Kwanini nchi za Afrika ikiwemo Tanzania bado maskini licha ya kupokea Misaada na Mikopo ya mamilioni ya Fedha kutoka nchi zilizoendelea? - Part I

Nchi za Ulaya kabla ya vita zilikuwa tayari zina taasisi imara na watu wenye uzoefu wa kuendesha nchi. Kwa hiyo walikuwa na uwezo wa kujenga upya nchi zao baada ya vita kuziharibu. Watanzania na Waafrika wengine hatuna uzoefu wa kuendesha nchi, tumezoea kuendesha makabila na tribal kingdoms. Ni ngumu kumchukua mtu ambaye labda alikuwa ni chifu wa kabila moja au mtoto wa chifu wa kabila moja kama Nyerere halafu utegemee ataweza kuendesha nchi ya makabila zaidi ya 100 kama nchi za Ulaya. Kuziendesha nchi ambazo zilikuwa zinaendeshwa kikabila ni kazi ngumu hata ukipewa misaada ya mamilioni.
Pamoja na jibu lako zuri, ambalo kimsingi naliunga mkono, sikubaliani nawe katika mlinganisho huo wa nchi za ulaya na hizi zetu, hasa Tanzania.

Tumepata uhuru takribani miaka sitini sasa. Ndio, tulianzia chini sana, na uwezo wetu ulikuwa mdogo sana, lakini muda huo ni muda mzuri na wa kutosha sana kuleta mabadiliko chanya kuliko haya tuliyofikia sasa hivi kama tungekuwa makini na kufanya mambo yetu kwa ueledi na uhakika zaidi.
Leo hii, hata yale mambo mazuri tuliyokuwa tumekwishayatimiza, ni kama tunarudi nyuma, kwa sababu hatuna tabia ya kuwa na kumbukumbu ya mazuri tuliyokwishafanya na kuyaendeleza ili tusigharimie tena kuyafanya upya. Ni kama serikali yetu haina kumbukumbu, pamoja na kwamba ni chama kilekile kinachounda serikali hizo. Wakati mwingine, serikali hiyo hiyo inarudia tena makosa yale yale yaliyofanyika huko nyuma.
Utapataje maendeleo kwa hali ya namna hiyo!

Pili, sisi haitulazimu tena tukagundue kurudumu upya. Kuna mambo mengi sana tunayotakiwa kugezea tu yalivyofanywa na wengine ili nasi tufaidike nayo. Hata kama ikilazimu kubadili kidogo ili yalingane na hali yetu ilivyo, isingekuwa vigumu na kutuchukua muda mrefu namna hii kuleta mabadiliko ya maisha ya wananchi wetu.

Jambo ninalojua ni moja. Tunakosa kiongozi mwenye dira na usimamizi wa dira hiyo ili kutufikisha kwenye hayo anayoamini nchi yetu inayahitaji.

Chukulia mfano wa kilimo na elimu tu, maeneo mawili ambayo mimi naamini yangeweza kutubadilisha haraka sana kama nchi kama yangewekewa mkazo unaostahiri. Sisemi kamwe hapa kwamba mengine yote yataachwa, lakini haya mawili yawe na kipa umbele cha ziada katika uongozi wa kiongozi shupavu na imara ndani ya miaka kumi.
Kilimo ambacho wananchi wetu wengi ndiko wanakopatia ridhiki yao, wakapata mbegu bora, vitendea kazi na ushauri mahususi juu ya kazi zao; na serikali ikafanya kila iwezalo kuwasaidia kutafuta soko la mazao yao..., hali itakuwaje ndani ya miaka kumi?

Elimu yetu inaonekana kama tunarudi kinyumenyume. Tunakuwa na wasomi wengi, lakini thamani ya wasomi hawa inakuwa haijionyeshi katika jamii. Ni hawa hawa wahitimu wetu ndio tunaowategemea wasaidie kuleta mabadiliko ndani ya jamii zetu. Lakini sasa angalia tunavyokwenda, hata mashirika ya Vodacom na Tigo hawawezi kabisa kupata watu ndani ya nchi hii wa kuendesha vikampuni hivi, baada ya miaka sitini ya kufundisha watu wetu wenyewe?

