Kwanini Manji anaandamwa na huu utawala?

Kwani Makonda si mlisema ni Team Membe.?
Na mkasema huwa anakutana na Membe Kumuhujumu Rais..
Na pia kwa mujibu Wa Msukuma Juzi Bungeni Ni Kwamba 'Makonda Alikuwa Analelewa Na kuishi Kwa Membe'..How Come Tena mseme Makonda Anamkomoa Manji Kwasababu Ya Mahela Ya Membe.?

Bavicha Stop This Please..
Somji, wa bili havai moja
 
Una ushahidi mana sasa mnalalamika watu wanavunjiwa heshima. We unachofqnya nini. Ogopa sana mtihani wa kutunga mwenyewe. We hapa sema mtu hana kosa mi wakili wake kesi tumemaliza alionewa.
Hakimu mkuu sio wakili
 
Nikweli lakini hainamaana kwamba tajiri hawezi kukosea.
Saazingine sisi wenyewe tumekua tukilala mika kwamba maranyingi matajiri hawashugulikiwi wanapo kosea kwasababu ya pesazao.
Ngoja sheria ifuatemkondowake kama hana hatia ataachiwa.
Point yangu haija mlenga Manji tu, yaani Magu ki ujumla akiona mtu ana pesa nadhan huwa ina muuma
 
Wao wanajali madaraka tu nyie Watanzania kufeni na shida zenu kwa kukosa huduma muhimu wao hawajali, sasa wakimuona mtu ana support upinzani indirect wanamuundia zengwe maana wa naona wataharibiwa ulaji.
Sasa awamu hii ndo maskini jeuri haswa hawajali shida za watu wao full ubabe, bora punda afe ila mzigo ufike.
Ni matumbo yao sisi tunaambulia vitisho vyao tuogope wale.
 
Manji amepatwa misukosuko mingi tangia hawa vibosile wakamate ulaji kwa sababu kubwa moja tu wakati Wa mchakato Wa uraisi ndani ya CCM alimpigia debe la nguvu Membe.

Yale maburunkutu yalidakwa baadaye yakatakatishwa na polisi kuwa hayakuwa na dhamira ya kuhonga wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM bali yalikuwa ya kuendesha shughuli za mfanyabiashara huyo.

Membe alipodondoka na Manji khali yake kisiasa ikaingia matatani.

Iwe Koko Beach, iwe ni Yanga na sasa madawa ya kulevya Manji anasomeshwa namba na chama chake.

Visasi ndiyo mkakati uliopo lakini pia kumdhoofisha kiuchumi na kisiasa asiweze kufurukuta na kuwa na ushawishi wowote chaguzi zijazo.

Unapoona kibosile anakerwa gari la Manji kuoshwa Central Police na kama yeye angelikuwa ni IGP angeona cha mtema kuni ujue huo ni uhasama mtupu na visasi.

Kwani kuosha gari polisi ni kuvunja sheria ipi hadi kibosile autamani u-IGP?

Manji ikumbukwe alianza kutajirika wakati wa Mwinyi, Mkapa na JK wakamneemesha vilivyo kwa madili kebekebe sasa ni wakati wake Wa kusoma namba.

Akina Professa Kapuya waliomnyoshea njia wako kwenye mawe na ndiyo maana anasoma namba ila hajaielewa......ukiona hata maamuzi ya mahakama vibosile hawa wanayapuuza ujue hii ni vita ya "survival of the fittest."
Na wewe una matatizo ya problem! Hivi JPM alikutenda nini?
 
Sasa kwani kweny ile Press conference lile Range Rover lake nalo liliongea Jeuri? Maana nalo Mzee wa White House Alisema nalo lilipaswa kuwekwa Mahabusu na akamlaumu Sirro kwa hilo!
Ni uhasama tu hapo hakuna darasa jingine.
 
Nikweli lakini hainamaana kwamba tajiri hawezi kukosea.
Saazingine sisi wenyewe tumekua tukilala mika kwamba maranyingi matajiri hawashugulikiwi wanapo kosea kwasababu ya pesazao.
Ngoja sheria ifuatemkondowake kama hana hatia ataachiwa.
Sheria wapi wakati Makonda kaingilia Kazi ya tume ambayo iko kisheria sasa haki itapenya wapi.
Haki za watuhumiwa wote waliotajwa na Makonda zimekiukwa inabidi wafutiwe makosa yote na waendelee na shughuli zao.
 
