Kwanini Nyerere hakutaifisha seminari za Katoliki?

Status
Not open for further replies.
Umbwe, Kwiro mbona zilitaifishwa? Tena tunataka serikali irudiashe shule za serikali maaana watu hata shukrani hawana
 
Kufuatia Azimio la Arusha serikali ilitaifisha taasisi ikiwemo hospitali, vyuo,majengo n.k. vya watu binafsi na mashirika ya kidini. Lakini shule za seminari za Kikatoliki hazikuguswa nini sababu hasa?mwenye kujua naomba msaada.
Moja ya maswali ya kipumbavu sana humu JF. Kazi ya seminary ni kutoa mafunzo kwa makasisi wanaotumikia kanisa, sasa angetaifisha Mapadri na Masista wangetoka wapi? Hamjaridhika tu na shule zoooote alizotaifisha zinazomilikiwa na kanisa?
 
Kufuatia Azimio la Arusha serikali ilitaifisha taasisi ikiwemo hospitali, vyuo,majengo n.k. vya watu binafsi na mashirika ya kidini. Lakini shule za seminari za Kikatoliki hazikuguswa nini sababu hasa?mwenye kujua naomba msaada.

sio zimetaifishwa serikali ilichukua kwa nguvu but still hati za shule hizo zipo kanisani,refer mgogoro wa ndanda!
serikali imeonekana imeshindwa kuziongoza hizo shule walizozichukua sasa kanisa zinadai shule zake tumeanza na forodhani(now st joseph cathedral)imerudi

pugu(st francis) inafuata

n.k
 
Kufuatia Azimio la Arusha serikali ilitaifisha taasisi ikiwemo hospitali, vyuo,majengo n.k. vya watu binafsi na mashirika ya kidini. Lakini shule za seminari za Kikatoliki hazikuguswa nini sababu hasa?mwenye kujua naomba msaada.

Kuna taasisi nyingi sana za kidini zilitaifishwa kipindi kile akilenga kusaidia kutoa elimu kwa watanzania bila kuzingatia suala la dini. Pugu Sekondari, Minaki, Tosamaganga, Forodhani (St. Joseph ya sasa), Ndanda High school na nyingine nyingi zilikuwa za kanisa katoloki lakini zilichukuliwa. Seminari ni tofauti kwa sbb malengo yake siyo kutoa elimu ya sekondari bali kuandaa viongozi wa kidini
 
Kufuatia Azimio la Arusha serikali ilitaifisha taasisi ikiwemo hospitali, vyuo,majengo n.k. vya watu binafsi na mashirika ya kidini. Lakini shule za seminari za Kikatoliki hazikuguswa nini sababu hasa?mwenye kujua naomba msaada.
Jibu ni rahisi sana. Serikali haina dini wakati lengo kuu la shule za seminari ni kufundisha mapadre. Kama serikali ingetaifisha shule za seminari maana yake mapadre wangekuwa wa serikali au kama ingebadirisha lengo lake basi mapadre wasingekuwepo tena. Mtu yeyote anayehitimu katika shule za seminari anakuwa padre
 
Mleta mada inaonekana kama umesoma basi umesoma sekondari ya Kata.Nakutajia shule mojawapo iliyotaifishwa miaka ya sitini mwishoni ni Kantalamba Sekondari.Kama huna takwimu ulizofanyia utafiti usikurupuke kuandika na kusema
 
Watanzania ni wavivu kufikiri, mtoa mada kauliza kwa nin SEMINARI za KATOLIKI hazikutafishwa mtu anakuja kusema zilitaifishwa ikiwemo Forodhani? Really? Forodhani ilikuwa SEMINARI toka lini? TOFAUTISHENi SEMINARI vs SHULE ZA KAWAIDA ZA KANISA> Takbiiiriiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii..................
 
Kufuatia Azimio la Arusha serikali ilitaifisha taasisi ikiwemo hospitali, vyuo,majengo n.k. vya watu binafsi na mashirika ya kidini. Lakini shule za seminari za Kikatoliki hazikuguswa nini sababu hasa?mwenye kujua naomba msaada.
Pugu Secondary School ilikuwa katoliki kabisa na leo ipo serikalini. Forodhan pia ilikuwa katoliki, middle schools zote zilikuwa za kikatoliki, rudi kwenye data
 
Watanzania ni wavivu kufikiri, mtoa mada kauliza kwa nin SEMINARI za KATOLIKI hazikutafishwa mtu anakuja kusema zilitaifishwa ikiwemo Forodhani? Really? Forodhani ilikuwa SEMINARI toka lini? TOFAUTISHENi SEMINARI vs SHULE ZA KAWAIDA ZA KANISA> Takbiiiriiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii..................
Tafuta google. What is a seminary ndo uje tena.
 
Jibu ni rahisi sana. Serikali haina dini wakati lengo kuu la shule za seminari ni kufundisha mapadre. Kama serikali ingetaifisha shule za seminari maana yake mapadre wangekuwa wa serikali au kama ingebadirisha lengo lake basi mapadre wasingekuwepo tena. Mtu yeyote anayehitimu katika shule za seminari anakuwa padre
Hapana sio mtu yeyote anapitia seminari anakua padre ,mimi nimepita seminari lakini ni mshenzi tu wa tabia
 
seminary ziko kanisani, kutaifisha seminary ina maana angechukua na kanisa. Ila zilizokuwa nje ya kanisa zilitaifishwa. Shule nyingi za middle school zilikuwa zawakatolik na zilichukuliwa. Kama Pugu umetajiwa St mary's siku hizi mnaita Tabora girls na boys. nk.
zilijengwa kwa kodi ambayo mkoloni alikusanya kwa watu wa iman zote na kuwapa wamisionari
 
Pugu Secondary School ilikuwa katoliki kabisa na leo ipo serikalini. Forodhan pia ilikuwa katoliki, middle schools zote zilikuwa za kikatoliki, rudi kwenye data
hela ya kujenga na kuendesha ilitoka kwa mkoloni ambayo ni kodi toka kwa watu wote
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom