Kwanini Nyerere hakutaifisha seminari za Katoliki?

Status
Not open for further replies.
Kufuatia Azimio la Arusha serikali ilitaifisha taasisi ikiwemo hospitali, vyuo,majengo n.k. vya watu binafsi na mashirika ya kidini. Lakini shule za seminari za Kikatoliki hazikuguswa nini sababu hasa?mwenye kujua naomba msaada.

Kuna taasisi nyingi sana za kidini zilitaifishwa kipindi kile akilenga kusaidia kutoa elimu kwa watanzania bila kuzingatia suala la dini. Pugu Sekondari, Minaki, Tosamaganga, Forodhani (St. Joseph ya sasa), Ndanda High school na nyingine nyingi zilikuwa za kanisa katoloki lakini zilichukuliwa. Seminari ni tofauti kwa sbb malengo yake siyo kutoa elimu ya sekondari bali kuandaa viongozi wa kidini

Asante kwa maelezo makini sana....

huyu mleta. maada....nadhani akisoma hapo hawakuwa na swali lingine juu ya hili alouliza....

ubarikiwe sana mkuu...
 
Kufuatia Azimio la Arusha serikali ilitaifisha taasisi ikiwemo hospitali, vyuo,majengo n.k. vya watu binafsi na mashirika ya kidini. Lakini shule za seminari za Kikatoliki hazikuguswa nini sababu hasa?mwenye kujua naomba msaada.
NB:
Ieleweke si kila shule inayomilikiwa na katoliki ni Seminari (mfano; St. Francis High School = sasa Pugu Sec. hii haikuwa seminari per se).
Chemsheni bongo msitoe majibu laini laini kama kawaida ya watanzania, hii sio kipima joto cha ITV kubwabwaja utumbo hapa ni "pweinti" tu zinatakiwa.
Mwenyewe unaanza kubwabwaja utumbo, halafu unawaamuru wengine wasibwabwaje......! Unauliza swali huku unaonesha unataka majibu ya aina gani....!
Anyway, jaribu kutafuta nini maana ya "seminary" V/S "a private school", then from there utajua tu kwannini ilikuwa hivyo....! Si vibaya ukapitia pia maana ya "madrasa"....!
 
Hivi St. Anthony's Sec. School - Mbagala vs Nyegezi Seminary (Mwanza) au Maua Seminary ni sawa? Watanzania wazito mno kuelewa aisee ndo maana wakenya wanatudharau jitu halijui tofauti halafu linakuja kujamba jamba tu. Daah hivi mkoloni si alipata kazi sana kututawala? na JPM kweli atawaweza hawa mamburula!!!

Hivi kweli unajua maana ya seminari?,...

ni nini hasa dhumuni la kanisa kujenga seminary?...

na Je unajua maana ya misikiti kuwa na madrasa?..

ukiyajua hayo hutauliza maswali ya kipumbavu kiasi hicho .....

umepewa majibu mzuri lakini huyasomi....lengo lako ni nini?
 
Hapana sio mtu yeyote anapitia seminari anakua padre ,mimi nimepita seminari lakini ni mshenzi tu wa tabia
Wao lengo lao lilikua ni kuandaa mapadre na sio washenzi wa tabia. Wewe uliamua tu kuwa mshenzi wa tabia na kama wangejua lengo lako ni kua mshenzi usingepata nafasi hiyo
 
Exac

Exactly, kuna watu wana vichwa vibovu.
 
Seminari ni vituo maalum vya Kanisa kwa ajili kufundishia viongozi wenye wito wa kulitumikia Kanisa. Kutaifisha ingekuwa sawa na kutaifisha majengo ya makanisa!
Mkuu umenena point halisi ya kwanini ikawa hivyo!
 
Mkuu blessings mimi ndugu yako,unajuwa wapi huwa tunakutana...
Ipo hivi,Seminary ni mahali pa kuandaa Vijana wabatizwa wa kanisa katoliki ambao wanapaswa kuja kuwa Mapadre baadae.Vijana hawa huandaliwa kuanzia ngazi ya Kigango,parokia na hatimaye jimbo.Kwa ngazi ya Kigango Katekista ndio msimamizi wa malezi yao,kwa ngazi ya parokia Paroko ndio msimamizi wao na kwa ngazi ya Jimbo,Mkurugenzi wa Miito wa Jimbo(Vocation Director) ndio huchukua jukumu hili kwa niaba ya Baba Askofu.Ili uwe mseminari ni lazima uwe mkristo mkatoliki uliyepata sacramenti zote muhimu kama ubatizo,komunyo na kipaimara.

