Mizania
JF-Expert Member
- May 17, 2023
- 1,842
- 1,700
Mkuu Deno acha nikuulize jambo, unaweza kuweka ushahidi wa wizi au ufisadi wa J. M. Kikwete hapa hata wa shilingi 50?Utakuwa unafaidi sehemu ya huu ufisadi wa awamu hii ya sita. Mawazo ya kipuuzi kabisa kwako ndio unayapigia vigelegele!.
Unaweza kuweka ushahidi wa mheshimiwa Salma kuwashurutisha, kuwalazimisha au kuwahonga wabunge wote wa CCM kupitisha sheria ya mafao ya wenza?
Mkuu naheshimu mawazo yako na mtazamo wako ila sikubaliani nao. Kwa msingi huo nawe una uhuru wa kutofautiana nami bila kunituhumu kisa tu nipo kinyume na mahaba yako.
Nakusihi usikubali kuambukizwa maradhi ya kuchukia watu bure, huna any basis ya kumchukia JK, unafuata mkumbo, wewe sio wa hivyo Mkuu!
Tuelimishane taratibu, tutofautiane kwa hekima, na turekebishane kwa staha. I always see wisdom in you not otherwise, unless I am wrong!