Mkuu Bepari2020, nakumbuka mara ya mwisho tulikutana kule kwa Kagame na Rwanda yake. Pamoja na kwamba hatukuweza kukubaliana katika yale mambo huko, leo hii nitakubali katika hili moja la yeye kuwa na dira, basi.

Umetolea mfano wa nchi za Ulaya, sijui utasemaje kuhusu nchi kama Malaysia, Vietnam na nyingine ambazo nazo zimeibuka kutoka kwenye umaskini miaka kadhaa baada ya kuwa huru.
 
"Science and Technology are the keystones for developments"
Uko sahihi lakini sababu kubwa ni vichwa vya raia wa nchi husika. japan ni nchi ndogo isiyokuwa na resources zozote ila Vichwa vya wananchi wake vimeamka barabara kubuni teknolojia mbalimbalwai

Tanzania tuna wanasayansi wengi tumesomesha ndani na nje na wengine wako nje ya nchi lakini Ubunifu wa teknolojia ni zero. HAWANA WALICHOKIBUNI

tukubali tu kuwa hata uwe na resources, zote kama Raia wako ni bongo lala vichwa vibovu resources zote hazina maana Mfano ni Kongo nchi Tajiri kwa resources kuliko nchi yeyote duniani lakini maskini, Tanzania hivyo hivyo

Sijui ilikuwaje sehemu zenye Mali nyingi Mungu aliweka wajinga ndio wawe wakazi wa eneo hilo
Africa ina mali kaweka wajinga waAfrika nchi za kiarabu kuna mali hasa mafuta na gesi kaweka mijinga miarabu kuwa mikazi ya eneo hilo
 
Nchi za Ulaya kabla ya vita zilikuwa tayari zina taasisi imara na watu wenye uzoefu wa kuendesha nchi. Kwa hiyo walikuwa na uwezo wa kujenga upya nchi zao baada ya vita kuziharibu. Watanzania na Waafrika wengine hatuna uzoefu wa kuendesha nchi, tumezoea kuendesha makabila na tribal kingdoms. Ni ngumu kumchukua mtu ambaye labda alikuwa ni chifu wa kabila moja au mtoto wa chifu wa kabila moja kama Nyerere halafu utegemee ataweza kuendesha nchi ya makabila zaidi ya 100 kama nchi za Ulaya. Kuziendesha nchi ambazo zilikuwa zinaendeshwa kikabila ni kazi ngumu hata ukipewa misaada ya mamilioni.
Ili tuendelee tufanyeje?
 
Uko sahihi lakini sababu kubwa ni vichwa vya raia wa nchi husika. japan ni nchi ndogo isiyokuwa na resources zozote ila Vichwa vya wananchi wake vimeamka barabara kubuni teknolojia mbalimbalwai

Tanzania tuna wanasayansi wengi tumesomesha ndani na nje na wengine wako nje ya nchi lakini Ubunifu wa teknolojia ni zero. HAWANA WALICHOKIBUNI

tukubali tu kuwa hata uwe na resources, zote kama Raia wako ni bongo lala vichwa vibovu resources zote hazina maana Mfano ni Kongo nchi Tajiri kwa resources kuliko nchi yeyote duniani lakini maskini, Tanzania hivyo hivyo

Sijui ilikuwaje sehemu zenye Mali nyingi Mungu aliweka wajinga ndio wawe wakazi wa eneo hilo
Africa ina mali kaweka wajinga waAfrika nchi za kiarabu kuna mali hasa mafuta na gesi kaweka mijinga miarabu kuwa mikazi ya eneo hilo
YEHODA, siku hizi tunaelewana sana. Sijui ilikuwaje huko nyuma ukawa umeharibika kiasi kile?

Hapana, siyo wananchi hata kidogo. Tatizo lipo kwa viongozi. Tunakosa viongozi wenye kutuonyesha dira ya maendeleo ya nchi yetu ikoje.

