Kwanini hela ya Kenya ina thamani zaidi, tena mbali kuliko ya Tanzania wakati tumebarikiwa kila kitu?

Shocker

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
1,625
2,000
Jambo moja linalonipa shida kuliko hata kuibiwa kura ni hili la hawa wakenya jirani zetu, hela yao ipo na thamani kubwa sana sana kuliko za kwetu -- tatizo ni nini?

Na kila siku tunajilabu tuna utajiri uliotukuka, naikumbuka ile sentensi ya Mwalimu Nyerere. Watanzania Uchumi mnao...

Tufanye nini ili tuwapite maana tuwe tunashinda kwa mazuri na moja ni hela yetu kuwa na thamani. Saa ingine huwaza lile tarajio la Tanzania kuwepo uchumi wa kati au ndio tumekwisha jaaliwa yaani haiwezi badilika?
 

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
30,509
2,000
Kenya pia ni shamba la bibi la wazungu

Mzungu anaabudiwa sana kule aweza toka hata Marekani akawa mpiga debe au kondakta wa daladala bila shida akiwa bado raia wa Marekani na bila kuomba kibali cha kazi tofauti na sisi ona mpiga debe na kondakta huyu mzungu toka marekani

 

ismailjf

Member
Aug 5, 2011
37
95
Jambo moja linalonipa shida kuliko hata kuibiwa kura ni hili la hawa wakenya jirani zetu,hela yao ipo na thamani kubwa sana sana kuliko za kwetu tatizo ni Nini ...
Kaka mimi sio mchumi lakini ni kweli fedha ya Kenya kwa miaka zaidi ya 15 imeandelea kucheza kati ya 1Kshs = Tshs 18 - 22. Lakini hiyo haimaanishi uchumi wetu sio mzuri, ila kinachoangaliwa ni thamani ya hiyo fedha inaweza kufanya nini. Kama Mkate mmoja unaweza kununuliwa kwa Tshs. 1,000 ya Tanzania, Je ukienda ukachenji hiyo Tshs. 1,000 na kupata fedha ya Kenya, ambayo ni almost Ksh.47.6 JE UNAWEZA KUPATA MKATE WA SIZE KAMA ULIONUNUA TANZANIA KWA TSHS. 1,000?.

Jingine limesemwa na mchangiaji hapo juu, cha msingi tuzalishe zaidi, pindi tutakapouza vingi nje, watahitaji kununua Shilingi yetu kwa wing, na hapo ndipo fedha yao itashuka thamani kuliko ya kwetu.

Nimejaribu kidogo, Wachumi wabobezi wataweza kuliweka sawa zaidi
 

King Kisali

JF-Expert Member
Nov 20, 2019
1,004
2,000
Jambo moja linalonipa shida kuliko hata kuibiwa kura ni hili la hawa wakenya jirani zetu,hela yao ipo na thamani kubwa sana sana kuliko za kwetu tatizo ni Nini?...
Nchi inaongozwa na mtu elimu yake inatiliwa shaka, Ina utata, hata maamuzi yake ni ya utata, hayafuati sheria, katiba, kanuni na miongozo ya utumishi, maamuzi yake yanaangalia nani? Na itegemea ameamkaje? Siku hiyo unategemea nini? Uchumi wa kati wa kusadikika .
 

Imapro

Member
Apr 18, 2012
75
125
Uchumi hauna uhusiano na exchange rate,Kwa taarifa yako sio kenya tuna wanatuzidi thamani kuna majirani kama malawi,Rwanda na Burundi hela zao zina thamani kuliko zetu.China na India thamani zao ziko chini lakini matajiri tu
 

Bulamba

JF-Expert Member
Sep 17, 2011
11,756
2,000
Nchi inaongozwa na mtu elimu yake inatilwa shaka , Ina utata , hata maamuzi yake ni ya utata ,hayafuati sheria , katiba , kanuni na miongozo ya utumishi , maamuzi yake yanaangalia nani ? Na itegemea ameamkaje ?siku hiyo unategemea nini ? Uchumi wa kati wa kusadikika .
Vipi kuhusu uchumi wa Zimbabwe na exchange rate yao??Asante
 

Stefano Mtangoo

JF-Expert Member
Oct 25, 2012
5,319
2,000
Jambo moja linalonipa shida kuliko hata kuibiwa kura ni hili la hawa wakenya jirani zetu, hela yao ipo na thamani kubwa sana sana kuliko za kwetu -- tatizo ni nini?...
Pata muda soma sheria zetu zinazogusa vyanzo vya uchumi. Soma sera zetu vizuri. Ukimaliza njoo uulize swali sasa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom