuu UncleBen Tumsifu Yesu Kristo....We ni kijana wa Seminari ipi?
Kama umenisoma vizuri kwenye post yangu hapo juu nilisema "Vijana wanaostahilishwa kuwa mapadre japo hawakustahili"....hii ni sentensi ya kinyenyekevu mbele za Mungu,kwamba hata hao wanaokuwa Mapadre si kwamba wanastahili,bali wanastahilishwa tu,ili waweze kutangaza utukufu na sifa za Mungu.Ndio maana siku ya kiapo cha Upadre wao husema "Ee bwana ulichokianzisha ndani yangu ukitimize,si kwa ajili yangu,bali ni kwa sifa na utukufu wa jina lako,kwa maana mimi sistahili kwa lolote kuyashika yaliyo matakatifu yako"
 
Kwa hiyo unataka kuiambiaje jamii kuwa ilikuwa kosa kutokuzitaifisha ????!

Huko kanisani huduma za PCB, HKL zipo na zinahitajika sana tu. Ni sawa na kusema jeshini watu wacheze gwaride na kujifunza silaha tu. Tusiwe na madaktari, mainjinia nk. Kanisa ni taasisi ina mahitaji ya jumla
Kumbe hata hujui ni wapi mjadala wangu umeanzia ?? Kwa majibu yako hapa maana yake ni upo upande wangu ,mdau niliye mqoute alisema kwamba wote wanaopita seminari ni mapadre ndio nikamkatalia kwamba sio lazima wote wawe mapadre
 
Shule ngapi za waislam zilitaifishwa? Au hawakuwa nazo.. Madrasa zilitaifishwa?
 
Jambo la msingi ujue kuwa hata shule zilizokuwa zinamilikiwa na Kanisa Katoliki zilitaifishwa. Inabidi utofautishe yafuatayo.
1. Seminari ni shule maalum za kuandaa wasomi watumishi wa Kanisa kama vile Mapadri. masomo yaliyo mengi wanayosoma yanaendana na Theolojia na maadili ya kanisa husika. Waalimu wanaofundisha shule hizo ni Mapadri na Brothers. Kwa misingi hiyo maeneo hayo hayakuguswa pasipo kuangalia dhehebu kwa sababu yalifundisha Dini (Imani ya kuabudu.)
Shakidinkili Theolojia inafundishwa Seminari Kuu tu,huku chini ni elimu dunia tu,na kwa huku chini walimu si lazima wawe mapadre na mabruda.Hata walei pia hufundisha
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom