Mto Songwe
JF-Expert Member
- Jul 17, 2023
- 6,015
- 12,281
Katika suala la maandamano kuna aina mbili maarufu za maandamano.
Moja maandamano ya amani haya pia unaweza kuyaita maandamano ya hisani au matembezi ya hisani .
Ni aina ya maandamano ambayo huhusisha njia za amani katika kukemea, kupongeza, kuunga mkono au kuonesha hisia kuhusu jambo fulani katika jamii.
Mfano wa maandamano haya ni matembezi ya hisani kama siku ya wanawake duniani, kuhimiza kuchangia damu n.k
Pili ni maandamano ya fujo, haya ni maandamano ambayo huusisha matumizi ya nguvu kubwa kwa kundi la watu katika kudai kile wanacho amini, hitaji, kutoa malalamiko au kuonesha hali ya kuto kufurahishwa kuhusu jambo fulani.
Msingi wa maandamano ya namna hii ni katika kushinikiza jambo fulani litekelezwe kutokana na matakwa ya waandamanaji.
Maandamano ya namna hii yametumika sana katika shughuli za kisiasa kuleta mabadiliko ya kiutawala, sheria, muongozo, mifumo n.k katika historia ya tawala mbalimbali hapa duniani.
Utofauti mkubwa uliopo baina ya aina hii ya maandamano ni sehemu za matumizi yake na lengo kusudiwa la waandamanaji.
Katika siasa matembezi ya hisani sio mahala pake sahihi.