Hivyo Seminari hizi hulea vijana walio wakatoliki tu bila mchanganyiko na dini nyingine.Mara chache Seminari nyingine huchukua Mabruda au Masista wa mashirika ya kikatoliki wanaotaka kujiendeleza kielimu.Seminari hizi zipo kwa hatua,hatua hizo ni kama zifuatazo
1)Preparatory Seminary
2)Junior Seminary
3)Major Seminary
Hiyo ya kwanza Vijana hukaa mwaka mmoja kabla ya kuingia kidato cha kwanza,huchukuliwa mara tu ya kumaliza darasa la saba,hapa vijana hulelewa na kutayalishwa kuingia Junior Seminary.Mfano Jimbo la Njombe Pre-Seminary ipo Matola,Jimbo la Iringa ipo Tosamaganga,Jimbo la Kigoma ipo Itelambogo n.k
Junior Seminary hujumuisha kidato cha kwanza mpaka cha sita.Hapa kijana huandaliwa kwa kupata elimu dunia na kidogo elimu ahera.Mitaala yake ni ya serikali na hufanya kazi chini ya miongozo ya baraza la Mitihani la Taifa.Mfano wa Junior Seminaries ni kama Visiga Seminari Jimbo la Dsm,St.Peter's Junior Seminari Jimbo la Moro,Kasita Seminari Jimbo la Mahenge,Kaengesa Seminari Jimbo la S'wanga,Bihawana Seminari Jimbo la Dodoma,Rubya Seminari Jimbo la Bukoba,Katoke Seminari Jimbo la Rulenge,Mafinga Seminari Jimbo la Iringa,Kilocha Seminari Jimbo la Njombe,Nyegezi Seminari Mwanza,Makoko Seminari Musoma kwa kutaja kwa uchache.Ikumbukwe kuwa kuna Seminari za Jimbo na Seminari za Mashirika ya dini ya kikatoliki,ambazo huandaa mapadre wa Jimbo la Mapadre ya Shirika kwa kufuata nadhiri za mashirika,Mafano wa Seminari za Mashirika ni St.Francis De Sales ya Morogoro,Maua Seminary ya Moshi,Don Bosco Seminary na Hanga Seminari ya Shirika la Benedictine's Fathers Songea.

Major Seminary(Seminari Kuu),hapa hasaa huandaliwa vijana waliomaliza kidato cha sita na sasa wanataka kuendelea kwa dhati na wito wa Upadre,huku vijana huenda kusoma masomo ya Taihudi(Theology) na Falsafa(Philosopy),mara nyingi husoma Falsafa kwa miaka mitatu na Taihudi kwa miaka minne,na baadae mwaka mmoja wa kichungaji,tena ushemasi na mwaka wa nane au wa tisa baada ya safari ya seminari kuu,kwa kadiri ya majiundo ya kimwili na kiroho kijana "hustahilishwa" kupata daraja la Upadre japo kwa ubinadamu wetu hakuna ambae "hustahili".Kwa Seminary nyingi Afrika zimekuwa affiliated na University Seminaries za Ulaya na hasa Rome Italy,hivyo Miaka mitatu ya theology huwa degree ya kwanza na miaka minne ya falsafa huwa ni degree ya pili(Hivyo padre yoyote huwa na degree mbili kabla ya kupadirishwa).Mfano wa Major Seminary (Simanari Kuu) kwa Tz ni Peramiho Major Seminary,Kipalapala Major Seminary Tabora,Segerea Major Seminary Dsm,Ntungamo Major Seminary Bukoba na Kibosho Seminary Moshi,hizi ni zile za Jimbo.Seminary Kuu za Mashirika kwa Tz ipo moja tu ambayo ni Salvatorian Major Seminary Morogoro ambayo bila shaka kwa sasa ndio Jordan University College.

