Kwanini Nyerere hakutaifisha seminari za Katoliki?

Status
Not open for further replies.

Biro

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2010
Messages
331
Points
250

Biro

JF-Expert Member
Joined Aug 27, 2010
331 250
Kufuatia Azimio la Arusha serikali ilitaifisha taasisi ikiwemo hospitali, vyuo,majengo n.k. vya watu binafsi na mashirika ya kidini. Lakini shule za seminari za Kikatoliki hazikuguswa nini sababu hasa?mwenye kujua naomba msaada.
NB:
Ieleweke si kila shule inayomilikiwa na katoliki ni Seminari (mfano; St. Francis High School = sasa Pugu Sec. hii haikuwa seminari per se).
Chemsheni bongo msitoe majibu laini laini kama kawaida ya watanzania, hii sio kipima joto cha ITV kubwabwaja utumbo hapa ni "pweinti" tu zinatakiwa.
Katika hali ya kawaida ungekuwa wewe ungetaifisha kwa mfano jengo au shule ambayo ipo ndani ya mazingira ya nyumba ya ibada? Kibasila secondary ya dsm ilikuwa ikiitwa st xavery... Ilitaifishwa na kulikuwa hostel ya kiume pale shule na za kike zilikuwa kule kanisani... Kwa hostel ilichukuliwa ile ya kiume tu ile ya kike sababu ilikuwa pale kanisani chang'ombe ikaachwa....Ukiyaangalia mazingira hayo utapata jibu.
 
kadoda11

JF-Expert Member
Joined
Jan 6, 2011
Messages
21,537
Points
2,000

kadoda11

JF-Expert Member
Joined Jan 6, 2011
21,537 2,000
We ukiangalia majipu meengi kama hawa kina kitilya tibaijuka chenge the list is long woote ni vibaka kutoka seminary
hata rais wako/wetu JPM ambaye pasi na shaka ndio rais bora zaidi kwa sasa ktk ukanda huu wa afrika mashariki.naye pia alipitia seminary na tena alitaka kuwa padre.kwa maelezo zaidi tafuta CV/historia yake.

sio wote waliopitia seminary Wapi kama hivyo ulivyosema.
 
Msambichaka Mkinga

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2015
Messages
1,403
Points
2,000

Msambichaka Mkinga

JF-Expert Member
Joined Oct 22, 2015
1,403 2,000
Mtoa ameuliza seminari za Kikatoliki (na sio shule za kawaida za kanisa, sijui St. Francis=pugu n.k)
Huyu aliyeleta mada hii nadhani hana uelewa hata kidogo wa malengo na kazi za seminari za wakatoliki.

Yaweke kichwani haya ninayoyaweka hapa chini yatakusaidia siku nyingine:

Kanisa Katoliki lina shule na vyuo vya ngazi mbalimbali kwaajili ya kila anayependa kusoma katika taasisi hizo. Hizi ni shule na vyuo vya kawaida lakini vinamilikiwa na Kanisa Katoliki. Hizi ni moja ya taasisi za kijamii zinazomilikiwa na kanisa.

Shule zinazoitwa Seminari na Seminari Kuu ni maalum kwaajili ya kuwapata mapadre. Shule hizi haruhusiwi kusoma mtu yeyote uwe mkristo, muislam au mpagani kama dhamira yako siyo kuja kuwa padre. Na ili kusoma katika shule hizi, unatakiwa upitie kwenye mfumo wa Kanisa uliowekwa, na assessment huendelea wakati wote mpaka utakapokuja kuwa padre, japo mwanafunzi akiwa katika hatua mbalimbali anaweza kuachishwa au yeye mwenyewe kuacha kama itagundulika kuwa wito wa kuja kuwa padre haupo tena.

Kwa hiyo Seminari siyo miongoni mwa taasisi za kijamii zinazomilikiwa na Kanisa bali ni taasisi za kidini. Kuzitaifisha Seminari za Kikatoloki ingekuwa ni sawa na kutaifisha kanisa au msikiti. Maana shule hizo zipo kwaajili ya maendeleo ya kiimani na siyo maendeleo ya kijamii.
 
