Mwande na Mndewa
JF-Expert Member
- Feb 26, 2021
- 1,113
- 3,141
Tundu Lissu ni mwanasiasa anayerudi nchini Tanzania kula bata baada ya matakwa yake yote kutimizwa, utakuta kuna mtu anamsubiri Tundu Lissu akiamini ni mpinzani, la hasha, Tundu Lissu anarudi nchini Tanzania baada ya yale yote aliyoyapigania katika harakati zake kutimizwa na Hayati Rais Magufuli, Tundu Lissu si yule wa mwaka 2009 aliyekuwa anaandika vitabu na kufanya tafiti kule North Mara kuhusu migodi akiwa pamoja na Viongozi wa Kitaifa wa Chadema wakipitia mikataba ya madini na kusema tunadhulumiwa sana kwenye mikataba yetu ya madini, Tundu Lissu sio yule wa 2008 akionekana TBC1 akielezea issue ya mgodi wa North Mara, Buzwagi na GGM.
Centre boulevards of Brussels bila shaka hii ni mitaa maarufu ambako Lissu anapendelea zaidi kutembelea! akiwa uko Ubelgiji au kama yupo nje na Brussels huko Antwerp au Le ROI centre ni dhahiri hakuweza kukumbuka tena kurudi kwenye siasa za Tanzania,mitaa hiyo ilimfanya asahau shida za Watanzania na miezi michache nyuma kilio cha Tundu Lissu klikuwa ni kulipwa stahiki zake,Rais wetu Mama Samia kaona isiwe nongwa kamlipa.Kwa maisha mazuri ya Centre boulevards, Chadema wananjia moja tu ya kumruhusu Tundu Lissu agombee nafasi ya Urais,na hili lijulikane pia, akishiriki kugombea nafasi hiyo,ikitokea ameshindwa!
Naini hawezi ishi nchini kamwe! atarudi tena mitaa ya Centre boulevards of Brussels na Antwerp,tusitaniane bajameni,Ulaya ni Ulaya tuu,Africa itabaki kuwa Africa tu,Ole wa mtu mweusi aonje maisha ya ulaya tena Kwa kibali cha huko, na akapata walau ajira!!! hawezi kumbuka home! kama natania basi Tundu Lissu atakapotua Tanzania hiyo tarehe 25 aape kwa Mungu kuwa hatarudi tena Ulaya,
-Sifa na Harakati za Fidel Castro na Che Guevara.
Fidel Castro na Che Guevara walikuwa vijana mashujaa waliolikomboa bara la Amerika ya kusini walikuwa ni watu wenye uchungu mkubwa kuona maisha ya dhiki,njaa, magonjwa katika nchi za America ya kusini,wakawa na mwamko mkubwa kubadili hali ile kwa kuwa waliamini ya kuwa mfumo wa ubepari ndio chanzo kikubwa kilichokuwa kinaitafuna Latin America.Mwaka 1964 akiwa kama mmoja ya msafara wa watu wa serikali ya Cuba umoja wa Mataifa New York MArekani, aliweza kupata “sifa” ya “mwanamapinduzi halisi wa kukumbukwa” pale aliposimama kwenye ukumbi wa Umoja wa Mataifa na kutoa hotuba ndefu kulaumu wazi ukimya wa Umoja huo juu ya kilichokuwa kinaendelea Afrika ya kusini ambao ni ubaguzi wa rangi uliokithiri,
Mwaka 1965 Fidel Castor na Che Guevara waliingia katika ardhi ya Tanzania,walifikia katika ubalozi wa Cuba mtaa wa Lugalo Upanga,wakiwa na maofisa wa ubalozi wao,dhamira ya safari yao ilikuwa kupanga mipango ya ukombozi na ki mapinduzi kusini mwa Afrika,inasadikika Che Guevara alibakia kwa miezi mitatu nchini akiwa na vitambulisho bandia,Viongozi wa Frelimo walikuja na kukutana na Che Guevara. Baada ya hapo alielekea Bolivia.