Hivyo wakati wa kutaifisha,Nyerere hakuwa na ulazima wa kuzichukua Junior Seminary sababu kwanza hazikuwa mali ya Serikali na wala hazikuendeshwa na kodi za Watanganyika.Pia hazikujumuisha watu wa dini tofauti,kabla ya miaka ya 1990's mwishoni,Junior Seminary zilikuwa zinapata misaada toka Vatican ili kuziemdesha,ndio maana ada zake zilikuwa ndogo sana,Mfuko huu uliitwa "Vatican Propagandum Fide" yaani Vatican Propagation of Faith.Hivyo pesa za chakula na majengo na kila kitu zilitoka Rome.Baadae Pope John the Second akasema inatosha,Afrika sasa ijitegemee.Hivyo hii hali ya MCC na Serikali ya Tz kwa sasa kanisa ilishaianza zamani.Ndio maana siku hizi Kanisa Katoliki la Tz linajiendesha bila misaada "mikuu" toka Rome.Hivyo Nyerere alikosa uhalali wa kuzikomba Seminary ila alipata uhalali wa kuchukua shule za dini tu,japo kuna maeneo hata "Seminary" kanisa liliamua kumuachia Nyerere la lenyewe kwenda kujenga Seminary nyingine mpya.Mfano Tosamaganga ilikuwa inaandaa Mapadre wa Jimbo la Iringa lkn baada ya sera hii Kanisa liliiacha shule na kwenda Mafinga kujenga Junior Seminary yake ambayo ndio Mafinga Seminary.Hawa kina Mahiga waziri wa Mambo ya Nje ni kizazi cha mwanzo kuifungua Mafinga Seminary baada ya Kanisa kuichia Seminary ya Tosa kwa serikali na wao wakabaki na Preparatory seminary eneo la chini la Tosa.Kule S'wanga Kigonsera ilikuwa Semanary na ndio alisoma Rais Mkapa na Mh.Pinda,lkn kanisa likagawa na kwenda kujenga Kahengesa Seminary.Mifano ipo mingi sana,tafadhari ndugu yangu blessings uwe unajiridhisha kwanza kabla hujaaandika

Nakutakia siku njema,kama bado una swali basi karibu......Wabilakh Tawufiq!!!
 
Shule za seminari ni mahsusi kwa ajili ya kuwaandaa Mapadre na watawa wa kanisa katoliki,ukizitaifisha viongozo hawa watatoka wapi?uendeshaji wake ni wa kikanisa na misingi yake pia.
 
Duuuuh....Tumsifu Yesu Kristo Padre Ngaliba Dume....Upo deep mkuu!!maneno kama majiundo,kustahikishwa nk ni maneno ya Altareni haya..Umekamua kwelikweli
 
Kufuatia Azimio la Arusha serikali ilitaifisha taasisi ikiwemo hospitali, vyuo,majengo n.k. vya watu binafsi na mashirika ya kidini. Lakini shule za seminari za Kikatoliki hazikuguswa nini sababu hasa?mwenye kujua naomba msaada.
NB:
Ieleweke si kila shule inayomilikiwa na katoliki ni Seminari (mfano; St. Francis High School = sasa Pugu Sec. hii haikuwa seminari per se).
Chemsheni bongo msitoe majibu laini laini kama kawaida ya watanzania, hii sio kipima joto cha ITV kubwabwaja utumbo hapa ni "pweinti" tu zinatakiwa.
Nenda kavae mabomu isis.Badala ya kujadili mustakabali wa Taifa unajadili mambo ya mwaka "47".Bakwata wamejenga sekondari ngapi? vyuo vikuu vingipi? aibu aibu aibu!!!!!!
 
Mkuu blessings mimi ndugu yako,unajuwa wapi huwa tunakutana...
Ipo hivi,Seminary ni mahali pa kuandaa Vijana wabatizwa wa kanisa katoliki ambao wanapaswa kuja kuwa Mapadre baadae.Vijana hawa huandaliwa kuanzia ngazi ya Kigango,parokia na hatimaye jimbo.Kwa ngazi ya Kigango Katekista ndio msimamizi wa malezi yao,kwa ngazi ya parokia Paroko ndio msimamizi wao na kwa ngazi ya Jimbo,Mkurugenzi wa Miito wa Jimbo(Vocation Director) ndio huchukua jukumu hili kwa niaba ya Baba Askofu.Ili uwe mseminari ni lazima uwe mkristo mkatoliki uliyepata sacramenti zote muhimu kama ubatizo,komunyo na kipaimara.

