Kwanini Marekani ameshindwa kuimaliza Iran haraka?

mabazazi na mandunya sidhani kama wamekuelewa...mkuu hivi unafahamu kwamba mabazazi na mandunya wengi wao ni ccm?
 
😄😄
 
Hoja kuu ya MALCOM LUMUMBA ambayo ninaiona inamashiko ni Wairan bado wengi wanamshikamano na serikali yao.
Hiyo ndio hoja kuu.

Kwamba Marekani na Israel vita hii itakuwa ngumu kwao kushinda au itachukua muda mrefu kushinda kwa sababu bado Iran inanguvu ya umoja baina yao.

Kwamba Wamerakani wameshindwa kuwagawanya wa Iran. Tofauti na Marekani alivyotarajia.

Hii itapelekea ugumu kwa Marekani kuvamia Iran kijeshi kwa kutumia Majeshi ya ardhini.
Na kama hakuna majeshi ya ardhini itamaanisha lengo la regime change halitafikiwa.
Naona hiyo ndio hoja yako kubwa.

Lakini mpaka sasa Iran yupo kujihami, anajitetea na Hana lengo na hawezi kushinda kwa kusema amuangamize adui yake.

Ukweli ni kuwa Marekani na Israel hii vita wanaitaka, na kwao ni muhimu kushinda. Na Hilo litatokea tuu.

Kwa vile Marekani na Israel nao ni watu kama watu wengine. Ikitokea Wameshindwa kufikia Malengo basi mambo mengi yatabadilika hapo Mashariki ya Kati lakini pia Mtazamo wa mataifa duniani kumhusu Mmarekani
 
So Kama Hali ndio Iko hii it means fair treat katika siasa haipo na haiwezi kuwepo , Kwa muktadha huu inaweka wazi kwamba Russia ana haki ya kujilinda dhidi ya adui na kama alifuatwa hatua za kidiplomacy kutaka kumaliza mgogoro halafu hakusikilizwa basi Hilo ndio linalo mpaka mandate kabisa ya kufanya kile alicho kifanya
 
🤣 Mnanini lakini !? Halafu wamefumba macho na masikio
 
...lakini kusema kwamba NATO+EU wataiangusha ni jambo lisilowezekana. Mataifa makubwa huwa yanafanya makosa pia (Political Blunders)​
Waliweza kuingausha USSR kwasababu ya ukubwa na uchumi. Russia ya leo haiwezi kugawanyika , in fact nchi zilizojitoa zinasikitika. Urusi kama Taifa kubwa ilifanya kosa! kudharau nguvu ya Uzalendo.
Putin alidhani ataingia Kiev kama mkata keki. Kipigo cha mwanzo kilimvuruga na kuijengea Ukraine confidence.
Vijana wengi sijui ni kwa kutojua, kiburi , uzembe au udumavu!! hoja hii hawaioni kabisa.

Iran inapigana na Mataifa zaidi 9. Ni Iran iliyo katika vikwazo vya uchumi kwa miaka 40.
Iran haipigani vita, inapigania Survival.

Iran inaangaliwa kwa 'jicho la kengeza ''biased''inatuhumiwa kushambulia majirani bila kujua inapigania survival. Israel ilipopiga Gaza, Lebanon , Syria, Tunisia, Yemen na Qatar ilisemwa hiyo ni ''self defense''.

Donald J Trump alisema ni siku nne tu baada ya Ayatollah kulambishwa mchanga basi, Iran ingekuwa kaputi.​
Trump aliwatimua Makamanda walioshiriki vita za nyuma kwa kudhani wanamhujumu.

Makamanda hawakukubali ''ndio mzee'' kwahiyo akapoteza '' institution memory ya Pentagon''
Jaribio la Venezuela likamtia kiburi kwamba Pentagon wanaweza kufanya lolote Duniani

Nia ya Trump ni ''TACO'' kwamba anatisha bila kufanya jambo kuilazimisha Iran ikubali masharti.

Vyombo vya usalama 'kwa taarifa ya jana'' vilimweleza tatizo la kumuua Ayatollah
Trump hakupenda lakini kuna nguvu nyingine, Israel isiyotaka majadiliano bali Iran apigwe.

Waziri wa mambo ya nje M.Rubio amethibisha kwa kauli kwamba hawakutaka lakini Israel ilisema itamuua Ayatollah bila USA. Hilo likawalazimu Marekani kujiunga katika Vita.

Kumuua Ayatollah Khamenei kwa kudhani wananchi wataingia mtaani kuchukua nchi ni kosa.

Vita ya siku 12 ilionyesha Wananchi wa Iran waliungana badala ya kutengana.

