Kwanini Manji anaandamwa na huu utawala?

Kwanini Manji anaandamwa na huu utawala?

Manji amepatwa misukosuko mingi tangia hawa vibosile wakamate ulaji kwa sababu kubwa moja tu wakati Wa mchakato Wa uraisi ndani ya CCM alimpigia debe la nguvu Membe.

Yale maburunkutu yalidakwa baadaye yakatakatishwa na polisi kuwa hayakuwa na dhamira ya kuhonga wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM bali yalikuwa ya kuendesha shughuli za mfanyabiashara huyo.

Membe alipodondoka na Manji khali yake kisiasa ikaingia matatani.

Iwe Koko Beach, iwe ni Yanga na sasa madawa ya kulevya Manji anasomeshwa namba na chama chake.

Visasi ndiyo mkakati uliopo lakini pia kumdhoofisha kiuchumi na kisiasa asiweze kufurukuta na kuwa na ushawishi wowote chaguzi zijazo.

Unapoona kibosile anakerwa gari la Manji kuoshwa Central Police na kama yeye angelikuwa ni IGP angeona cha mtema kuni ujue huo ni uhasama mtupu na visasi.

Kwani kuosha gari polisi ni kuvunja sheria ipi hadi kibosile autamani u-IGP?

Manji ikumbukwe alianza kutajirika wakati wa Mwinyi, Mkapa na JK wakamneemesha vilivyo kwa madili kebekebe sasa ni wakati wake Wa kusoma namba.

Akina Professa Kapuya waliomnyoshea njia wako kwenye mawe na ndiyo maana anasoma namba ila hajaielewa......ukiona hata maamuzi ya mahakama vibosile hawa wanayapuuza ujue hii ni vita ya "survival of the fittest."

Acha kujikomba na kujipendekeza wewe, Polisi ni sehemu ya kuoshea magari ya watuhumiwa kenge wewe unaandika upumbavu huna hata chembe ya huruma na nchi yako katika wote umemuona Manji peke yake ficha upumbavu wako wewe huoni hiyo ni dharau kwa nchi na serikali kwa ujumla?
 
Hivi huyu alikuwa anatokea kampuni gani vile?

20150711062922%2B%25281%2529.jpg
 
Kwani Makonda si mlisema ni Team Membe.?
Na mkasema huwa anakutana na Membe Kumuhujumu Rais..
Na pia kwa mujibu Wa Msukuma Juzi Bungeni Ni Kwamba 'Makonda Alikuwa Analelewa Na kuishi Kwa Membe'..How Come Tena mseme Makonda Anamkomoa Manji Kwasababu Ya Mahela Ya Membe.?

Bavicha Stop This Please..
Unachanganya na Sitta we ndo huelewi kumbe
 
Hahaha
It always works, angalia Museveni Uganda, Angalia Kagame, it will work kwake pia.
1. Keep your opponents silent, wasiwe na uwezo wakukuchafua and keep your citizens silent wasiwe na uwezo wa kujiuliza.
2. Keep them poor, so yuo can corrupt them during election.
3. Keep telling lies on how uli ikuta nchi ime oza , so they will see hata hivo umejitahidi and you are patriot than the former regime .
4. Keep other two branches of govet under your influence, so maovu yako yasi fichuliwe.
5.keep the press silent, so you wont be accountable to any one.
6. Befriend Military and police forces, in case things are not working so you can spress any resistance.

Hapo unaweza kuongoza hata milele. Na ndio anacho fanya jamaa.
Umeandika point za mashiko viongozi wa ki Africa huwaza madaraka na kuogopwa ka miungu licha ya nchi nyingi kupata Uhuru wake lakini siku zinavozidi kwenda ndo umaskini unazidi kila kukicha hao kina kagame, museveni Mugabe hadi watafiwa madaraka ni, ka bara letu linatia aibu, mbaya huwa tunapata viongozi wajuaji kuliko.
 
Visasi visasi vya kijinga.

Haya ndiyo yale mambo watu wakisikia umekufa wanafanya sherehe.

Niombeeni.
Hujui watu wanakuombea nini.

Hayeni
Visasi ni kitu kibaya sana hakijengi zaidi ya kubomoa hata maandiko yatuasa tusilipe kisasi maana ni juu ya Mungu.
 
Kila jambo lina wakati wake. Nalo hili litapita tu.
 
Ukoo wa Manji ni matajiri toka enzi za mwl wakiwa na Quality garage ya kuunda mabodi ya magari. Huyu dogo ame neemesha zaidi utajiri wao sasa mkulu anataka kimfilisi ama kimfunga.
 
Mahaba jambo baya sana.Kuitwa polisi tayari mtu anaandamwa??!!
 
Mahaba jambo baya sana.Kuitwa polisi tayari mtu anaandamwa??!!
 
Sheria wapi wakati Makonda kaingilia Kazi ya tume ambayo iko kisheria sasa haki itapenya wapi.
Haki za watuhumiwa wote waliotajwa na Makonda zimekiukwa inabidi wafutiwe makosa yote na waendelee na shughuli zao.
Wafutiwe makosa? Makosa gani mkuu sibado wengine hawajafikishwa mahakamani.
Sasahivi wanatuhumiwa tu.
Tuhuma zisipo dhibitishwa wakitaka wafungue kesi ya madai kudhalilishwa.
 
Haha apo nje 2 ile ndani kama first class ya ndege" au sijui alimaind jamaa kufutia na bendera ya ccm [emoji23] sio kwa kumaindi kule.
Ile chuma si mchezo
Hahaaaaaaa gari hatari ile ujue sipati picha huko ndani kukoje maana series za week ilopita si mchezo kwa kweli shabiki hadi akachanganyikiwa Mara waumini wa gwajima waimbe bora hili swala limeisha taharuki ilishazidi mno.
 
Rutashubanyuma

Manji utajiri aliukuta toka enzi za baba'ke na pengine hata babu yake.

Nyerere hakumtaifisha baba'ke kwa sababu maalum.

Labda wakati wa Mwinyi aliongezea utajiri kwa kuwa tayari walikuwa na mitaji mikubwa kwenye familia yao.
Kwa heshima yako,tunaomba utueleze kwanini Nyerere hakumtaifisha baba yake? Je una maana huu mfupa Magufuli hauwezi????
 
Wakati Wa Nyerere kulikuwa na cha kuiba kweli hesabu zangu zaonyesha miamala ya QUALITY GROUP ndiyo imemnenepesha vilivyo.

Kwa Mujibu wa Report za World Bank, Fedha zimeanza kuchotwa na kwenda kufichwa Uswizi 1974!
 
Hahaaaaaaa gari hatari ile ujue sipati picha huko ndani kukoje maana series za week ilopita si mchezo kwa kweli shabiki hadi akachanganyikiwa Mara waumini wa gwajima waimbe bora hili swala limeisha taharuki ilishazidi mno.
Watu ad walisahau kutafuta hela wale wanakula story tu, mondi kajuta kutoa marry you msimu huu [emoji23] [emoji23] [emoji23] "
 
Back
Top Bottom