Hivyo Seminari hizi hulea vijana walio wakatoliki tu bila mchanganyiko na dini nyingine.Mara chache Seminari nyingine huchukua Mabruda au Masista wa mashirika ya kikatoliki wanaotaka kujiendeleza kielimu.Seminari hizi zipo kwa hatua,hatua hizo ni kama zifuatazo
1)Preparatory Seminary
2)Junior Seminary
3)Major Seminary
Hiyo ya kwanza Vijana hukaa mwaka mmoja kabla ya kuingia kidato cha kwanza,huchukuliwa mara tu ya kumaliza darasa la saba,hapa vijana hulelewa na kutayalishwa kuingia Junior Seminary.Mfano Jimbo la Njombe Pre-Seminary ipo Matola,Jimbo la Iringa ipo Tosamaganga,Jimbo la Kigoma ipo Itelambogo n.k
Junior Seminary hujumuisha kidato cha kwanza mpaka cha sita.Hapa kijana huandaliwa kwa kupata elimu dunia na kidogo elimu ahera.Mitaala yake ni ya serikali na hufanya kazi chini ya miongozo ya baraza la Mitihani la Taifa.Mfano wa Junior Seminaries ni kama Visiga Seminari Jimbo la Dsm,St.Peter's Junior Seminari Jimbo la Moro,Kasita Seminari Jimbo la Mahenge,Kaengesa Seminari Jimbo la S'wanga,Bihawana Seminari Jimbo la Dodoma,Rubya Seminari Jimbo la Bukoba,Katoke Seminari Jimbo la Rulenge,Mafinga Seminari Jimbo la Iringa,Kilocha Seminari Jimbo la Njombe,Nyegezi Seminari Mwanza,Makoko Seminari Musoma kwa kutaja kwa uchache.Ikumbukwe kuwa kuna Seminari za Jimbo na Seminari za Mashirika ya dini ya kikatoliki,ambazo huandaa mapadre wa Jimbo la Mapadre ya Shirika kwa kufuata nadhiri za mashirika,Mafano wa Seminari za Mashirika ni St.Francis De Sales ya Morogoro,Maua Seminary ya Moshi,Don Bosco Seminary na Hanga Seminari ya Shirika la Benedictine's Fathers Songea.

Major Seminary(Seminari Kuu),hapa hasaa huandaliwa vijana waliomaliza kidato cha sita na sasa wanataka kuendelea kwa dhati na wito wa Upadre,huku vijana huenda kusoma masomo ya Taihudi(Theology) na Falsafa(Philosopy),mara nyingi husoma Falsafa kwa miaka mitatu na Taihudi kwa miaka minne,na baadae mwaka mmoja wa kichungaji,tena ushemasi na mwaka wa nane au wa tisa baada ya safari ya seminari kuu,kwa kadiri ya majiundo ya kimwili na kiroho kijana "hustahilishwa" kupata daraja la Upadre japo kwa ubinadamu wetu hakuna ambae "hustahili".Kwa Seminary nyingi Afrika zimekuwa affiliated na University Seminaries za Ulaya na hasa Rome Italy,hivyo Miaka mitatu ya theology huwa degree ya kwanza na miaka minne ya falsafa huwa ni degree ya pili(Hivyo padre yoyote huwa na degree mbili kabla ya kupadirishwa).Mfano wa Major Seminary (Simanari Kuu) kwa Tz ni Peramiho Major Seminary,Kipalapala Major Seminary Tabora,Segerea Major Seminary Dsm,Ntungamo Major Seminary Bukoba na Kibosho Seminary Moshi,hizi ni zile za Jimbo.Seminary Kuu za Mashirika kwa Tz ipo moja tu ambayo ni Salvatorian Major Seminary Morogoro ambayo bila shaka kwa sasa ndio Jordan University College.

Hivyo wakati wa kutaifisha,Nyerere hakuwa na ulazima wa kuzichukua Junior Seminary sababu kwanza hazikuwa mali ya Serikali na wala hazikuendeshwa na kodi za Watanganyika.Pia hazikujumuisha watu wa dini tofauti,kabla ya miaka ya 1990's mwishoni,Junior Seminary zilikuwa zinapata misaada toka Vatican ili kuziemdesha,ndio maana ada zake zilikuwa ndogo sana,Mfuko huu uliitwa "Vatican Propagandum Fide" yaani Vatican Propagation of Faith.Hivyo pesa za chakula na majengo na kila kitu zilitoka Rome.Baadae Pope John the Second akasema inatosha,Afrika sasa ijitegemee.Hivyo hii hali ya MCC na Serikali ya Tz kwa sasa kanisa ilishaianza zamani.Ndio maana siku hizi Kanisa Katoliki la Tz linajiendesha bila misaada "mikuu" toka Rome.Hivyo Nyerere alikosa uhalali wa kuzikomba Seminary ila alipata uhalali wa kuchukua shule za dini tu,japo kuna maeneo hata "Seminary" kanisa liliamua kumuachia Nyerere la lenyewe kwenda kujenga Seminary nyingine mpya.Mfano Tosamaganga ilikuwa inaandaa Mapadre wa Jimbo la Iringa lkn baada ya sera hii Kanisa liliiacha shule na kwenda Mafinga kujenga Junior Seminary yake ambayo ndio Mafinga Seminary.Hawa kina Mahiga waziri wa Mambo ya Nje ni kizazi cha mwanzo kuifungua Mafinga Seminary baada ya Kanisa kuichia Seminary ya Tosa kwa serikali na wao wakabaki na Preparatory seminary eneo la chini la Tosa.Kule S'wanga Kigonsera ilikuwa Semanary na ndio alisoma Rais Mkapa na Mh.Pinda,lkn kanisa likagawa na kwenda kujenga Kahengesa Seminary.Mifano ipo mingi sana,tafadhari ndugu yangu blessings uwe unajiridhisha kwanza kabla hujaaandika