-Uanamajumui wa Kwame Nkrumah
Kwame Nkrumah alitumia muda wake mwingi juu ya maandalizi ya kisiasa,yeye na rafiki yake George Padmore walikuwa miongoni mwa waandaaji wa kuu wa mkutano wa tano na wa mwisho kuelekea kuikomboa Afrika na mkutano huo ulipewa jina la "Congress Pan-African" uliyofanyika huko Uingereza katika mji wa Manchester,katika mkutano Nkhurumah alifafanua mkakati na Mlengo yake wa kuweza kuzikomboa nchi za Afrika na kusema umoja ndio njia pekee inayoweza kuwa weka pamoja waafrika kwani unyonyaji na ubaguzi wa rangi kimsingi inazidi ukoloni uliopo barani Afrika.
Nkhurumah alikuwa na imani za Ujamaa wa Kiafrika (Africans Socialism) na hatima yeye na wenzake Walikubaliana kuendeleza shirikisho la Umoja wa Mataifa ya Afrika ili kuweza kuikomboa Afrika yote kutoka mikono ya ukoloni, na interlocking mashirika ya kikanda,ikiwa ni pamoja na kuwasaidia viongozi wa Ukombozi kupitia mataifa tofauti yatakayo kuwa yanadai Uhuru,Nkrumah alipendelea na walipanga kujiingiza katika utamaduni mpya wa Afrika bila ukabila na demokrasia ndani ya mfumo wa ujamaa au ukomunisti ikiwa ni pamoja na kuikusanya masuala ya jadi na fikra za kisasa.
-Umajumui wa Nelson Mandela.
Mwaka 1962, Nelson Mandela alikamatwa kwa kuongoza harakati ya kupinga ubaguzi wa rangi na alihukumiwa kifungo cha maisha miaka miwili baadaye kwa “kosa la kupindua serikali kwa njia za vurugu”. Wakati akitumikia kifungo cha miaka 27 jela kabla ya kuachiliwa mwaka 1990, Mandela alisema, China ilikuwa ndio nguzo yake ya kiroho iliyomsaidia kuishi siku zake katika jela iliyopo kisiwa cha Robben. Kwani akiwa huko alisoma kwa hamu kubwa vitabu vya the Selected Works of Mao Zedong alivyokuwa akitumiwa na mke wake Winnie, na kusifu sana kitabu cha Liu Shaoqi cha ‘How to be a Good Communist’. Hayati Mandela aliwahi kusema Safari ndefu ya Jeshi Jekundu la China pamoja na mapambano ya kishujaa yaliyofanywa na watu wa China katika ukombozi wa taifa imewatia moyo Waafrika Kusini katika mapambano yao dhidi ya ubaguzi wa rangi.
Lakini tukumbuke kwamba muda wote huo China ilikuwa ikiisaidia Afrika Kusini na mapambano yake dhidi ya ubaguzi wa rangii. Wakati Mandela alipotoka jela akiwa na miaka 71 Februari 1990, China ilimpongeza sana, na baada ya hapo, Mandela aliendelea kuifuatilia China. Wahenga wanasema penye nia pana njia, kwani Oktoba 1992, Mandela alitembelea nchini China kwa mara ya kwanza akiwa Mwenyekiti wa chama cha ANC, na kupokelewa pamoja na kupewa heshima kubwa kama wanavyopewa wakuu wa nchi,Ahsante Baba Nelson Mandela.