Matola

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2010
Messages
40,139
Points
2,000

Matola

JF-Expert Member
Joined Oct 18, 2010
40,139 2,000
Ndio walikuwa navyo, Tambaza, Azania Kisutu na Zanaki zilikuwa za Waislam (Aga Khan Muslim) nadhani pia walikuwa na shule Mwanza na Musoma zilizotaifishwa
Hawa wanavaa sutu na kuongea kingereza, sidhani kama wavaa kandambiri wanawahesabu kama ni waislamu wenzao. Agha Khan mwenyewe anaishi Paris Ufaransa.
 
Ngalikihinja

JF-Expert Member
Joined
Sep 1, 2009
Messages
20,569
Points
2,000

Ngalikihinja

JF-Expert Member
Joined Sep 1, 2009
20,569 2,000
Kufuatia Azimio la Arusha serikali ilitaifisha taasisi ikiwemo hospitali, vyuo,majengo n.k. vya watu binafsi na mashirika ya kidini. Lakini shule za seminari za Kikatoliki hazikuguswa nini sababu hasa?mwenye kujua naomba msaada.
NB:
Ieleweke si kila shule inayomilikiwa na katoliki ni Seminari (mfano; St. Francis High School = sasa Pugu Sec. hii haikuwa seminari per se).
Chemsheni bongo msitoe majibu laini laini kama kawaida ya watanzania, hii sio kipima joto cha ITV kubwabwaja utumbo hapa ni "pweinti" tu zinatakiwa.
Mkuu nimekuelewa...lakini je,
1. madrasa zilitaifishwa..??
2. huoni kuwa nia haioiwa kutaifisha shule zinazotoa elimu ya dini husika..?
 
Bijou

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2011
Messages
1,194
Points
1,250

Bijou

JF-Expert Member
Joined Feb 25, 2011
1,194 1,250
Kufuatia Azimio la Arusha serikali ilitaifisha taasisi ikiwemo hospitali, vyuo,majengo n.k. vya watu binafsi na mashirika ya kidini. Lakini shule za seminari za Kikatoliki hazikuguswa nini sababu hasa?mwenye kujua naomba msaada.
NB:
Ieleweke si kila shule inayomilikiwa na katoliki ni Seminari (mfano; St. Francis High School = sasa Pugu Sec. hii haikuwa seminari per se).
Chemsheni bongo msitoe majibu laini laini kama kawaida ya watanzania, hii sio kipima joto cha ITV kubwabwaja utumbo hapa ni "pweinti" tu zinatakiwa.
Forodhani Secondary ilikuwa ni Kinondoni Muslim???
 
mafutamingi

JF-Expert Member
Joined
Feb 14, 2011
Messages
1,721
Points
2,000

mafutamingi

JF-Expert Member
Joined Feb 14, 2011
1,721 2,000
Nyerere hakutaifisha Seminari yoyote. Alitaifisha shule na si seminari. Kama ipo aliyotaifisha iweke mezani.
Kufuatia Azimio la Arusha serikali ilitaifisha taasisi ikiwemo hospitali, vyuo,majengo n.k. vya watu binafsi na mashirika ya kidini. Lakini shule za seminari za Kikatoliki hazikuguswa nini sababu hasa?mwenye kujua naomba msaada.
NB:
Ieleweke si kila shule inayomilikiwa na katoliki ni Seminari (mfano; St. Francis High School = sasa Pugu Sec. hii haikuwa seminari per se).
Chemsheni bongo msitoe majibu laini laini kama kawaida ya watanzania, hii sio kipima joto cha ITV kubwabwaja utumbo hapa ni "pweinti" tu zinatakiwa.
 
