Habari ya leo wanajumuia wa hapa, Leo nimeona tushirikiane juu ya jambo hili. Niende moja kwa moja kwenye Mada.
Miaka ya karibuni K umekuwa nana ongezeko kubwa la ndoa zinazofungwa lakini matokeo yake asilimia kubwa ya ndoa hizo hazidumu, mpaka tunajiuliza kulikoni mbona walipendana vya kutosha imekuaje? Mbona harusi yao ilifana sana? Ndani ya mwaka mmoja wameachana sababu ni :-
1. Wanawake kufanya harakati kwenye ndoa, hapa wanawake wanafika kwenye ndoa wakiwa na akili ya kutaka haki sawa, kitu ambacho kwenye tasisi ya ndoa hakipo kabisa, mwanaume ameumbwa na amepewa mamla ya kutawala tangu pale Mwanadamu wa kwanza kuasi pale bustani ya Edeni(Mwanzo;3:16, "Akamwambia mwanamke, Hakika nitakuzidishia uchungu wako na kuzaa kwako, utungu utazaa watoto na tamaa yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala") kwahiyo maana yake ukiolewa uko chini ya utawala wa Mume, ukitaka usawa maana yake hakuna maana ya mwanamke kuolewa bali kuoa.
2. Utii; Wanawake siku hizi wamekosa utii labda kwa sababu kuna taasisi nyingi zipo kwa minajili ya kutetea haki zao, au pengine ni kutokana na Elimu waliyoipata utii umekosekana mwanamke ili adumu kwenye ndoa utii kwa mume unamhusu, kwa wakristo wale walokole wanakosa utii kwa waume zao matokeo yake wanapeleka utii kwa wachungaji wao wa kiroho, wenyewe ni mashahidi ndoa za wengi wao zimevurugika na kashfa kibao kosa ni kukosa utii( kolosai 3:18) imempasa mwanamke kumtii mume wake katika hali yeyote huo utii kwa kiingereza wametumia neno submissive yaani utii ukiwa na unyenyekevu, neno utii limesisitizwa pia waefeso 5:22-24, 1petro 3:1-2.
Mtasema mbona umeongelea wanawake tu na sio wanaune , wanawake ndo wamepewa dhamana kuijenga ndoa na ndo maana ukisoma mithal inasema mwanamke mpumbavu huibomoa nyumba kwa mikono yake maana yake MWANAMKE mwerevu huijenga.
Niwatakie siku njema