Wananchi watajipanga vizuri kabisa kutimiza dira hiyo kama ipo na imesimamiwa ipasavyo. Mwalimu Nyerere alijaribu sana, lakinini wakati na mambo yalikuwa magumu sana enzi zile.

Sasa hatuna kabisa mategemeo ya kiongozi anayeweza kusimamia anayoyaona mbele ya nchi yetu. Tunajipigia tu mradi liende.
 
Kwa akili za viongozi zinazowaza madaraka, kuua upinzani, ngono, kuiba, utajiri binafsi, kula bata, kutapeli, kudanganya, wivu, kuzuia wengine wasipate maendeleo, kabila langu, ndugu zangu, kijijini kwangu, kutalii nje kulikoendelea, nk, sijui.

Naomba tujaribu kufanya tathmini, viongozi wengi na watumishi wa serikali wanawaza nini?
 
YEHODA, siku hizi tunaelewana sana. Sijui ilikuwaje huko nyuma ukawa umeharibika kiasi kile?

Hapana, siyo wananchi hata kidogo. Tatizo lipo kwa viongozi. Tunakosa viongozi wenye kutuonyesha dira ya maendeleo ya nchi yetu ikoje.

Wananchi watajipanga vizuri kabisa kutimiza dira hiyo kama ipo na imesimamiwa ipasavyo. Mwalimu Nyerere alijaribu sana, lakinini wakati na mambo yalikuwa magumu sana enzi zile.

Sasa hatuna kabisa mategemeo ya kiongozi anayeweza kusimamia anayoyaona mbele ya nchi yetu. Tunajipigia tu mradi liende.
Hili la kuwaza viongozi Kila wakati si kweli mabilionea wakina Billy gates waliogundua. Microsoft hawakusaidiwa au kupewa dira na kiongozi yeyote awe wa serikali au yeyote au dira ya nchi akili zao ziiamka za wao kama wao
Wagunduzi wa Internet, simu, magari nk wote hakuna cha serikali wala nini
Wenzetu kwa asilimia kubwa huamini kuwa hatima ya maisha yao imo mikononi mwao wao wenyewe kama individuals sisi sababu tuko wavivu hatutaki kubeba responsibility hatima zetu tunasukumia viongozi! !!! Hivyo tunasababisha bongo zetu kulala sababu tutakuwa tumekabidhi viongozi ndio wawaze kwa niaba yetu ambao nao Ni bongolala kama sisi hawana tofauti sana na sisi! ! !! Mjinga akikabidhi mijinga kiongozi awaze kwa niaba yake matokeo yake yatakuwaje? Ndipo tulipo tuamke! !!!

Sasa Mungu aliumba ubongo kwenye kichwa cha kila mtu wa nini? Je ni kutumia tu kujua Choo kiko wapi au?
 
Hizo ni zile za IMF; wanazosema ni za UVIKO-19!

Hapo sasa wanazitumia kufufua sekta ya utalii kwa kuandaa mapicha!
Dah!

Kazi kweli kweli,kwaiyo zinaenda kufanya kazi tofauti na lengo walizoombea huo mkopo?
 
Hili la kuwaza viongozi Kila wakati si kweli mabilionea wakina Billy gates waliogundua. Microsoft hawakusaidiwa au kupewa dira na kiongozi yeyote awe wa serikali au yeyote au dira ya nchi akili zao ziiamka za wao kama wao
Wagunduzi wa Internet, simu, magari nk wote hakuna cha serikali wala nini
Wenzetu kwa asilimia kubwa huamini kuwa hatima ya maisha yao imo mikononi mwao wao wenyewe kama individuals sisi sababu tuko wavivu hatutaki kubeba responsibility hatima zetu tunasukumia viongozi! !!! Hivyo tunasababisha bongo zetu kulala sababu tutakuwa tumekabidhi viongozi ndio wawaze kwa niaba yetu ambao nao Ni bongolala kama sisi hawana tofauti sana na sisi! ! !! Mjinga akikabidhi mijinga kiongozi awaze kwa niaba yake matokeo yake yatakuwaje? Ndipo tulipo tuamke! !!!

