Kwanini Lowassa anakwepa kuzungumzia ufisadi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini Lowassa anakwepa kuzungumzia ufisadi?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Zak Malang, Oct 12, 2012.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Oct 12, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Ni swali ambalo huwa linanitatiza sana, labda wadau mnaweza kunikumbusha ni lini, tuseme tangu baada ya uchaguzi mkuu uliopita au hata kabla huyu mjamaa ambaye inadaiwa anautaka urais kwa udi na uvumba, amezungumzia ufisadi.

  Ni katika kikao, mkutano au hafla gani amewahi kulizungumzia suala hilo ambalo majority ya Watz linawakera na linaashiria kutuletea machafuko huko tuendako.

  Jibu la mara moja linaloonekana ambalo ni plausible ni kwamba mtu huyu binafsi kaguswa na ufisadi, ni mtuhumiwa wa kansa hiyo, hivyo hawezi kulizungumzia kwa kulikemea kwa nguvu zote, labda wakati anafanya hivyo, macho yake ayaelekeze chini.

  Wasiwasi wangu ni kwamba akitiunga Ikulu, hawezi kulishughulikia suala hilo, atakuwa kama huyo mwenzake aliyepo sasa hivi. Ni nadra sana JK kuzungumzia ufisadi katika hafla za hadhara, hata katika kampeni zake za 2010, mada hii alikuwa anaikwepa sana. Tusisahau alikwepa midahalo na akina Slaa na Lipumba bila shaka kukwepa suala la ufisadi ambalo lazima lingeibuliwa.

  Hivyo EL akitinga Ikulu, ina maana kwamba kwa miaka 20 suala la ufisadi hapa nchini halitakuwa linapiganwa kwa dhati.

  What a waste of time. Watz tuamke, tusidanganyike hapa.
   
 2. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #2
  Oct 12, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Mkuu, ni kweli hata mimi sijamsikia akitoa comment zozote kuhusu ufisadi uanoitafuna nchi. Ni tofauti kabisa na wanaodaiwa kuwa mahasimu wake -- kwa mfano Sitta au Mwakyembe. Lakini siyo Membe, Membe naye ni kama EL, huwa hazungumzii ufisadi vile vile.

  Nimetafakari sana suala hili na kugundua kuwa mtu kama Sitta hana mali zozote za kutisha, hana tuhuma za ufisadi. Natoka naye mkoa mmoja, -- hana kitu ukilinganisha na wengine wanaotajwa -- akina Vijisenti, Ngeleja, Maige, EL mwenyewe, et al. Nadhani hata Mwakyembe, mwenye data za tuhuma za Mwakyembe aziweke hapa, angalau moja. Nadhani naye hana kitu.

  Ukweli unabakia pale pale -- kwamba mtu fisadi humuwia ugumu sana kulizungumzia suala hilo kwa nguvu zote. Anaweza akataja tu kwa kupita lakini siyo kwa nguvu sana.

  Nakubaliana nawe kwamba EL akiingia Ikulu, basi tushuhudie miaka kumi mingine ya danadana tu na ulimbikzaji mali kwa vigoigo wa CCM -- a.k.a. hasa wale wanaokula bila kunawa.
   
 3. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #3
  Oct 12, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Yaani hata ufisadi ndani ya chama chake, katika chaguzi zinazoendelea haoni kama ni kero? Au hazioni kama ni dhambi? Nataka siku moja atafute ujasiri na aseme "Vitendo vya rushwa katika chaguzi vitatupeleka pabaya!'

  Thubutu aseme hivyo? Siku akisema hivyo siku ya pili jua litatoka magharibi na kutua mashariki.
   
 4. M

  Mzee Kipara Member

  #4
  Oct 12, 2012
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 83
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 15
  Umeongea jambo ambalo watanzania wote wanatakiwa walitafakari, we dont want ten more years of irresponsibility and squandering of national resources. Ila sijui kama sredi yako itadumu, mara nyingi sredi zinazoainisha madhara ya Lowasa kuwa rais huwa zinadissapear.
   
 5. h

  hans79 JF-Expert Member

  #5
  Oct 12, 2012
  Joined: May 4, 2011
  Messages: 3,802
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 145
  Yeye ndiye unategemea ataongea,
  si alikimbia swali la mwanafunzi kuhusu dhana ya utawala bora.
   
