Kwanini Lowassa anakwepa kuzungumzia ufisadi?

Kwanini Lowassa anakwepa kuzungumzia ufisadi?

Ameamua kujipanga kukemea hadharani wale wote wanaojihusisha na rushwa na ufisad. Amedai kuwa wanalitia aibu taifa letu.
Hiyo nimeipata kutoka kwa wapambe wa Lowassa a.k.a team Lowassa kuwa mzee wao kaamua kuja na style hiyo ya kukemea rushwa na ufisadi pengine labda inaweza kumtoa kimasomaso kwenye kinyang'anyiro cha urais 2015 October.

Hahahaha hahahaha hahahaha...........! Hii kali ya mwaka
 
mi sioni tatizo lolote kwenye kukemea rushwa kwa bongo...kila mtu saiz anakemea rushwa kila kona ...kukemea sio ishu..ishu ni kuizuia..!! mwache akemee tu kwani kuna tatizo...mi mwenyewe kila siku nakemea na nikikutana na traffic njiani akinikamata ndo wa kwanza kumpa buku tano!! Sasa utafanyaje...na maisha ndo yalivyo hivi tanzania..
 
Kama kweli ana ubavu amuibue DHAIFU kwa kuigeuza Ikulu kuwa danguro la mafisadi na kuwakumbatia wapokea rushwa ndani ya Ikulu kwa kuwataja majina Gurumo na wenzie wote na kutaka wafukuzwe kazi mara moja, warudishe pesa zote mara moja na wote wapandishwe kizimbani kwa kulihujumu Taifa. Pia amshinikize DHAIFU kuiweka hadharani ripoti ya wapokea rushwa kupitia bank ya STANBIC na siyo kuishia kubwabwaja tu na kauli zisizo na mashiko.

Ameamua kujipanga kukemea hadharani wale wote wanaojihusisha na rushwa na ufisad. Amedai kuwa wanalitia aibu taifa letu.
Hiyo nimeipata kutoka kwa wapambe wa Lowassa a.k.a team Lowassa kuwa mzee wao kaamua kuja na style hiyo ya kukemea rushwa na ufisadi pengine labda inaweza kumtoa kimasomaso kwenye kinyang'anyiro cha urais 2015 October.
 
propaganda za kitoto hizo... Lowassa hana muda wa kuongelea Obvious ...
 
Ndani ya CCM unakemea UFISADI? Watu wanapiga deal ndani ya Ikulu, wenye kujinadi kuwa wao ni wasafi ndo wezi wakubwa tena wengi wao wako kwenye Cabinet!!! Lowassa kukaa kimya kunawafanya Jamaa wamuogope na wako tayari kuwaachia CHADEMA na Ukawa nchi kuliko Lowassa... Wamemshughulikia Komba huku wao wakigawana ngawira za ESCROW live bila Chenga .. Lowassa mbona hayuko kwenye List ya EPA, ESCROW, Mikataba ya Madini, Wauza Sembe??? ... Angalia mambo kiundani kiuhalisia kabla ya kuropoka ndugu ... JKN mwenyewe alizimishwa baada ya kuja kuujua ukweli...
Hana muda wa kukemea ufisadi eti eeh! Ila ana muda wa kupiga ufisadi tu au?
 
Mbona watetezi wa Lowassa wanagwaya kumtetea kwenye hii thread? Au kweli huyu mtu kasingiziwa eeh? Shetani ataokoka nadhani siku kauli hii ya mtoa mada ikiwa kweli
 
Back
Top Bottom