Kwanini nchi za Afrika ikiwemo Tanzania bado maskini licha ya kupokea Misaada na Mikopo ya mamilioni ya Fedha kutoka nchi zilizoendelea? - Part I

Wolle Melkas Fernando

JF-Expert Member
May 4, 2016
218
297
Niliuliza hili swali kupata maoni, sio hapa tu ni kwenye majukwaa mbalimbali, Asante kwa wote waliotoa maoni yao.

Lakini kwa ufupi misaada na Mikopo kihistoria vilianza miaka ya 1945 na ilikuwa baada ya vita kuu ya pili ya dunia kwa malengo mawili;

i) Kujenga miundombinu iliyoharibiwa wakati wa vita na jukumu hili ilipewa Benki ya Dunia.

(ii) Na lengo la pili lilikuwa ni kuharakisha maendeleo ikiwemo biashara na kudhibiti masuala yote yahusuyo Fedha Duniani, jukumu hili likawa ni la Shirika la Fedha Duniani (IMF) na Shirika la Biashara Duniani.

Lakini kwa pamoja mashirika haya waliyaweka pia kwaajili ya kudhibiti ama kuzuia kutokea tena kwa mdororo wa uchumi (Great Economic Depression) uliowahi kutokea miaka ya 1930's (Hawa watu wana akili , kumbuka Kati ya wadau 700 waliokuwa wanajadili haya, hakuna mdau hata mmoja aliyetoka Afrika kwa ujumla).

Mwaka 1946 na 1947 nchi za Ulaya zilichukua mikopo na misaada kutoka kwenye mashirika haya. Nchi kama Ufaransa, Denmark, Netherlands na Luxembourg waliweza kufanikisha kuunda upya nchi zao na kufuta uharibifu wote uliosababishwa na vita, pamoja na kujenga uchumi wao. Kwa kiasi kikubwa taasisi hizi za Kimataifa zilimudu kudhibiti na kuchochea Uchumi wa Dunia.

Sasa ni nini kilizikuta nchi za Afrika ikiwemo Tanzania ambapo nchi hizi zinaonekana kuwa na ugonjwa sugu wa Umaskini usiosikia dawa licha ya kupewa mikopo na misaada ya matrilioni ya Fedha? Tutaona Part (ii)

IMG-20210908-WA0033.jpg
 
Wenzetu waliwekeza kwenye uchumi wa familia Kwanza kwa kulazimisha Kila familia kuwa na idadi ya watoto wachache watakaoweza kujiimarisha kiuchumi mfano China, Nchi za Ulaya idadi ya watoto haizidi wanne hivyo uchumi wa familia umezingatiwa Kwanza Ili kuiacha serikali ipambane na uchumi wa Nchi na ustawi wa mazingira mazuri ya Kila huduma za jamii.
 
Tatizo upigaji mwingi chaajabu wanaopigwa ni maskini kama Mimi, nakumbuka wakati nikiwa shule tuliagizwa tupeleke ndoo nakweli tulifanya hivyo
Ndoo zilikuwa mpya na wanafunzi wengi sana tulipeleka chaajabu baada ya week 2 hatukuziona zile ndoo na tulivyo na nidhamu ya uoga hatukuweza kuhoji ikawa nitolee

Pia Kuna wanafunzi wenzetu walipewa Lim ili wazipange vzuri chaajabu wakaanza kuficha baadhi ya makalatasi unaona nikwajinsi gani upiga niutamaduni wetu

Yaani hata wewe mtoa mada hii leo ukipewa uongozi lazima utaanza kufikilia kijenga ile nyumba yako iliyoishia juu y linta

Kwakifupi upigaji na umimi imetamalaki miyoni mwetu.
 
Utaendeleaje kama akili zetu ndo hizi tunazoziona sasa hivi.Bila mapinduzi ya fikra kamwe hatuwezi kufanya jambo lolote.Tukishapindua fikra zetu ndipo tutakapoweza kutumia rasilimali tulizonazo ipasavyo,watu watakua wabunifu,viongozi watakua na weledi na uwajibikaji achana na hawa wa tunaowaona,tutakua na siasa safi yakusikilizana,tutapunguza ubinafsi na ufisadi,tutajali mambo ya msingi kama elimu,afya namengine badala yakutumia muda mwingi kujadili ujinga na matakataka mengine.kwa ujumla sisi bado niwajinga.
 
Hii nchi haiwezi kuendelea chini ya ccm hata wakipewa miaka 1000. Hilo sahau.
socialism imeharibu sana watu akili, si chama chenu ndo kinakoleza moto wa misaada, magufuli alivoamua tuanze kujitegemea mkamuona diktetea kwa kifupi nyie mnatakiwa wote mumfuate mbowe ukonga ni janga kwa hii dunia
 
Nchi za Ulaya kabla ya vita zilikuwa tayari zina taasisi imara na watu wenye uzoefu wa kuendesha nchi. Kwa hiyo walikuwa na uwezo wa kujenga upya nchi zao baada ya vita kuziharibu. Watanzania na Waafrika wengine hatuna uzoefu wa kuendesha nchi, tumezoea kuendesha makabila na tribal kingdoms. Ni ngumu kumchukua mtu ambaye labda alikuwa ni chifu wa kabila moja au mtoto wa chifu wa kabila moja kama Nyerere halafu utegemee ataweza kuendesha nchi ya makabila zaidi ya 100 kama nchi za Ulaya. Kuziendesha nchi ambazo zilikuwa zinaendeshwa kikabila ni kazi ngumu hata ukipewa misaada ya mamilioni.
 
Niliuliza hili swali kupata maoni, sio hapa tu ni kwenye majukwaa mbalimbali, Asante kwa wote waliotoa maoni yao.
Mkuu 'FM WOLLE', kukusaidia kupata jibu sahihi kwa swali lako, nami ningependa nikuulize wewe na wasomaji wako wengine swali, ambalo kama mnaweza kulijibu kwa usahihi, basi swali lako nalo litakuwa limepata jibu:

Kuna nchi ngapi duniani ambazo zilishapata maendeleo kutokana na misaada?

Usikimbilie kujibu hili swali bila ya tafakuri makini juu yake, kama kweli nia yako ya kutaka jibu ya swali lako ni halali.
 
Back
Top Bottom