Sasa Mungu aliumba ubongo kwenye kichwa cha kila mtu wa nini? Je ni kutumia tu kujua Choo kiko wapi au?
YEHODA! Taratibu basi mkuu!

Unasahau mazingira waliyokuwemo hao akina Billy Gates wakigundua hayo unayoyasema hapa.

Hilo la kuwaza "hatma ya maisha kuwa mikononi mwa mhusika" ni lazima liungane na maono na mwelekeo wa nchi, hayaji tu hivi hivi.
 
Dah!

Kazi kweli kweli,kwaiyo zinaenda kufanya kazi tofauti na lengo walizoombea huo mkopo?
Hapana, lengo ni lile lile, ila sasa naona wameamua kujifaidisha na wao wenyewe. Hatujui wamepanga kufanya nini tena, maanake hele ni ndefu ya kutosha. Mahela ya namna hii ndiyo huwa yanatumika hovyohovyo. Si ajabu ukasikia miradi ya ajabu ajabu inaibuliwa huko Makunduchi.

Umesikia hata machifu wanadai watambuliwe. Ni mahela ya namna hii ndiyo huwa yananunua mashabiki kama hao ili kiongozi aonekane anapendwa.
 
YEHODA! Taratibu basi mkuu!

Unasahau mazingira waliyokuwemo hao akina Billy Gates wakigundua hayo unayoyasema hapa.

Hilo la kuwaza "hatma ya maisha kuwa mikononi mwa mhusika" ni lazima liungane na maono na mwelekeo wa nchi, hayaji tu hivi hivi.
Tanzania wako mabilionea akina Mengi family Azam akina Dewji nk kwenye nchi hii tunayosema haina maono na viongozi hawana Dira,! ! Na kwenye mazingira haya haya wameibuka natajiri

Wao binafsi wameamua ku take personal responsibility kwa hatima zao wakati wengine wanasubiri hatima zao zibebwe na viongozi wa siasa
 
Niliuliza hili swali kupata maoni, sio hapa tu ni kwenye majukwaa mbalimbali, Asante kwa wote waliotoa maoni yao.

Lakini kwa ufupi misaada na Mikopo kihistoria vilianza miaka ya 1945 na ilikuwa baada ya vita kuu ya pili ya dunia kwa malengo mawili;

i) Kujenga miundombinu iliyoharibiwa wakati wa vita na jukumu hili ilipewa Benki ya Dunia.

(ii) Na lengo la pili lilikuwa ni kuharakisha maendeleo ikiwemo biashara na kudhibiti masuala yote yahusuyo Fedha Duniani, jukumu hili likawa ni la Shirika la Fedha Duniani (IMF) na Shirika la Biashara Duniani.

Lakini kwa pamoja mashirika haya waliyaweka pia kwaajili ya kudhibiti ama kuzuia kutokea tena kwa mdororo wa uchumi (Great Economic Depression) uliowahi kutokea miaka ya 1930's (Hawa watu wana akili , kumbuka Kati ya wadau 700 waliokuwa wanajadili haya, hakuna mdau hata mmoja aliyetoka Afrika kwa ujumla).

Mwaka 1946 na 1947 nchi za Ulaya zilichukua mikopo na misaada kutoka kwenye mashirika haya. Nchi kama Ufaransa, Denmark, Netherlands na Luxembourg waliweza kufanikisha kuunda upya nchi zao na kufuta uharibifu wote uliosababishwa na vita, pamoja na kujenga uchumi wao. Kwa kiasi kikubwa taasisi hizi za Kimataifa zilimudu kudhibiti na kuchochea Uchumi wa Dunia.