Nakutakia siku njema,kama bado una swali basi karibu......Wabilakh Tawufiq!!!

Umeeleweka vizuri sana
 
Kufuatia Azimio la Arusha serikali ilitaifisha taasisi ikiwemo hospitali, vyuo,majengo n.k. vya watu binafsi na mashirika ya kidini. Lakini shule za seminari za Kikatoliki hazikuguswa nini sababu hasa?mwenye kujua naomba msaada.
NB:
Ieleweke si kila shule inayomilikiwa na katoliki ni Seminari (mfano; St. Francis High School = sasa Pugu Sec. hii haikuwa seminari per se).
Chemsheni bongo msitoe majibu laini laini kama kawaida ya watanzania, hii sio kipima joto cha ITV kubwabwaja utumbo hapa ni "pweinti" tu zinatakiwa.
Jambo la msingi ujue kuwa hata shule zilizokuwa zinamilikiwa na Kanisa Katoliki zilitaifishwa. Inabidi utofautishe yafuatayo.
1. Seminari ni shule maalum za kuandaa wasomi watumishi wa Kanisa kama vile Mapadri. masomo yaliyo mengi wanayosoma yanaendana na Theolojia na maadili ya kanisa husika. Waalimu wanaofundisha shule hizo ni Mapadri na Brothers. Kwa misingi hiyo maeneo hayo hayakuguswa pasipo kuangalia dhehebu kwa sababu yalifundisha Dini (Imani ya kuabudu.)
 
Hatuzungumzii washenzi kama wewe, Tunazungumzia lengo la Semiary ni nini? Na ujue pale wanachujwa kupata wenye wito kama huna wito hata ukiwa seminary kuu utatemwa tu,Seminary ni maalumu kwaajili ya kuandaa mapadre wake baada ya mchujo mkali kielimu na maadili ndio maana serikali isingezigusa kwa sababu ndio zinaandaa viongozi wa kanisa.
Nilijua tu utaingia kwenye huu mtego lengo la seminari ni kutoa viongozi wa dini ,na sio kituo cha kuandaa watakatifu ,ushenzi wa tabia hata hao waliopita seminari kuwa watumishi wa kanisa baadhi yao wana tabia chafu ,ujaskia padri anatembea na sista,hujasikia ishu ya ushoga kwao ?? Dhuluma nk ?

Sasa sijui unashangaa nini mimi kusema ni mshenzi wa tabia
 
Madhaifu yako, hulazimishwi kama umeshindwa utume.
Jamani kusoma seminari sio lazima uwe padri au sista ,eleweni maana yangu,kama lengo ni kuwa padri ,kusingekua na PCB,PCM,HGL,HKL nk watu wangesoma tu theology mwanzo mwisho
 
Nilijua tu utaingia kwenye huu mtego lengo la seminari ni kutoa viongozi wa dini ,na sio kituo cha kuandaa watakatifu ,ushenzi wa tabia hata hao waliopita seminari kuwa watumishi wa kanisa baadhi yao wana tabia chafu ,ujaskia padri anatembea na sista,hujasikia ishu ya ushoga kwao ?? Dhuluma nk ?

Sasa sijui unashangaa nini mimi kusema ni mshenzi wa tabia
Sizungumzii tabia nazungumzia kuandaa Mapadre, kama wanavyoandaliwa wataalamu wengine kama walimu, mambo ya tabia sio lengo la muuliza swali.
 
Mswahili daima hana shukrani. Ungependa afanye nini pamoja na kuchukuwa taasisi zoote hizo pamoja na za kanisa Catholic? !. Kweli mswahili balaa

Uswahili ni kama ugonjwa vile...kuanzia asubuhi ni kupiga story na kazi kidogo...halafu kutafuta sifa sana
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom