Kwanini Nelson Mandela hakumsamehe Winnie Mandela

Half american

JF-Expert Member
Sep 21, 2018
26,153
68,477
Ukweli ni kwamba Winnie alikuwa na wapenzi wengi kipindi mandela yupo gerezani. miezi kadhaa kabla ya mandela kutolewa alikuwa na uhusiano na Dali Mpofu mwanasheria alietofautiana naye miaka 30 ambaye alikuwa katika timu ya wanasheria wa utetezi

Aliendeleza uhusiano huo hata baada ya Mandela kutoka gerezani, wanachama wa ANC waliokuwa karibu na mandela waliudukua mchezo kama ambavyo walidukua matukio kadhaa ya ulevi wa Winnie

Winnie alikuwa kituko katika kipindi cha miaka miwili baada ya mandela kutoka gerezani. kumfuata kumweleza ukweli
Ilifikiriwa kuwa hatua ya juu sana ya busara kwa wapigania uhuru hao wa ANC

Lakini ulifika wakati ambapo mandela au jamii isingeweza kujidanganya. maelezo kuhusu mapenzi ya Winnie na Mpofu yalifikia sehemu mbaya kiasi cha kuonakana hadharani, nakuandikwa kweye gazeti

Gazeti liliandika barua ya Winnie Mandela kwa Mpofu ikifichua wivu wa wazi kwamba Winnie Mandela alichukia kusikia Mpofu kapata mtoto na mwanamke mwingine

"...Kumbuka ni namna gani kila mara unaniumiza. Naendelea kukueleza kwamba hali ya uhusiano inazidi kuzorota nyumbani wewe haujali sababu umeridhika na huyo mwanamke.
mimi si mpuuzi Dali"

Si hivyo tu. Mandela alivumilia mateso ya unyumba kupita kiasi. Kisa kimoja kilichomuumiza sana kilihusu safari. Winnie alikuwa amepata mwaliko wa kwenda marekani kwa ajili ya shughuli za ANC. alitaka kwenda na Mpofu lakini Mandela alimkatalia.

Winnie alikubali kutosafiri naye.ikaaminika Winnie ameondoka mwenyewe nchini lakini Mandela alipomgia simu Winnie kwenye hoteli aliyokuwa amefikia New York, aliyepokea na kujibu alikuwa Mpofu ikiwa na maana alikuwa amesafiri naye. mandela alikuwa mwanamume aliyefanyiwa uzinifu wa kutisha sana.

Mandela anakaririwa akisema hakuwahi kumtarajia Winnie kuwa mseja wakati alipokuwa gerezani lakini alimtaka awe msiri. pia hakukubali kabisa aendeleze uhusiana na wapenzi wake wa nje baada ya yeye kuachiwa gerezani

Mwisho.Tuishi nao kwa akili💔😥

FB_IMG_16946954956639627.jpg
FB_IMG_16946954886139686.jpg
FB_IMG_16946955006700902.jpg
 
Tatizo ni kumpenda mtu asiyekupenda...

Inaonyesha Mandela alimpenda Winnie lakini Winnie alimpenda sana Mpofu...
Kumpenda asiekupenda ni mateso makali sana na mtu wa hivyo hajali chochote.
Kuchapiwa hakujawahi kumuacha mtu salama
Ni hatari sana
Hivi maanake mandela kwa miaka 27 aliyokua kifungoni hakupiga mzigo? Aiseeee🤔🤔🤔
Sijui ila 27 yrs ni mingi waliowahi kufungwa miaka mingi watupe experience
 
Back
Top Bottom