Nyenyere

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2010
Messages
11,924
Points
2,000

Nyenyere

JF-Expert Member
Joined Sep 9, 2010
11,924 2,000
Kufuatia Azimio la Arusha serikali ilitaifisha taasisi ikiwemo hospitali, vyuo,majengo n.k. vya watu binafsi na mashirika ya kidini. Lakini shule za seminari za Kikatoliki hazikuguswa nini sababu hasa?mwenye kujua naomba msaada.
NB:
Ieleweke si kila shule inayomilikiwa na katoliki ni Seminari (mfano; St. Francis High School = sasa Pugu Sec. hii haikuwa seminari per se).
Chemsheni bongo msitoe majibu laini laini kama kawaida ya watanzania, hii sio kipima joto cha ITV kubwabwaja utumbo hapa ni "pweinti" tu zinatakiwa.
kwani alitaifisha madrasa pia?
 
Balantanda

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2008
Messages
12,405
Points
2,000

Balantanda

JF-Expert Member
Joined Jul 13, 2008
12,405 2,000
Kufuatia Azimio la Arusha serikali ilitaifisha taasisi ikiwemo hospitali, vyuo,majengo n.k. vya watu binafsi na mashirika ya kidini. Lakini shule za seminari za Kikatoliki hazikuguswa nini sababu hasa?mwenye kujua naomba msaada.
NB:
Ieleweke si kila shule inayomilikiwa na katoliki ni Seminari (mfano; St. Francis High School = sasa Pugu Sec. hii haikuwa seminari per se).
Chemsheni bongo msitoe majibu laini laini kama kawaida ya watanzania, hii sio kipima joto cha ITV kubwabwaja utumbo hapa ni "pweinti" tu zinatakiwa.
Kuna tofauti kubwa sana kati ya seminari na shule zingine za sekondari...Seminari ni shule maalum ambazo pamoja na kufundisha elimu/masomo ya kawaida pia zinawalea vijana ambao baadae huwa mapadre...Kuna junior seminary na Major seminary...

Kuna shule za sekondari za kikatoliki (sio seminari) ambazo zilichukuliwa na serikali...Mfano ni shule ya sekondari Sangu ya Mbeya
 
Babuyao

JF-Expert Member
Joined
Jun 6, 2009
Messages
1,732
Points
1,225

Babuyao

JF-Expert Member
Joined Jun 6, 2009
1,732 1,225
Seminari (seminarium kwa kilatin) maana yake kitalu kunakopandwa mbegu za wito wa upadre, wito wa kuwa mtumishi wa Mungu. Huko ndiko mbegu changa ya wa vijana wenye wito huo hulelewa mpaka kukomaa na kuzaa matunda (kuufikia upadre). Shule hizi ni maalum kwa kazi hiyo. Kumbe ratiba zake na mitaala yake (kwa seminari ndogo) zinatofautiana kwa kiasi kikubwa na sekondari za kawaida hata zile zilizo chini ya kanisa katoliki. Mitaala yake inajumlisha elimu ya kawaida (elimu dunia) ya sekondari na pia elimu au malezi ya pekee ya kipadre, ambapo unakuta kwenye ratiba vijana wanashiriki kwa pamoja na uzito mkubwa sala ya Kanisa (breviari), wanasali rozari bila kukosa, wanashiriki misa takatifu kila siku, wanasoma mambo ya kiroho kwa msisitizo mkubwa, wanalelewa katika useja, wana walezi wao wa kiroho ambao ni mapadre, nk. Haya yote yanawatofautisha sana na shule au sekondari zingine hata zile za kikatoliki ambazo siyo seminari.
Isingekuwa rahisi kuzitaifisha shule hizi na kuzifanya kila mwanafunzi ajiunge nazo kwani mkazo wake, mitaala yake, na ratiba zake ni za kipekee kwa ajili ya watu wa pekee. Ndiyo maana kwa kujua hilo Mwalimu aliziacha zibaki kwa ajili ya malengo hayo.
 
Status
Not open for further replies.

Forum statistics

Threads 1,389,914
Members 528,056
Posts 34,038,496
Top