Tangawizi
JF-Expert Member
- Jun 25, 2009
- 7,838
- 8,462
Najaribu kufikiri ni sababu gani Chadema wameshindwa kujibu tuhuma za baadhi Wanachama zinazomkabili kiongozi wao Heche badala yake wanatupiana matusi ya kudhalilishana?
Siku zote Tuhuma huwa hazina Ushahidi zinatakiwa kuchunguzwa tofauti na Mashtaka ambayo kisheria huhitaji Ushahidi. Tatizo nini haswa?
Hapo nyuma kidogo tulishuhudia Heche na Tundu Lissu wakiongoza mashambulizi dhidi ya Mbowe kwa tuhuma kama hizi, kuaminisha Wanachama wa Chadema kwamba Kiongozi wao Mwenyekiti Mbowe alilamba asali, Mbowe alifisadi chama ilihali Mbowe sii mhasibu wala mweka fedha za Chama kama wanavyomtea Heche leo hii.
Chadema wameshindwa kukabiliana na tuhuma hizi badala yake wanachukua mkondo ule ule ambao miaka yote wamekuwa wakiwatuhumu viongozi wa CCM kwa Ufisadi ambao Viongozi wa CVM pia waliendelea kudai hakuna Ushahidi.
Je, tumefikia pahala kila sauti inayokemea Ufisadi na Ubadhilifu lazima mtia tuhuma awe Ushahidi?
b
Kama wao hawana shida pesa zao zikiliwa, wengine mnasumbukia nini?
Si wapo wanaosema awepe account yake personal ili wamchangie ili iwaume zaidi?
Namna hii ya kutengeneza fitna kama ndio njia sahihi ya siasa imepitwa na wakati.
Tena wakati huu ambao wasiompenda wanamjua, wahangaike na CDM ili iweje?