Kwanini jimbo la Kawe limetoka kupelekewa miradi mikubwa ya maendeleo badala yake linapelekewa jezi za mpira? Tunakwenda wapi kama Taifa?

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
877
4,106
Kuna majimbo ambayo tunapaswa kuwainua wananchi kwa kuwapelekea sukari na maziwa na majimbo ambayo tunapaswa kupeleka miradi kuboresha miundombinu hili uzalishaji ukue

Jimbo la kawe ni jimbo la kimkakati katika nchi ambalo lina jamii ya daraja la kwanza. Jimbo kama lile linahitaji zaidi lami mitaani, vituo vya afya, kuboresha madarasa, kuongeza masoko nk

Leo Mbunge wa kawe naona for three years now hana jambo kubwa analopeleka kwenye jimbo, hakuna miradi wa mkakati alionao na wala hana hoja serious aliyopeleka bungeni.

Ameona uchaguzi serikali za mtaa umekaribia ameanza drama za kwenda na vyombo vya habari na vijana wasio na kazi kwenda kugawa mipira na jezi........kwanini tunadhalilisha matajiri? Kawe kata gani ambayo wakaazi wake wameshindwa kununua mpira na jezi?
 
Mbona amejitahidi sana Mbunge wetu...
Ametengeneza miundombinu na Tunashukuru amesimamia sana swala la Maji maeneo yakwetu Madale na Mivumoni
 
Back
Top Bottom