 6. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #6
  Oct 12, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Kwenye red: Umemsahau Magufuli. Huwa anazungumzia sana ufisadi, lakini kwa kiini macho tu.

  Kwa mfano, atasema wizara yake imejaa mafisadi, lakini hata siku moja hatujasikia yeyote kafikishwa mahakamani.
   
 7. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #7
  Oct 12, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Kwanza kabisa as certain as next sunrise, EL akitinga Ikulu 2015, lile gamba lililoamua kulivua gamba lake (RA) atarudi ulingoni kwa kishindo! Kwa hiyo business as usual!

  Hivi lini Mungu atasikia kilio cha Watz?
   
 8. Maxence Melo

  Maxence Melo JF Founder Staff Member

  #8
  Oct 12, 2012
  Joined: Feb 10, 2006
  Messages: 2,606
  Likes Received: 1,704
  Trophy Points: 280
  Mnampandisha Lowassa tu, kwanini tusifikirie tofauti kidogo? Ndio maana hata watoto wa wanasiasa hawa wanajiona kuwa watoto wa wafalme na kuamini kuwa 'Ninyi watanzania ni wa kutawaliwa tu'. We need to change this attitude.

  Sitarajii RA ajiingize kwenye siasa moja kwa moja tena hapa TZ, atafanya biashara zake na wanasiasa na ataiendesha nchi kwa remote lakini si moja kwa moja kama unavyotarajia. Kumbuka, tayari anadaiwa kuwa na mkono kwenye uchaguzi wa Kenya!
  Hapa Mungu mnamwonea tu, hata mimi ningekuwa Mungu, ningewaangalia tu. Mnaamshwa, hamtaki kuamka. Mnamwagiwa maji yenye ubaridi mwingi, mnashtuka na kukung'uta vichwa, mnajipangusa nyuso kisha mnarejea usingizini.

  Hapa mnastahili adhabu kali, si kuonewa huruma kwa kilio chenu.
   
 9. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #9
  Oct 12, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  angalau huyu huwa anawataja kama alivyo mtaja ritta mlaki akiwa naibu waziri wake kipindi hicho km sikosei lakini Magufuli hakuhojiwa matakukuru wala takukuru mbaya zaidi ritta hakukamatwa sasa hapa nani mwenye maksa
   
 10. lakiwosha

  lakiwosha Senior Member

  #10
  Oct 12, 2012
  Joined: Sep 9, 2012
  Messages: 198
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 45
  mi hapa naona kama kuna mambo mawli

  mosi, ni kama ulivosema kwamba anaona aibu kulizungumzia kwa sababu alivokuwepo alikuwa mstari wa mbele kula rushwa kwa hiyo inakua kazi kwake kuligusia kwa sababu wenzake watamnyoshea kidole

  pili, inawezekana vilevile ana jambo ambalo ni gumu kwake kulisema ukizingatia anweza kuwaletea wenzake matatizo kama alivosema mwenyewe "kufanya maamuzi magumu"
   
 11. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #11
  Oct 13, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  nafsi inamsuta sana hataweza kuzungumzia suala kama hilo na isitoshe yeye ni mwanachama wa chama kinachowasujudia
   
 12. m

  mharakati JF-Expert Member

  #12
  Oct 13, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 1,275
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  mfumo huu unawabana sana watu wengi ndani ya CCM na serikali (wale angalau wanapenda kufanya kazi) kwa sababu nakumbuka kuna wakati CAG alipochukua ofisi alitaka kumfuta mama mmoja kazi kwa kudharau kanuni za ofisi, lakini yule mama akamwambia thubutu, itatoka barua ikulu ikimueleza CAG simfukuze mtu kazi. CAG akanywea...jiulize wangapi wana dhamira lakini wanabanwa na mfumo, wako wengi sana na hiki siyo kiini macho ni mazingira na tamaduni yenyewe ya kazi.

  angalia Tibaiujuka na yule jamaa wa NHC, kimya sasa hivi pamoja na kwamba wanania sana ya kufanya kazi, baada ya muda tunawapoteza kabisa wanakua watu wa system tu.

