UncleBen
JF-Expert Member
- Oct 27, 2014
- 9,597
- 11,991
Milele aminaMkuu UncleBen Tumsifu Yesu Kristo....We ni kijana wa Seminari ipi?
Kama umenisoma vizuri kwenye post yangu hapo juu nilisema "Vijana wanaostahilishwa kuwa mapadre japo hawakustahili"....hii ni sentensi ya kinyenyekevu mbele za Mungu,kwamba hata hao wanaokuwa Mapadre si kwamba wanastahili,bali wanastahilishwa tu,ili waweze kutangaza utukufu na sifa za Mungu.Ndio maana siku ya kiapo cha Upadre wao husema "Ee bwana ulichokianzisha ndani yangu ukitimize,si kwa ajili yangu,bali ni kwa sifa na utukufu wa jina lako,kwa maana mimi sistahili kwa lolote kuyashika yaliyo matakatifu yako"
Nashukuru mkuu wewe ndio umenijibu vizuri ,niliposema mimi ni mshenzi wa tabia wengi hawakunielewa ,badala yake hawakutaka kuniuliza kwanini nimesema hivyo wakaanza kuni atack kana kwamba wale wanaofanywa kuwa mapadre ni watakatifu ,kumbe hata wao sio kwamba wanastahili bali ni wanastahilishwa ,kwa kiapo hicho ambacho wengi wa wachangiaji walikua hawakijui ama wanakijua wakaamua tu kupuuza na kuniona mimi ni mkosaji mkubwa sana niliposema mimi ni mshenzi wa tabia