Maandamano yanayoratibiwana Israel na Marekani yana watu maelfu lakini kuna mamilioni Wanaipenda serikali yao. Kwa mfano, baada ya kuuawa mamilioni waliingia mtaani licha ya mabomu kurindima katika mitaa yao.
Marekani kweli kawatandika Iran, lakini nao wamemtandika vibaya mno. Mara ya mwisho kambi za kijeshi za Marekani zimelipuliwa hivi ilikuwa ni mwaka 1941 kule Pearl Harbour ambapo Japan aliua zaidi ya wanajeshi 2000. ​
Hakuna kambi ya US iliyobaki pale middle east. Nani amewahi kufanya hivyo katika miaka 85!
Jambo la kushangaza kulikuwa na silaha za ulinzi za kisasa kabisa kwenye hizo kambi kama THAAD na PATRIOT ambazo zilikuwa na mfumo bora kabisa wa rada duniani ambao umelipuliwa.​
Kama utakumbuka , sehemu ya kwanza Iran kushambulia ni ile RADAR kubwa middle east.
Walipoiondoa kukakosekana muundo wa kuona makombora.

Kilichotumika ni THAAD na PATRIOT kutumiwa kuangusha Drone ya USD 25K.

Kwasasa hakuna tena air defense pale middle east, THAAD na PATRIOT zilizobaki zimehamishiwa Israel.
Nchi za Kiarabu zimejawa na jazba kwamba zimetumika na ulinzi umehamishiwa Israel.
Vita ya siku 12 iliwa andaa sana Iran, hata hivyo kuna usaidizi wa kiitentelejensia kutoka ''within''
Uchunguzi unaendelea kuhusu ndege 3 zilizotunguliwa Kuwait kukiwa na hisia za hujuma.

Intelijensi ya Iran ni rahisi sana ku penetrate middle east kwasababu ya madhebu.
Kwa mfano kuwait na Qatar kuna Shia wengi. Ndivyo ilivyokuwa kwa UAE, Saudi na Oman
Iran ina wasomi wa maana sana. Siku ya kwanza ya shambulio waliuawa Wasichana zaidi ya 100.

Watu hawajiulizi kwanini waliuawa Wasichana? Marekani na Israel hawajatoa madai yoyote ya eneo la shule kuwa la kijeshi. Kwa taarifa, shule ile ni ya Watoto wenye vipaji katika science.

Iran ina literacy level katika 99 kukiwa na University ambazo Wanawake ni wengi kuliko wanaume.
Iran ni vinara wa mathematics na sayansi ya anga. Nyuma ya computers kuna akili za Wairan

Ni wazuri sana wa Teknolojia .Wasomi wa Iran wanatumia makosa kujifunza
Vita na Iraq, wameona ya Libya na hata vita ya siku 12. Wametumia wataalamu kujifunza
Iran wame survive miaka 40 ya vikwazo, wamegeuza vikwazo kama kichocheo cha maendeleo yao.
MADHARA ENDAPO VITA HAITAISHA MAPEMA:

Mosi
, The Aura of American Invincibility has been shattered before the world. Zile propaganda za kusema hakuna wa kumgusa Marekani hazipo tena. Iran katuonesha kwamba Marekani na Israel wanagusika.
​
In fact Iran kaonyesha matundu ya Marekani, na Trump anajitahidi sana pa kutokea vita isiendelee.
Waandishi wa habari wanahoji vifo! ingawa ni siri na tunajua Trump hataki kuonekana ameshindwa, ipo siku watu watabaini vifo si 6 !

Iran imethibtisha yale ambayo vijana hawakuyaona. Kwa miaka mingi tumeeleza hapa kwamba Israel haiwezi kusimama yenyewe, ipo katika mbeleko ya USA. Vijana wakasema ni Taifa lenye nguvu sana za kijeshi. Tel Aviv inatekea! Iron dome, David sling, Arrow, THAAD, PATRIOT Zote zimefeli.
Iran imepiga kila taasisi ya ulinzi ya Israel na kila kona iliyosemwa haiguswi.

Vita iliyopo sasa ni ya Marekani na washirika, Israel inatajwa tu lakini ukweli ni kwamba inapigwa sana
Hebu sasa fikiria, endapo Uchina ataamua kuvamia Taiwani​
Marekani haingii
True!
 
Muulize siyupo karibu na Cuba Nini kilicho tokea baada ya kuvamia Cuba !? 😄
 
Till now mitazamo ya watu imeshaanza kubadilika kama Nina kupa hadhi / dhamana ya kunilinda and still Nina shambuliwa wakati wewe mlinzi wangu upo so what do you expect!?? .

Wewe ulitegemea kuona kitu kama hicho !?
 
Iran ni taifa dogo kushinda marekani lakini USA ain't having an easy way.

Marekani hawezi kupigana vita bila kuwa na allies ambae kwa sasa ni waarab(wote wamechezea) na Israel.

Iran anasurvive peke yake, pamoja na kwamba amekuwa kwenye economic sanctions kwa miaka zaidi ya 40 sasa.

Waajemi sio wamatumbi kwamba you can have an easy route.
 
