screpa
JF-Expert Member
- Sep 10, 2015
- 10,792
- 15,693
EL anahangaika bure uraisi ataishia kuusikiliza kwenye radio.
VOTE FOR UKAWA
haha hii comment sahivi bilashaka hutaki kuiona
EL anahangaika bure uraisi ataishia kuusikiliza kwenye radio.
VOTE FOR UKAWA
Wewe jipongeze tu, safari hii MAJIZI ya ESCROW, MEREMETA, KAGODA, EPA n.k na yenye kujimilikisha migodi, mbuga za wanyama n.k IKULU BASI TENA.Ni swali ambalo huwa linanitatiza sana, labda wadau mnaweza kunikumbusha ni lini, tuseme tangu baada ya uchaguzi mkuu uliopita au hata kabla huyu mjamaa ambaye inadaiwa anautaka urais kwa udi na uvumba, amezungumzia ufisadi.
Ni katika kikao, mkutano au hafla gani amewahi kulizungumzia suala hilo ambalo majority ya Watz linawakera na linaashiria kutuletea machafuko huko tuendako.
Jibu la mara moja linaloonekana ambalo ni plausible ni kwamba mtu huyu binafsi kaguswa na ufisadi, ni mtuhumiwa wa kansa hiyo, hivyo hawezi kulizungumzia kwa kulikemea kwa nguvu zote, labda wakati anafanya hivyo, macho yake ayaelekeze chini.
Wasiwasi wangu ni kwamba akitiunga Ikulu, hawezi kulishughulikia suala hilo, atakuwa kama huyo mwenzake aliyepo sasa hivi. Ni nadra sana JK kuzungumzia ufisadi katika hafla za hadhara, hata katika kampeni zake za 2010, mada hii alikuwa anaikwepa sana. Tusisahau alikwepa midahalo na akina Slaa na Lipumba bila shaka kukwepa suala la ufisadi ambalo lazima lingeibuliwa.
Hivyo EL akitinga Ikulu, ina maana kwamba kwa miaka 20 suala la ufisadi hapa nchini halitakuwa linapiganwa kwa dhati.
What a waste of time. Watz tuamke, tusidanganyike hapa.