Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,181
Manji amepatwa misukosuko mingi tangia hawa vibosile wakamate ulaji kwa sababu kubwa moja tu wakati Wa mchakato Wa uraisi ndani ya CCM alimpigia debe la nguvu Membe.
Yale maburunkutu yalidakwa baadaye yakatakatishwa na polisi kuwa hayakuwa na dhamira ya kuhonga wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM bali yalikuwa ya kuendesha shughuli za mfanyabiashara huyo.
Membe alipodondoka na Manji khali yake kisiasa ikaingia matatani.
Iwe Koko Beach, iwe ni Yanga na sasa madawa ya kulevya Manji anasomeshwa namba na chama chake.
Visasi ndiyo mkakati uliopo lakini pia kumdhoofisha kiuchumi na kisiasa asiweze kufurukuta na kuwa na ushawishi wowote chaguzi zijazo.
Unapoona kibosile anakerwa gari la Manji kuoshwa Central Police na kama yeye angelikuwa ni IGP angeona cha mtema kuni ujue huo ni uhasama mtupu na visasi.
Kwani kuosha gari polisi ni kuvunja sheria ipi hadi kibosile autamani u-IGP?
Manji ikumbukwe alianza kutajirika wakati wa Mwinyi, Mkapa na JK wakamneemesha vilivyo kwa madili kebekebe sasa ni wakati wake Wa kusoma namba.
Akina Professa Kapuya waliomnyoshea njia wako kwenye mawe na ndiyo maana anasoma namba ila hajaielewa......ukiona hata maamuzi ya mahakama vibosile hawa wanayapuuza ujue hii ni vita ya "survival of the fittest."