Sasa ni nini kilizikuta nchi za Afrika ikiwemo Tanzania ambapo nchi hizi zinaonekana kuwa na ugonjwa sugu wa Umaskini usiosikia dawa licha ya kupewa mikopo na misaada ya matrilioni ya Fedha? Tutaona Part (ii)

View attachment 1929403Jibu ni kwamba nchi husika hazijawa huru itakiwavyo hasa baada ya kukataa kuungana na kuwa nchi moja kubwa ili kuweza kuwa na sauti katika nyanja za kimataifa.Pia Afrika ilitawalilwa na wakoloni weusi ambao waliiga kila kitu walichofanya mabwana zao kiasi cha kuendelea kuiumiza. Waafrika watawaliwa pia walijengewa uwezo mdogo wa kujikomboa na badala yake wanategemea wazungu. Hata elimu iliyotolewa pindi baada ya kupata uhuru ilitengeneza wasaka kazi maofisini lakini siyo wabunifu na watu wanaoweza kujikomboa kulhali.Ndo maana bado tunaabudia shahada badala ya nini msomi anaweza kufanya. Kimsingi, wakoloni walidumaza akili zetu sana.Ndo maana bado tuna watu wanategemea miujiza au kucheza kamali kufanikiwa katika maisha ukiachia mbali wanaotegemea kuhujumu nchi zao kwa wale wanaofanya kazi serikalini. Inapotokea wezi wakubwa wakaiba na kufukarisha jamii,mafukara huwaabudia badala ya kuwachoma moto kama vibaka wengine.
 
Uko sahihi lakini sababu kubwa ni vichwa vya raia wa nchi husika. japan ni nchi ndogo isiyokuwa na resources zozote ila Vichwa vya wananchi wake vimeamka barabara kubuni teknolojia mbalimbalwai

Tanzania tuna wanasayansi wengi tumesomesha ndani na nje na wengine wako nje ya nchi lakini Ubunifu wa teknolojia ni zero. HAWANA WALICHOKIBUNI

tukubali tu kuwa hata uwe na resources, zote kama Raia wako ni bongo lala vichwa vibovu resources zote hazina maana Mfano ni Kongo nchi Tajiri kwa resources kuliko nchi yeyote duniani lakini maskini, Tanzania hivyo hivyo

Sijui ilikuwaje sehemu zenye Mali nyingi Mungu aliweka wajinga ndio wawe wakazi wa eneo hilo
Africa ina mali kaweka wajinga waAfrika nchi za kiarabu kuna mali hasa mafuta na gesi kaweka mijinga miarabu kuwa mikazi ya eneo hilo

Mungu kafanya hivyo ili kuweka Balance, mfano kama hao wenye akili ndio wangalipewa maeneo yenye resources na hao (sisi) Wajinga tungepewa sehemu zisizo na resources hali ingejuaje kwetu???---- Mambo yangalikuwa mabaya MNO, tungeishi kama Wanyama na tungekuwa watumwa wa hao wenye akili kwa kiasi kikubwa sana.
 
Nimekubali kabisa hili jibu limeenda shule la great thinker
 
Mkuu 'FM WOLLE', kukusaidia kupata jibu sahihi kwa swali lako, nami ningependa nikuulize wewe na wasomaji wako wengine swali, ambalo kama mnaweza kulijibu kwa usahihi, basi swali lako nalo litakuwa limepata jibu:

Kuna nchi ngapi duniani ambazo zilishapata maendeleo kutokana na misaada?

Usikimbilie kujibu hili swali bila ya tafakuri makini juu yake, kama kweli nia yako ya kutaka jibu ya swali lako ni halali.
Huwezi kupata maendeleo kwa misaada utapata maendeleo kwa juhudi zako
 
Nchi za Africa zitaendelea kwa kutumia ARDHI tu. Sisi tuna ardhi ya kutosha, mapori ya akiba lukuki kufanya kilimo cha kimkakati ili tuuze mazao yetu Ulaya, Asia na Uarabuni tumegoma, badala yake tumeanza kuchangishana TOZO ili tujikwamue.

Bila kilimo cha kimkakati Africa & Tanzania haitakaa ijikomboe kwa wimbi la umasikini, TOZO hazifuti umaskini, tozo ni kama upatu mnachangishana then mnanunua TV kwa wanakikundi mmoja - mtatokaje hapo sasa.
 
Dah!

Kazi kweli kweli,kwaiyo zinaenda kufanya kazi tofauti na lengo walizoombea huo mkopo?
Resources zetu tu ziko kibao zimesshindwa kututoa kwenye umaskini misaada na mikopo ndio itaweza?
 
Back
Top Bottom