Ziara ya Daniel Sillo Katika Jimbo la Babati Vijijini Kukagua Miradi ya Maendeleo

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944

ZIARA YA MHE. DANIEL SILLO KATIKA JIMBO LA BABATI VIJIJINI NA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO

Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini na Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti bungeni Mhe. Daniel Sillo ameendelea na ziara katika Jimbo la Babati Vijijini ambapo ametembelea Vijiji 66 kati ya Vijiji 102 vya babati vijijini huku akielezea Mafanikio na kusikiliza Changamoto za Wananchi na kukagua Miradi ya Maendeleo.

Mhe. Daniel Sillo kuanzia tarehe 21.02.2023 alianza ziara katika Vijiji vya Kakoyi na Vilima Vitatu Kata ya Nkaiti; Kijiji cha Gichameda Kata ya Magugu na kuwaahidi wananchi kwenda kuzifanyia kazi Changamoto zote na zingine kuzipeleka ngazi husika, yaliyopo ngazi ya Kata, Ofisi ya Kata ishughulikie.

Mhe. Sillo aliwaeleza wananchi miradi mikubwa iliyotekelezwa ndani ya kipindi chake ikiwemo Ujenzi wa Barabara ya Kakoyi; Mradi wa Maji wa Kata ya Magugu na Nkaiti - Mwada na Kisangaji wenye thamani ya Bilioni 5.6; Umeme wa REA; Na, Ujenzi wa daraja la Gichameda lililofikia 95% la shilingi bilioni 1.2.

Katika hatua nyingine Mhe. Daniel Sillo amekabidhi Mabati 160 kwaajili ya ujenzi wa jengo la Ofisi ya Kijiji cha Duru Kata ya Duru Wilayani Babati Mkoani Manyara ikiwa ni utekelezaji wa ahadi yake aliyoitoa hapo awali.

Mwenyekiti wa CCM Kata ya Qash, Iddy Matata amesema tangu kijiji cha Tsamas kiundwe mwaka 1974 hakikuwahi kuwa na barabara Mpaka Mwaka 2023 baada ya Mbunge Daniel Sillo kushughulikia. Wananchi wataka jina la barabara iitwe jina la Daniel Sillo ambayo ilikuwa haipitiki na sasa inapitika.

Mhe. Daniel Sillo alishiriki ziara ya Katibu Mkuu CCM Ndugu Daniel Chongolo na Sekretarieti katika Jimbo la Babati Vijijini. Pia, alishiriki Matembezi ya Vijana wa Chama cha Mapinduzi na Maafisa usafirishaji maarufu "Bodaboda" Mkoa wa Manyara Wilaya yaliyoongozwa na Ndugu Mohamed Kawaida.

Vilevile, Wananchi wa Babati Vijijini walimpa Mbunge salamu za kumfikishia Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa aliyowafanyia wana Nkaiti na Taifa kwa Ujumla huku wakimpongeza Mbunge wao kwa kazi nzuri anayoifanya jimboni.

WhatsApp Image 2023-03-11 at 17.41.41.jpeg

WhatsApp Image 2023-03-11 at 17.41.40(1).jpeg

WhatsApp Image 2023-03-11 at 17.41.38(2).jpeg

WhatsApp Image 2023-03-11 at 17.41.48(1).jpeg

WhatsApp Image 2023-03-11 at 17.41.45.jpeg

WhatsApp Image 2023-03-11 at 17.41.43(2).jpeg
 
Back
Top Bottom