Kwanini hela ya Kenya ina thamani zaidi, tena mbali kuliko ya Tanzania wakati tumebarikiwa kila kitu?

kenya wazungu bado wapo hawakuwafukuza kama sisi .viwanda vingi ni vya wazungu wana export sana kwa wazungu wenzao ulaya mashemeji nk
Kwamba wazungu ndio factor. Ooh please!

Kwamba sisi hatukuwa na viwanda? Vilikwenda wapi? Kwamba bila kuwa wazungu hatuwezi kuwa tuna export?

Hivi visababu visivyo na kichwa wala miguu vinatufanya vipofu. Tunashindwa hasa kuona sababu halisi!
 
Jambo moja linalonipa shida kuliko hata kuibiwa kura ni hili la hawa wakenya jirani zetu, hela yao ipo na thamani kubwa sana sana kuliko za kwetu -- tatizo ni nini?

Na kila siku tunajilabu tuna utajiri uliotukuka, naikumbuka ile sentensi ya Mwalimu Nyerere. Watanzania Uchumi mnao...

Tufanye nini ili tuwapite maana tuwe tunashinda kwa mazuri na moja ni hela yetu kuwa na thamani. Saa ingine huwaza lile tarajio la Tanzania kuwepo uchumi wa kati, au ndio tumekwisha jaaliwa yaani haiwezi badilika?
Sababu Kenya kuna covid 19 ,,Tanzania hatuna,,very simple..
 
Hera ya kenya ina thamani kubwa lakini hera ya Tanzania ina nguvu zaidi ya manunuzi

mfano ukiwa na Elfu moja Tz unanunua vitu vingi kuliko ukiwa kenya

hivyo basi sisi tupo vizuri zaidi kuliko kenya
MMMmmmh nasubiri ufafanuzi. Naona kama vile unaongea kitu na kujipinga mwenyewe.
 
kenya wazungu bado wapo hawakuwafukuza kama sisi .viwanda vingi ni vya wazungu wana export sana kwa wazungu wenzao ulaya mashemeji nk
Wenzetu wana friendly and conducive environment for foreign investments, mzunguko wao wa pesa ni mkubwa na uko stable kiasi kwasababu wanaoshika pesa nzuri kule wako wengi comparing to Tanzanians.
 
Tanzania maji ya 1/2 lita ni Tsh 500/=,
Kenya maji ya 1/2 lita ni Ksh 50/=

Ukifanya hesabu maji ya 1/2 lita Kenya ni ghali kuliko Tanzania kwa zaidi ya mara mbili zaidi.
Tofauti yake inakuja pale mnapoagiza toka nje. Inabidi wote mtumie dolari.

Tungetunga sera bora na kuzisimamia. Tusingekuwa tunajilinganisha na Kenya bali na the like of South Africa et al. Tunapaswa kujitazama upya kama nchi. Sisi ni bora kuliko hapa tulipo!
 
Tofauti yake inakuja pale mnapoagiza toka nje. Inabidi wote mtumie dolari.

Tungetunga sera bora na kuzisimamia. Tusingekuwa tunajilinganisha na Kenya bali na the like of South Africa et al. Tunapaswa kujitazama upya kama nchi. Sisi ni bora kuliko hapa tulipo!
Hapo nimekusoma vizuri.
 
Hata almasi na dhahabu wanazo kila kona na wanatapeliwa kwa mikataba mibovu.

Siyo lazima wawe na kila tulichonacho 1:1, hata wao wana vitu ambavyo sisi hatuna, isistoshe Almasi ya Tanzania wala siyo nyinbgi hivyo kama mnavyofikiria, ...
 
Mtoa mada nikukumbushe tu kua hela ya japani (japaneese Yen) ina thamani almost sawa na hiyo shilingi ya kenya lakini hiyo haimaanishi uchumi wa japani na Kenya zinakaribiana.
 
Jambo moja linalonipa shida kuliko hata kuibiwa kura ni hili la hawa wakenya jirani zetu, hela yao ipo na thamani kubwa sana sana kuliko za kwetu -- tatizo ni nini?...
Kwanza hesabu idadi ya viwanda walivyinavyo kwa miaka mingi na vinavyoendelea kujengwa.Pili kuna daily flight ya Nairobi -London na baadhj ya nchi za ulaya, jiulize hapa kwetu tuna flights ngapi angalo kwa wiki za kubeba abiria na export products na je tuna viwanda vingapi vinavyozalisha bidhaa za ku-export nje.

Ukishapata majibu tulia unywe Maji.
 
Shilling moja ya Kenya ipo karibu Sawa na yen moja ya Japan so kiuchumi haimanishi Kenya ipo karibu Sawa na Japan kiuchumi, so kaa ukijua exchange rate si kigezo ktk kupima nguvu za kiuchumi ktk nchi!
 
Hela ya Kenya ina thamani kubwa lakini hela ya Tanzania ina nguvu zaidi ya manunuzi

Mfano ukiwa na Elfu moja Tanzania unanunua vitu vingi kuliko ukiwa Kenya

Hivyo basi sisi tupo vizuri zaidi kuliko Kenya
Ati nini?
 
Kenya wazungu bado wapo hawakuwafukuza kama sisi, viwanda vingi ni vya wazungu wana export sana kwa wazungu wenzao Ulaya mashemeji nk
Sisi wazungu tumewafukuza. Tunakwama wapi? Kwa nini hatufikii hata Morrocco tu? Maana nao walifukuza wafaransa.
 
Back
Top Bottom