Kwanini mahusiano/ndoa nyingi hazidumu?

Kwanini mahusiano/ndoa nyingi hazidumu?

Tatizo binadamu ni wabishi sana...

Changamoto za kukabiliana shida na raha... Uzuri na karaha...

Watu wanatoleana mapovu mpaka kufikishana pabaya kwenye mambo madogo sana, ambayo mmoja angesema nimekosa nisamehe mambo yangekuwa shwari...


Cc: mahondaw
 
Babu na bibi zetu mpaka Leo wapo kwenye mahusiano .. Unakuta wtu wanatimiza miaka 60 ya kuish pamoja

Lakin kizaz Chetu ndoa zmekua zikivunjika kila kukichwa...nilishuhudia mke akipewa talaka siku moja baada ya harusi

Zama hzi ndoa ikifkisha miaka 10 ujue watu wamevumiliana sana...
Je, nini kinasababsha hili janga??

1) usaliti?
2) kutokua makini wakat wa kuchagua mwenza?
3) wanandoa kutojua wajibu wao?
4) utandawazi unachangia?

Tujadiliane huu Uzi wakuu
Ndoa ndoana bora mm ambae sitaoa
 
Uongo uliotukuka ktk mahusiano na kukosekana kwa uaminifu ndio chanzo cha yote hayo.
 
Wanaume wanatakiwa kuishi na wake zao kwa akili, ndoa nyingi zinavurugika kwa kufikiri pesa ndio kila kitu, badala ya kuishi nao kwa akili.
 
Tatizo la siku hizi, mwanaume akitega, mwanamke naye anatega.... Mwanaume ukishafungulia, upande wa pili unamalizia
 
Ujua mwingi kila mtu kujiona anajua mambo.....
Kutosikilizana na kujishusha mmojawapo
Sababu ni nyingi mzee,so inategemea na wahusika.
Kuwa na michepuko mingi hapo ndo dharau zinakuja maan utaona akwambii kitu mkiachna unajua wengi wanakutaka kumbe ni akili za usiku, mara nyingi ukiwa kwa mahusiano huoni faida ila ukitoka ndo unajua kumbe kule kutamu kuliko ulivyokuwa unaona nje!
 
, kubwa ni uvumilivu kitu ambacho hakipo siku hizi kwa wote tena wanaume na wanawake

Nilitaka ni comment lakini nilivyo fika hapa nikaona hakuna umuhimu tena wakuendelea kusoma comments wala kuandika nilichotaka kuchangia.

Zaburi 133:1 tazama ilivyopendeza jinsi ndugu,wanandoa wakae pamoja na kuwa umoja.( maana yake WANANDOA ni kitu kimoja kosa la mmoja ni la wote hivyo nguzo kuu ni kuvumiliana)
 
Hasa kosa ni kutokuwa makini wakati wa uchumba. Uchumba wa mda mrefu hata kama mmoja akaficha makucha iko siku atajisahau na utamgundua. Ukiwa makini hata baada ya ndoa tatizo likiwepo ni mapenzi ya Mungu. Fanya uchunguzi wa kina wakati wa chumba na ndoa itadumu kama wazee wa zamani.
 
Back
Top Bottom