Wewe jamaa tangu uandike uongo uongo kule kwenye uzi wa mgogoro wa Urusi na Ukraine, inahitaji kusoma mara mbili mbili unachoandika.
Kwa hiyo nyinyi mnafurahi taifa moja kuua political leadership ya taifa jingine kisa vita???Hiyo ni sign ya weakness sio nguvu.Nguvu inatambulika kwenye utiifu wa sheria za kimataifa, sio kulipua watu na nchi kisa una jeshi kubwa, nguvu kubwa etc.
Pili mlitaka Urus wamle kichwa Zelensky ili tu awafurahishe watu kama nyinyi et ndo nguvu hizo au sio???Umesahau Putin alimuhakikishia waziri mkuu wa Israel kipindi kile kuwa hatomgusa Zelensky???Uo ndo uongozi...
Vita sio betting, au Simba na Yanga, kwamba mna-prove ubishi wenu kwa kutembea na roho za watu.
Et Urusi hatawali anga, mosi hujui kuwa kuna vijeba vimejichimbia pale -NATO na air defenses za Kutosha, utalinganisha na Iran??
Pili Urusi anawezapiga popote kwa missiles akitokea kwake, kwa nini ahangaike kuweka rehani maisha ya airforce yake wakati ana alternative??Makombora tu na drones zinagusa kila kona..

US atashinda pambano pale Iran lakini hatshinda vita...BATTLES yes, atawatwanga kwelikweli lkn kushinda vita sio rahisi pale, nchi kubwa ile, milima na mapango kama yote
[/QUOTE]

Vita ya Urusi niliandika uongo gani, miaka minne iliyopita?

Political leadership haitakiwi kuuwawa ila inategemeana na mazingira, umeona Rais wa Iran anauwawa?
Sasa Ayatollah yeye main policy yake ni "Death to Israel" na haiachi miaka zaidi ya 40 sasa wafanyeje na wameishajizuia miaka mingi kumsitiri, Ayatollah atakayedumu atakaa kwa heshima. Mbona Hezbollah na Hamas nao wamejiheshimu baada ya kila kiongozi anayejifanya amechanganyikiwa, anauwawa.
Ni sheria za wanasiasa hizo ili kujilinda vita ikitokea, ili wapange mipango ya kipuuzi kutuma vijana wa watu wakafie frontline huku nyuma wao wanakula na kusaza. Kukiwepo tishio la kuwaua ndio sense inakaa kichwani mwao wanatafuta suruhisho haraka.
Viongozi wa kijeshi mara nyingi wanauwawa wakiwa kwenye majukumu ya kijeshi, ama yupo kambini au frontline au kwenye ammo dump au anakagua utekelezaji wa mikakati ya vita.

Hilo la air defense systems Iran ilinunua za Urusi na China, na hazijasaidia almost lolote. Iran ilitakiwa inunue fighter jets hasa Su-35 za Urusi zingewasaidia sana ila Urusi wenyewe ndio marafiki wanafiki.
 
Huo umbali ndio mojawapo kinachoitofautisha Marekani na Iran, na ndio kinachodhihirisha ubovu wa Urusi maana wapo karibu na Ukraine tofauti na mada na tittle yake.

Ayatollah mpya hajatangazwa rasmi, maana Assembly of Experts haijakaa kutokana na tishio la vita. Ila Mojtaba kijana mkubwa wa Khamenei anatajwa kama mrithi, inaonekana mazingira ya uchaguzi atapita na hasa IRGC inamtaka yeye.
Ingawa sio msomi wa juu kabisa kidini ila kisiasa ana uzoefu underground alikuwa anaendesha mambo kadhaa. Ni hardliner, misimamo kama ya baba yake hivyo simkubali sana kwa enzi za sasa ambazo zina maandamano, uchumi mbovu kabisa na vikwazo vingi. Atakuja kutaka consolidation of power jambo litakalotegemea kama ana uwezo sana au kama hana uwezo nchi inapata hasara kwa muda mrefu.

Wakati Ali Khamenei anachaguliwa alikuja kuwaunganisha watu, hakuwa mtu wa juu kabisa wala mwenye mizizi sana kama ambavyo mwanae alivyo sasa. Napendelea Ayatollah ajaye awe kama Khamenei alivyokuwa wakati anachaguliwa. Pia influence ya Ayatollah ipungue kiasi ili Rais, bunge, Guardian Council na Assembly of Experts viongeze maamuzi zaidi. Tatizo Ayatollah ndio kama anateua wote hao sasa ukileta mzoefu sana ni shida (maana atakuwa mdini lialia) na ukileta mgeni kabisa watamsumbua wazoefu.

Hata interim huyu Ayatollah Alireza Arafi bado simkubali sana naona ni hardliner, ila bora yake kuliko Mujtaba. Iranians wanataka mtu soft kidogo ambaye si msomi mkubwa wa kidini tu bali msomi labda wa sayansi au uchumi ili concentration yake iwe kukuza uchumi kupunguza ugumu wa maisha, kukuza teknolojia, biashara, standard of living ili baadae wajikusanye wakitaka kupigana na Israel. Sio sasa atokee kichwa ngumu waendelee kuumia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…