Mbunge wa Jimbo la Mwanga akagua Miradi ya Maendeleo, Kusikiliza Kero za Wananchi

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,897
942
MBUNGE wa Jimbo la Mwanga Joseph Tadayo amefanya ziara kukagua miradi ya maendeleo pamoja na kusikiliza kero za wananchi katika vijiji vinne vya kata ya Toloha na Kwakoa wilayani humo mkoani Kilimanjaro.

Katika ziara hiyo Tadayo ameambatana na wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Wilaya, ambapo wamekagua miradi ya elimu pamoja na kufanya mikutano ya hadara na kusikiliza kero za Wananchi.

Akizugumza wananchi mara baada kukagua miradi ya maendeleo Mbunge Tadayo amesema Serikali ya Awamu ya Sta chini ya Rais Dkt Samia Suluhu imepeleka fedha nyingi katika Jimbo la Mwanga kwa ajili ya miradi ya maendeleo ikiwemo hospitali ya wilaya, jengo la halmashauri , ujenzi wa shule mpya za kata Kivisini na Toloha, ujenzi chuo cha kisasa cha ufundi.

Amesema miradi mingine ni pamoja miradi ya barabara,maji na kilimo cha mwagiliaji, na kwamba lengo la Serikali ni kutoa huduma bora kwa Wananchi.

Ametoa mwito kwa wananchi kuendelea kusimamia miradi mbalimbali inayotekelezwa na sirikali katika maeneo yao ili iweze kutekelezwa kwa viwango vinavyotakiwa kulingana na fedha zilizotolewa.

Amasema Serikali ya Dk.Samia Suluhu Hasan ipo makini katika kutekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya mwaka 2020/2025 na kwamba imeendelea kutekeleza miradi mikubwa ya kitaifa.

Amesema katika kuhakikisha wananchi wanakuendelea kukiamini chama cha Mapinduzi CCM Serikali imeweka kipaumbele kusikiliza kero za Wananchi na ikiwa ni pamoja na kuchukua maoni

Ameongeza jimbo la Mwanga ni miongoni mwa majimbo ambayo yamenufaika na miradi mikubwa ya kimkakati na kwamba bado fedha zinaendelea kuletwa.


IMG-20230713-WA0032.jpg
IMG-20230713-WA0031.jpg
IMG-20230713-WA0029.jpg
 
Back
Top Bottom