  Tusiwe wanafiki tuwapongeze wale wachache wanaojaribu kama akina Mwaky, magufuli au sitta, kwani wengi wamenyamaza tu
   
 13. Japhari Shabani (RIP)

  Japhari Shabani (RIP) R I P

  #13
  Oct 13, 2012
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 721
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Anafahamu nini kinachoendelea katika chama chake CCM Chama Cha Mafisadi sio mnafiki kama walivyo viongozi wengi ndani ya CCM wanasimama majukwaani kukemea ufisadi na rushwa,wakati vitendo,maisha na kauli zao hazioani.Kusimama majukwaani na kuhubiri vita dhidi nya ufisadi wakati sera ya CCM kivitedo ni ufisadi ni unafiki.
   
 14. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #14
  Jul 7, 2013
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Nimekuwa nafuatilia kwa ukaribu sana hotuba na kauli za Lowassa akiwa sehemu mbali mbali hapa nchini na kuonyesha kero zake katika masuala mbali mbali katika jamii ambayo anayaona hayaendi vizuri. Mfano ni ajira kwa vijana, elimu duni na kadhalika.

  Yote hayo ni sahihi, lakini mwanasiasa huyu mkongwe inabidi ajiulize kwa nini masuala hayo yamekuwa ni chagamoto kubwa kwa jamii ya Tanzania. Jee hataki kukubali kabisa kwamba ufisadi katika ngazi za juu za uongozi wa serikali inayoongozwa na chama chake ndiyo kwa kiasi kikubwa unachangia serikali hiyo kushindwa kutatua masuala hayo?

  Haamini kwamba sehemu kubwa za bajeti zinazopangiwa sekta mbali mbali za maendelea zinaishia mifukoni mwa wachache? Haamini kwamba mikataba ya siri ya makampuni ya uchimbaji wa madini, mafuta na gesi ni ufisadi mtupu na ndiyo maana iko siri?

  La mwisho: Lowassa haziamini kabisa habari kwamba wapo vigogo wachache waliowekewa fedha katika mabenki ya Uswisi na makampuni ya nje yanayojishughulisha na utafutaji/uchimbaji wa gesi hapa nchini -- na kwa nini hata siku moja hazungumzii suala hilo ambalo wananchi wengi wanachukizwa nalo?
  Haoni kwamba serikali inapiga danadana tu katika kuwabaini akina nani hao na kudai kuzirejesha?
   
 15. Imany John

  Imany John Verified User

  #15
  Jul 7, 2013
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 2,778
  Likes Received: 262
  Trophy Points: 180
  “Tunataka tuwasaidie hawa vijana wetu, maana ni nguzo kubwa sana katika maendeleo ya taifa. Ilani ya CCM inasema lazima watu wawezeshwe kiuchumi.

  “Kwa maana hiyo katika nchi yetu kila mtu lazima ale. Na kula kwenyewe tunatofautiana, huyu anakula mkate na huyu anakula hiki. Na ili amani iwepo lazima RPC au OCD na wafanyabiashara wawathamini machinga,” alisema Lowassa.
   
 16. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #16
  Jul 7, 2013
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Yaani hapo kwa tathmini yako EL ameongelea kukerwa kwa ufisadi? hata kama ameoingea ki-mafumbo, sijalibaini fumbo lenyewe.
   
 17. Imany John

  Imany John Verified User

  #17
  Jul 7, 2013
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 2,778
  Likes Received: 262
  Trophy Points: 180
  Itakuchukua miaka kunielewa.
   
 18. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #18
  Jul 7, 2013
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Siku atakapoongelea ufisadi -- hasa ufisadi wa ngazi za juu (siyo rushwa za matrafiki na manesi) nitampa kura yangu bila kufikiri mara mbili -- iwapo atagombea urais.
   
 19. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #19
  Jul 7, 2013
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0


  Nikimsikia akizungumzia kukerwa na ufisadi mie nitajitundika -- kweli kabisa! Ni kama vile komredi wake JK naye hawezi kuzungumzia ufisadi majukwaani kwa njia ya bila kutafuna maneno.
   
 20. Mnyamwezi wa Urambo

  Mnyamwezi wa Urambo JF-Expert Member

  #20
  Jul 7, 2013
  Joined: Dec 7, 2011
  Messages: 932
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Sheikh Lowassa.jpg
   
Loading...