KalamuTena
JF-Expert Member
- Jul 7, 2018
- 13,189
- 17,157
Pamoja na jibu lako zuri, ambalo kimsingi naliunga mkono, sikubaliani nawe katika mlinganisho huo wa nchi za ulaya na hizi zetu, hasa Tanzania.Nchi za Ulaya kabla ya vita zilikuwa tayari zina taasisi imara na watu wenye uzoefu wa kuendesha nchi. Kwa hiyo walikuwa na uwezo wa kujenga upya nchi zao baada ya vita kuziharibu. Watanzania na Waafrika wengine hatuna uzoefu wa kuendesha nchi, tumezoea kuendesha makabila na tribal kingdoms. Ni ngumu kumchukua mtu ambaye labda alikuwa ni chifu wa kabila moja au mtoto wa chifu wa kabila moja kama Nyerere halafu utegemee ataweza kuendesha nchi ya makabila zaidi ya 100 kama nchi za Ulaya. Kuziendesha nchi ambazo zilikuwa zinaendeshwa kikabila ni kazi ngumu hata ukipewa misaada ya mamilioni.
Tumepata uhuru takribani miaka sitini sasa. Ndio, tulianzia chini sana, na uwezo wetu ulikuwa mdogo sana, lakini muda huo ni muda mzuri na wa kutosha sana kuleta mabadiliko chanya kuliko haya tuliyofikia sasa hivi kama tungekuwa makini na kufanya mambo yetu kwa ueledi na uhakika zaidi.
Leo hii, hata yale mambo mazuri tuliyokuwa tumekwishayatimiza, ni kama tunarudi nyuma, kwa sababu hatuna tabia ya kuwa na kumbukumbu ya mazuri tuliyokwishafanya na kuyaendeleza ili tusigharimie tena kuyafanya upya. Ni kama serikali yetu haina kumbukumbu, pamoja na kwamba ni chama kilekile kinachounda serikali hizo. Wakati mwingine, serikali hiyo hiyo inarudia tena makosa yale yale yaliyofanyika huko nyuma.
Utapataje maendeleo kwa hali ya namna hiyo!
Pili, sisi haitulazimu tena tukagundue kurudumu upya. Kuna mambo mengi sana tunayotakiwa kugezea tu yalivyofanywa na wengine ili nasi tufaidike nayo. Hata kama ikilazimu kubadili kidogo ili yalingane na hali yetu ilivyo, isingekuwa vigumu na kutuchukua muda mrefu namna hii kuleta mabadiliko ya maisha ya wananchi wetu.
Jambo ninalojua ni moja. Tunakosa kiongozi mwenye dira na usimamizi wa dira hiyo ili kutufikisha kwenye hayo anayoamini nchi yetu inayahitaji.
Chukulia mfano wa kilimo na elimu tu, maeneo mawili ambayo mimi naamini yangeweza kutubadilisha haraka sana kama nchi kama yangewekewa mkazo unaostahiri. Sisemi kamwe hapa kwamba mengine yote yataachwa, lakini haya mawili yawe na kipa umbele cha ziada katika uongozi wa kiongozi shupavu na imara ndani ya miaka kumi.
Kilimo ambacho wananchi wetu wengi ndiko wanakopatia ridhiki yao, wakapata mbegu bora, vitendea kazi na ushauri mahususi juu ya kazi zao; na serikali ikafanya kila iwezalo kuwasaidia kutafuta soko la mazao yao..., hali itakuwaje ndani ya miaka kumi?
Elimu yetu inaonekana kama tunarudi kinyumenyume. Tunakuwa na wasomi wengi, lakini thamani ya wasomi hawa inakuwa haijionyeshi katika jamii. Ni hawa hawa wahitimu wetu ndio tunaowategemea wasaidie kuleta mabadiliko ndani ya jamii zetu. Lakini sasa angalia tunavyokwenda, hata mashirika ya Vodacom na Tigo hawawezi kabisa kupata watu ndani ya nchi hii wa kuendesha vikampuni hivi, baada ya miaka sitini ya kufundisha watu wetu wenyewe?
Mkuu Bepari2020, nakumbuka mara ya mwisho tulikutana kule kwa Kagame na Rwanda yake. Pamoja na kwamba hatukuweza kukubaliana katika yale mambo huko, leo hii nitakubali katika hili moja la yeye kuwa na dira, basi.
Umetolea mfano wa nchi za Ulaya, sijui utasemaje kuhusu nchi kama Malaysia, Vietnam na nyingine ambazo nazo zimeibuka kutoka kwenye umaskini miaka kadhaa baada ya kuwa huru.