ni vema kujua Nini maana ya Neno "Fisadi" kama linavyotumika na waswahili.Kwenye Siasa Fisadi ,ni pale mtu anapotumia Ofisi ya Umma kwa maslahi yake binafsi.
kuna tabia mbaya imezuka kwa Watanzania ya kupenda Kula maneno ya Wanasiasa haswa wakiwa pale bohari Dodoma lilipo Bunge letu tukufu,
Mtanzania ataweka kumbukumbu ya hotuba zilizoamsha hisia kwa kusheheni maneno ya kejeli na vijembe lakini hatoweka kumbukumbu ya utendaji wa Kiongozi juu ya maneno Yale Yale aliyoyasikia kwa viongozi wengine.
Mimi nawajua Viongozi waliokemea Ufisadi waziwazi lakini walipoukuta sehemu zao hawakuushughulikia zaidi tu ya kufanya reshuffle,yaani viongozi hao wanamsimamo wa wazi juu ya Ufisadi ambao kimsingi umekithiri Serikalini na maeneo yao ya kazi ila cha ajabu hawana record ya kufanya maamuzi magumu Katika hilo na kuwasimamisha kazi Hata watu wawili kwa juhudi zao binafsi
lakini pia namjua Kiongozi mwenye Record ya kuongea kidogo na kutenda sana ,Hakika hajalisha watu maneno Bali kwa matendo yake hakuishia kusema tu juu ya ufisadi Bali alionyesha nini cha kufanya kwa nafasi yake pale alipokutana nao
sasa chagua Leo Unataka speech za kukemea ufisadi ama Unataka kuona nini unatakiwa ufanye pindi unapokutana nao.