Manji amepatwa misukosuko mingi tangia hawa vibosile wakamate ulaji kwa sababu kubwa moja tu wakati Wa mchakato Wa uraisi ndani ya CCM alimpigia debe la nguvu Membe.

Yale maburunkutu yalidakwa baadaye yakatakatishwa na polisi kuwa hayakuwa na dhamira ya kuhonga wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM bali yalikuwa ya kuendesha shughuli za mfanyabiashara huyo.

Membe alipodondoka na Manji khali yake kisiasa ikaingia matatani.

Iwe Koko Beach, iwe ni Yanga na sasa madawa ya kulevya Manji anasomeshwa namba na chama chake.

Visasi ndiyo mkakati uliopo lakini pia kumdhoofisha kiuchumi na kisiasa asiweze kufurukuta na kuwa na ushawishi wowote chaguzi zijazo.

Unapoona kibosile anakerwa gari la Manji kuoshwa Central Police na kama yeye angelikuwa ni IGP angeona cha mtema kuni ujue huo ni uhasama mtupu na visasi.

Kwani kuosha gari polisi ni kuvunja sheria ipi hadi kibosile autamani u-IGP?

Manji ikumbukwe alianza kutajirika wakati wa Mwinyi, Mkapa na JK wakamneemesha vilivyo kwa madili kebekebe sasa ni wakati wake Wa kusoma namba.

Akina Professa Kapuya waliomnyoshea njia wako kwenye mawe na ndiyo maana anasoma namba ila hajaielewa......ukiona hata maamuzi ya mahakama vibosile hawa wanayapuuza ujue hii ni vita ya "survival of the fittest."
Asante kwa kutujuza mkuu Luna mengi hapa yawezekana hawa wengine kupoteza maboya tu time will tell us
 
Ni matumbo yao sisi tunaambulia vitisho vyao tuogope wale.
Ili muwaogope wafanye watakayo na wapendavyo ndo maana walianza na bunge live. Na ifike mahali bunge liisimamie serikali bila kujali vyama vyao na mahakama ziwe huru ziache kufunga watu kisa wametumwa na viongozi wa juu.
 
Kama anaonewa arudi kwao Uhindini au aende kwa Trump si ana passport 2
 
Manji ambaye ni Mwenyekiti wa Kampuni ya Quality Group Limited (QGL) anasema safari yake ya kuongoza kampuni hiyo ilianza rasmi mwaka 1995 akiwa na umri wa miaka 20 baada ya kupokea mikoba kutoka kwa baba yake, Mehbub Manji aliyekuwa akiongoza kampuni ya vifaa vya magari.
Hata hivyo, Manji anasema yeye siyo tajiri na kwamba ni mfanyakazi tu katika kampuni hiyo na baada ya baba yake kufariki alimuachia hisa zote mama yake na yeye kubaki msimamizi anayelipwa mshahara kama wafanyakazi wengine.
Manji anasema kwa miaka 20 amemudu kuanzisha kampuni tanzu 17 ambazo zinajishughulisha na biashara 102 zikiwamo za maendeleo ya makazi, usambazaji wa vyombo vya moto, biashara ya kimataifa, vyakula na huduma za uchukuzi katika nchi 28 duniani.
Kwa mujibu wa mfanyabiashara huyo, usimamizi wa kampuni hizo haukuja kwa bahati mbaya kwake na badala yake ilikuwa ni matokeo ya kujituma kufanya kazi bila kuchoka kwa moyo wake wote.
“Mara kadhaa nimekuwa nikilala ofisini kwa siku tatu mpaka nne kutokana tu na kuwa na kazi nyingi, hili si wengi wanaoweza kuamini, lakini ndio ukweli kuhusu maisha yangu,” anasema.
Ratiba yake kwa siku
Manji anasema kwa kawaida huwa anaamka saa 10:15 usiku kila siku ili kuhakikisha hachelewi kazini kwani anaamini kulala sana ni dalili za uvivu.
“Ninapoamka tu naaza kwa kufanya mazoezi, kisha nasali na kuondoka nyumabani. Saa 12:00 asubuhi huwa nafika ofisini kwangu kwa ajili ya ujenzi wa Taifa,” anafafanua.

YUSUF MANJI : Wakati mwengine nalala ofisini kutokana na kazi
 
Back
Top Bottom