Ni laana kwa familia ya Mbowe kuwadhurumu waandishi wa habari wanyonge

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,262
9,714
Ndugu zangu Watanzania,

Ogopa sana machozi ya mnyonge yanayotiririka kutoka katika macho yake,ogopa sauti ya kilio cha mnyonge kinacho bubujisha machozi kwa kudhurumiwa haki yake,ogopa na kwepa sana manung'uniko ya mnyonge juu ya haki yake.kwa kuwa huwa machozi yake hayapotei wala kwenda bure, haki yake huwa haipotei bure,jasho lake huwa haliendi bure kwa kuwa jicho la Mungu huwatizama moja kwa moja watu wanyonge na maskini. ukiwazuruma maskini na wanyonge kwa sababu ya jeuri ya pesa zako au cheo chako au umaarufu wako basi juwa mkono wa hasira wa Mungu utakuwa juu yako na kizazi chako chote.

Leo hii kwa sababu ya jeuri ya pesa,umaarufu wa kisiasa pamoja na nafasi ya kiuongozi katika chama familia ya Mbowe imewadhurumu na kuwanyima haki yao waandishi wa habari takribani kumi ,ambao walikuwa wanafanya kazi katika gazeti la Tanzania Daima linalomilikiwa na Familia ya Mbowe Mwenyewe.waandishi hao walivunjiwa mikataba ya kazi pasipo kulipwa stahiki zao ikiwepo kulipwa malimbikizo ya mishahara yao ya kiasi cha shilingi milioni 62 ambapo ni baada ya mazungumzo ya pande mbili ,kwa kuwa awali ilikuwa ni million 114.

Kitendo hiki ni cha uonevu , unyanyasaji, ukandamizwaji, ukatili, unyonyaji,ubabe,mabavu ,jeuri pamoja na dharau kubwa sana. Hivi familia ya Mbowe wanashindwa kushikwa na huruma kweli? Yaani mtu amekufanyia kazi kwa uaminifu na weledi wa hali ya juu unashindwa kumlipa madai yake? Unashindwa kuguswa na maisha ya watu? Unashindwa kutambua kuwa watu hawa wana familia,wana watoto wanaosomesha,wana ndugu wanaowategemea,wana mahitaji wanayohitaji kama binadamu?

Huwezi ukaona huruma kweli mtu anawahi kazini kwako kila siku halafu wewe mwisho wa siku unashindwa kumlipa haki yake anayostahili? Sawa sikatai pengine biashara inaweza ikawa mbaya au mambo yakaenda ndivyo sivyo kibiashara au kampuni ikawa haipati faida au imepata hasara au mauzo yameshuka sana au gharama za uendeshaji zimeongezeka huku faida inayopatikana ni ndogo sana.

Kama jibu ni hilo ,kwanini usikae nao chini au mezani mkazungumza kwa hekima,uwazi na kuwekana sawa kwa kuambiana ukweli juu ya hali halisi ya kibiashara inavyokwenda? Unajuwa sisi sote ni binadamu na hakuna mtu anayeweza kushindwa kuelewa mkikaa chini kirafiki mkaelezana ukweli. hata mimi mwenyewe kuna mahali na wakati unaweza kufanya kazi bila malipo kwa muda fulani na ukawa na amani na morali ya kazi kwa kuwa unatambua hali ya kibiashara na kujuwa sasa hali ni ngumu na hivyo inahitaji kuvumiliana.ukiwaeleza watu na kuwaomba kuvumiliana wakati wa mpito hakuna anayeweza kukataa kukuelewa maana tunaishi kwa kutegemeana na kusaidiana.

Sasa unapovunja mikataba ya watu kibabe,ukashindwa kuwalipa stahiki na haki zao.mkaenda mahakamani wakashinda kesi na ukatakiwa kuwalipa na wewe ukakubali halafu baadaye unaanza ujeuri kwa kuwa tu unajuwa unazo pesa za kutosha kuweka mawakili uwatakao unakuwa hutendi haki.unaweza kushinda kwa janja janja ya kuwazungusha kuwapa haki zao ,lakini huwezi ukashinda mbele ya Mungu atoaye haki kwa haki .

Hivi kweli familia ya Mbowe inashindwa kuwapa na kuwalipa haki zao hao waandishi wa habari wanaodai million 62 ambazo hata mwanaye amekubali kuwa ni sahihi? Hivi Mbowe na familia yake anajenga taswira gani na kupeleka ujumbe gani kwa watanzania wanyonge? Analeta picha ipi? Ni vipi anaweza akawa anahubiri kwa nguvu neno haki katika mdomo wake wakati yeye mwenyewe siyo mtenda haki na amedhurumu jasho la wanyonge? Anaweza vipi wanyooshea kidole wengine watende haki wakati yeye kashindwa kuwa mtenda haki?

Anaweza vipi kusema anauchungu na maisha ya watu wakati ameshindwa kuwapa haki stahili waliotoa jasho lao kumfanyia kazi kama wafanya kazi wake? Kama ameshindwa kutenda haki na kuguswa na maisha ya wafanyakazi wake kumi tu ataweza vipi kuguswa na maisha ya watanzania million 62? Ataweza vipi kuwa na huruma na kuwasikiliza wenye shida? Ataweza vipi wasaidia na wasikiliza wanaodai na kupigania haki ikiwa yeye mwenyewe wapo aliowadhurumu haki zao? Anaweza kupata wapi ujasiri wa kutamka neno HAKI na akaeleweka kwa watu?

Mbowe na familia yako lipeni haki za watu.kuweni na huruma,gusweni na maisha ya watu,siyo vyema kufanya dhuruma,msiitumie nafasi zenu na uwezo wenu wa kifedha kuumiza watu wanyonge.,heshima ni pamoja na kuwatendea watu wote haki ,ni pamoja na kusemewa vizuri na watu wote. Wana familia kama ulivyo nayo wewe.acha kuwatesa na kuwasumbua. Ni laana mbele za Mwenyezi Mungu. usitake kupata laana na hasira ya Mungu ikawa juu yako.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.
 
Tupaze sauti zetu kuwatetea waandishi wa habari wanyonge walipwe pesa zao.tusifumbie macho dhuruma .leo kwako kesho kwangu.ukikaa kimya kwa sababu unaona haikuhusu basi tambua ya kuwa watu watakaa kimya pia yakikukuta.
Si wamefungua case mahakamani? Lakini naunga mkono kuwa Mbowe anapaswa kuonesha mfano kwa kuwatendea haki watu anao taka wampe nchi
 
Laana ipo kwa serikali ya chama chako ambao imewadhulumu haki zao waliokua wafanyakazi wa EAC, wazee wamepigania haki yao na wameishia kufa mmoja baada ya mwingine, na ile pesa haikua ya serikali, serikali ya ccm iliiba na kuzitumia haki zile kulipia madeni ya kagera war, hii ndio dhuluma wewe mtoa mada
 
Tupaze sauti zetu kuwatetea waandishi wa habari wanyonge walipwe pesa zao.tusifumbie macho dhuruma .leo kwako kesho kwangu.ukikaa kimya kwa sababu unaona haikuhusu basi tambua ya kuwa watu watakaa kimya pia yakikukuta.
brother unatia aibu sana; nakukumbusha na ntaendelea kukumbusha yakuwa ccm hawana maana
 
Back
Top Bottom