Kwanini hela ya Kenya ina thamani zaidi, tena mbali kuliko ya Tanzania wakati tumebarikiwa kila kitu?

Ukiwa na shiling elfu kumi Tanzania utanunua vitu vingi lakini ukichukua hiyohiyo elfu kumi ukaenda nayo kenya hautonunua vitu vingi kama ulivyonunua Tz so thamani ya shiling ikiwa ndogo kuna faida saana (hasa kwa nchi zinazozalisha bidhaa nyingi)
MMMmmmh nasubiri ufafanuzi. Naona kama vile unaongea kitu na kujipinga mwenyewe.
 
Jambo moja linalonipa shida kuliko hata kuibiwa kura ni hili la hawa wakenya jirani zetu, hela yao ipo na thamani kubwa sana sana kuliko za kwetu -- tatizo ni nini?

Na kila siku tunajilabu tuna utajiri uliotukuka, naikumbuka ile sentensi ya Mwalimu Nyerere. Watanzania Uchumi mnao...

Tufanye nini ili tuwapite maana tuwe tunashinda kwa mazuri na moja ni hela yetu kuwa na thamani. Saa ingine huwaza lile tarajio la Tanzania kuwepo uchumi wa kati au ndio tumekwisha jaaliwa yaani haiwezi badilika?
Unajua shilingi ya Kenya inafanana thamani ya Yen ya Japan? Je, uchumi wa Kenya unafanana au ni mkubwa kuliko wa Japan?
 
Jambo moja linalonipa shida kuliko hata kuibiwa kura ni hili la hawa wakenya jirani zetu, hela yao ipo na thamani kubwa sana sana kuliko za kwetu -- tatizo ni nini?

Na kila siku tunajilabu tuna utajiri uliotukuka, naikumbuka ile sentensi ya Mwalimu Nyerere. Watanzania Uchumi mnao...

Tufanye nini ili tuwapite maana tuwe tunashinda kwa mazuri na moja ni hela yetu kuwa na thamani. Saa ingine huwaza lile tarajio la Tanzania kuwepo uchumi wa kati au ndio tumekwisha jaaliwa yaani haiwezi badilika?
Nawe usiwe mvivu! Unaposema thamani una maana gani? Au una maana ya exchange rate? Kuna watu nhamtaki kutumia hata muda kidogo kujifunza elimu ya wengine kwa kuwa tu hamkufundishwa darasani. Exchange rate is nothing! Muhimu ni stability ya currency. Uzembe wa swali lako uko hapa, Jiulize juu ya uhusiano wa Euro, US dollar na TZS.
 
Hela ya Kenya ina thamani kubwa lakini hela ya Tanzania ina nguvu zaidi ya manunuzi

Mfano ukiwa na Elfu moja Tanzania unanunua vitu vingi kuliko ukiwa Kenya

Hivyo basi sisi tupo vizuri zaidi kuliko Kenya
Wachache watakuelewa. Wengi hawajui chochote kuhusu nguvu ya manunuzi ya pesa.

Ukiwa na shilingi 50 ya Kenya ni sawa na Shilingi 1000 ya Tanzania. Je unaweza kufanya manunuzi gani na hizo pesa. Kisha linganisha utajua pesa ipi ina nguvu zaidi.
 
MMMmmmh nasubiri ufafanuzi. Naona kama vile unaongea kitu na kujipinga mwenyewe.
Haujaelewa mkuu, chukua shilingi 1000 ya Tanzania ununue vitu hapa TZ, kisha hiyo hiyo 1000 vuka mpaka kisha ibadili kuwa shilingi ya kenya ununue vitu huko Kenya kisha linganisha.

Hapo ndipo utaelewa ni kwanini Mmarekani huwa ana mlalamikia mchina anapopunguza thamani ya kubadilisha pesa zake kimataifa.

Hili nalo vilaza watalidandia mbele na kuleta sababu za kipuuzi
 
Naona watu wanazungumza hata vitu wasivyojua. Kama wewe siyo mchumi basi jaribu hata kugoogle. Zamani fedha yetu ilikuwa na nguvu sana je unajua kilichoipunguza? Tuanzie hapo kwanza ukishaelewa uje tujadili mada sasa.
 
Ukiwa na shiling elfu kumi Tanzania utanunua vitu vingi lakini ukichukua hiyohiyo elfu kumi ukaenda nayo kenya hautonunua vitu vingi kama ulivyonunua Tz so thamani ya shiling ikiwa ndogo kuna faida saana (hasa kwa nchi zinazozalisha bidhaa nyingi)
Hakika mkuu, mnakuwa rahisi katika soko la dunia na ndicho hata China amekifanya kuzipiku nchi za Ulaya na Marekani hadi walikuwa wanamlalamikia.

Suala hapa ni sisi kuzalisha kwa wingi tunakuwa cheap katika soko la Afrika Mashariki. Mfano mzuri pia Mtanzania akiend Uganda atajikuta bidhaa za Uganda ni bei ndogo kushinda Tanzania. Hii pia inajidhihirisha kwenye change rate pesa yetu ipo juu kidogo kushinda Uganda
 
Na je ya RWANDA mbona nayo ina thamani kuliko ya TZ na wao hawana wazungu. Nchi ni mkoa mmoja wa TZ lakini mmmh hela ya inapita ya TZ kwa thamani, kwanin
 
Kiufupi ni hivi shilingi ya Tanzania kuwa na Thamani ndogo kuliko majirani zetu kuna faida zaidi kwa Tz hasa hichi kipindi ambacho Tz inapambana kuwa mzalishaji mkuu East Africa
Na je ya RWANDA mbona nayo ina thamani kuliko ya TZ na wao hawana wazungu. Nchi ni mkoa mmoja wa TZ lakini mmmh hela ya inapita ya TZ kwa thamani, kwanin
 
Mtoa mada nikukumbushe tu kua hela ya japani (japaneese Yen) ina thamani almost sawa na hiyo shilingi ya kenya lakini hiyo haimaanishi uchumi wa japani na Kenya zinakaribiana.
Na mimi nikukumbushe 1966 wakati tulipoachana na matumizi ya East Africa Schilling na kila nchi kuanza kutumia fedha zake Shilingi ya Tanzania na Shilingi ya Kenya zilikuwa sawa(1TSh=1KSh) iweje leo iwe mara 20?
 
Hela ya Kenya ina thamani kubwa lakini hela ya Tanzania ina nguvu zaidi ya manunuzi

Mfano ukiwa na Elfu moja Tanzania unanunua vitu vingi kuliko ukiwa Kenya

Hivyo basi sisi tupo vizuri zaidi kuliko Kenya
Mfano mzuri ni thamani ya pesa ya china kwa marekani ukija kwenye upande wa mauzo na manunuzi.
 
Kenya wana viwanda vingi na vya uhakika. Wanacheza na import na export, ina maana wanauza kwa wingi nje kuliko kuagiza. Pesa inaimarika kama ukiuza kwa wingi nje bidhaa zenye kiwango.
 
Mimi naona hilo gepu ni la kihistoria,liliathiriwa na vita ya Tz na Uganda, sisi wakati tunakung'uta Waganda wenzetu Kenya walikuwa wanajenga uchumi.Vita vinaisha wakawa wameshatuacha hatua nyingi Sana.
 
Back
Top Bottom