-Sifa na harakati za Tundu Lissu
Nilipomsikia akisema "tutashtakiwa MIGA", "Tanzania inawahitaji wazungu kuliko wazungu wanavyoihitaji Tanzania" nikajua sasa basi,Tundu Lissu si yule Shujaa wa mwaka 2009,Acacia kutupeleka mahakamani ni maamuzi yao, walikuwa wakitetea maslahi yao,hilo halishangazi,kilichonishangaza ni Tundu Lissu aliyekuwa mwanzilishi wa harakati hizi na mwakilishi wa wananchi kusaliti na kusimama upande wa mabeberu kinyume na maslahi ya nchi.It was clear kwa mtanzania wa kawaida kwamba Rais Magufuli was trying to do something positive,Rais Magufuli alikuwa akitimiza yale yote Tundu Lissu aliyoyafanyia utafiti Mwaka 2009, kwenye inshu ya madini, na Lissu alikuwa kinyume,sasa weka na kauli zake zingine alizoongea CNN,BBC na Straight talk Afrika,Shala Ssali na Balozi Masilingi zilizozidi kumuexpose jinsi alivyo kibaraka,
Hayati Rais Magufuli alifanyia kazi tafiti za Tundu Lissu za mwaka 2009 na kuunda timu kwa ajili ya kufuatilia tafiti za Tundu Lissu za kudhulumiwa kwenye madini,repori ikaja lakini cha ajabu Tundu Lissu akaipiga,Rais Magufuli kwa nafasi aliyokuwa nayo kama Rais (akipokea reports kutoka kwa washauri mbali mbali chini yake),na kwa uzoefu wake akiwa mjumbe wa baraza la mawaziri kwa miaka 20,alikuwa na data za kutosha kuhusu hili na kujua njia gani sahihi ya kutumia,lakini Tundu Lissu alipinga utekelezwaji wa kurejea tena mikataba yote ya madini na akasema tukigusa madini tutashtakiwa,sasa kama njia iliyotumika haikuwa sahihi ndivyo mapambano yalivyo,hakuna njia moja itakayokuwa effective aslimia 100. Cha muhimu hapa ilikuwa nia,uthubutu, na mwanzo (initiative) katika kuwaonyesha mabeberu kwamba tunahitaji mabadiliko,na vyovyote vile Tundu Lissu alivyolitazama suala hilo la report za makinikia hawezi kuunderestimate impact ya hizo initiatives za Hayati Rais Magufuli kwenye madini,Ni vizuri tukamsikia tena Tundu Lissu akitueleza njia sahihi za kutekeleza harakati zake za mwaka 2009 juu ya kudhulumiwa kwenye mikataba ya madini,
Nimalizie kwa kusema kwamba Tindu Lisu ni mtanzania wa kwanza,pengine siyo wa kwanza, kuuonyesha umma kwamba alaaniwe yeye awekaye tumaini lake kwa wanasiasa,kwa maana Tundu Lissu na Chadema walitugeuka wakati Rais Magufuli alipochuku ilani yao ya Chadema na kuifanyia kazi,pengine Mnyika alitoka hadharani na kusema Rais Magufuli anaifanyia kazi ilani ya Chadema lakini baada ya muda wao Chadema wakaanza kupinga utekelezwaji wa ilani hiyo,ubinadamu kazi,hakuna chochote alichokifanya Tundu Lissu katika sakata la makinikia kilichoonyesha kwamba yupo upande wa nchi iliyokuwa ikimlipa mshahara.Alifeli na alifeli pakubwa,Who cares kama kwa Rais Magufuli na sakata la makinikia lilikuwa na lengo la kumpatia umaarufu?Umaarufu gani aliutaka zaidi ya kuwa rais wa nchi? Na kama kweli kuthubutu kufight kwa ajili ya mabadiliko katika mifumo ya mikataba ya madini ilikuwa na lengo la kupata umaarufu then well and good,umaarufu kwa kusudi jema.Unataka tuwe na viongozi wa nchi wasiotaka kuwa maarufu kwa kutofanya chochote katika kuibadilisha nchi?
Siasa za Chadema kwa siku za karibuni tofauti na wakati ule kulikuwa na ajenda tunayosimama nayo,Miaka ya sasa chadema hawaeleweki Wana ajenda ipi,kwa mfano Leo hata matawini kupo kimya! Mbowe yupo kimya! Mnyika yupo kimya! Nchi nzima kimya! Lissu akija leo atakuwa na shughuli gani? Namkumbuka sana Daktari Wilbroad Slaa na "operation sangara" niliona nia yao thabiti nikiwa Mwanza mwaka ule wa 2008 nilichangia 10,000 ilikuwa ni hela nyingi kwa mwaka ule wa 2008 lalini sikujua Mwaka 2023 Chadema itakuwa haina ajenda wala sera,sikudhani kama chama kingekuwa chawa,namshauri Tundu Lissu aendelee kubaki Ubelgiji Chadema aliyoipigania hata kuweka maisha yake rehani haipo tena Lissu endelea kula mishikaki hapo centre boulevards na ukitamani mtindi njoo huku Antwerp kuna mtindi safi kabisa na mkate wa kuoka.
Nikiishia hapa, Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854
-Bachelor of Business Administration in International Business.
-Master of Leadership and Management.
Recent Publications;-
-Assessment on the effect of Micro-Financing on poverty reduction.