Kwanini CHADEMA wameshindwa kumchunguza Heche?

NB: Stop exposing your hypocrisy and let them be kwani chama ni chao na malengo, mikakati, direction na goals wamejipangia wenyewe
Mleta mada hatofautiani sana na TlaaTlaah, inapokuja kwenye maelezo kwa nini anajitoa akili zote kupigania hicho wanacxhokipigania chini ya Samia Suluhu Hassan.

Akili zote wanaziweka pembeni na kujisalimisha kwa hicho wanachokipigania chini ya Samia.
 
Nimeuliza swali halijajibiwa mpaka sasa, nasoma michango mingi ipo upande wa kutetea lakini mnaruka HOJA yangu. Narudia mara ya tatu (3)
Taarifa zilitoka na.kusambaa kuwa Lema, Sugu na Boniface ndio walohoji swala la Heche katika Mkutano wa Kamati kuu ya Chama Kigoma. Je, Kweli au Uongo?

Kisha nilisema mwanzoni Ufisadi wa Samia unatuhumiwa na watu wa Chadema.na Wanaharakati kweli sii kweli?, hivi mnataka kunambia nikubaliane na Viongozi wa CCM wanaosema hizo tuhuma hazina Ukweli kwa sababu zinatolewa na Chadema na Wanaharakati?

Katika Kisiasa kote duniani, tuhuma zote za kisiasa hutoka upande wa pili hazitoki ndani ya Chama. Aghalabu kusikia mtu wa ndani ya chama akimshutumu kiongozi wake, nimeshuhudia hili Chadema mwaka jana akishutumiwa Mbowe! Leo kwa Heche mnataka itokee vivyo hivyo ndio muamini.

Hata huko nje, Kiongozi anapofuja fedha za Umma, tuhuma hutoka upande wa Upinzani na ndio haswa sababu mojawapo ya kuwa na Vyama vingi. Kuna macho yanakutazama kila kona na kila upande.

Kinachotakiwa ni majibu sio kukaa kimya ati tuhuma zimeletwa na Ma CCM. Kwani Samia na Abdul wanatuhumiwa na Wanachama wa.CCM? Mauaji ya Oktober 29 mnataka atokee mtu wa CCM kulaani ndio iwe kweli? Haiwezekani watalindana tu, Na Chadema inaonekana ni Udaku! Sasa Ukweli utatoka wapi? What's wrong with you my people!

Na kwa.jinsi mnavyotetea hili swala mimi naona kama mnamtetea Heche kama CCM wanavyomtetea Samia na Mwigulu Mchemba bila majibu ya tuhuma tunazosikia. Mind you - Uongo ukisemwa sana hugeuka Ukweli.

Anyway, mimi nachosema, Chadema wanalamizika kulishughulikia swala hili mapema laa sivyo, mtapoteza Umaarufu wenu Kitaifa. Lema alisema maneno fulani mazito sana! Nataka atokee mtu wa Chadema amjibu Lema.
 
..Nadhani alitaka kusema yeyote anayetaka kumchangia ktk harakati za kisiasa apeleke mchango kwa chama na sio kwake.

..Ni vizuri Watanzania tukajenga utamaduni wa kuchangia taasisi / chama na sio viongozi. Pia ni vizuri kuwa na loyalty kwa chama na sio mtu, au kiongozi.
Haya maswala ya "kuchangia" ni muhimu sana yawekewe tahadhari kubwa ndani ya chama.

Michango ya kawaida ya wananchi si tatizo, tatizo linaanza wakati baadhi ya matajiri wanajiandaa kwa kuwekeza kwa matarajio ya kesho na kesho kutwa kupata ziada kwa uwekezaji wao; hasa hiyo ziada ikiwa inatokana na njia zisizokuwa halali.

Tajiri mkubwa anamchangia kiongozi wa chama kwa matarajio ya kupata upendeleo huko mbele ya safari, hili linapashwa kuangaliwa kwa makini sana wakati huu.
Viongozi wa CHADEMA wawe waangalifu wasijiweke kwenye nafasi ya namna hiyo wakati huu.
 
Anyway, mimi nachosema, Chadema wanalamizika kulishughulikia swala hili mapema laa sivyo, mtapoteza Umaarufu wenu Kitaifa. Lema alisema maneno fulani mazito sana! Nataka atokee mtu wa Chadema amjibu Lema.
Hili la kupoteza umaarufu lisikupe taabu sana. Subiri tiu uone watakavyopata taabu bila ya wewe na wengineo kuchochea moto kwa sababu zilizo wazi kabisa.

Waacheni CHADEMA wayamalize wenyewe, huko huko ndani ya chama chao. kama kuna mamluki mliowawekea matumaini kukivuruga chama, waacheni wapambane huko huko ndani ya chama; msiwaingizie sumu zenu toka huku nje.

Ni aibu kwa mtu kama wewe kulinganisha shutuma zinazoelekezwa kwa Samia na wenzake kwa uchafu unaofanywa siyo ndani ya chama chao tu, bali kwa taifa zima; halafu ulinganishe na mnayowafanyia CHADEMA, eti ni shutuma tu; huku lengo likiwa ni kukisambaratisha chama.

Huna nia njema katika hayo maswali unayouliza.
 
Nimeuliza swali halijajibiwa mpaka sasa, nasoma michango mingi ipo upande wa kutetea lakini mnaruka HOJA yangu. Narudia mara ya tatu (3)
Taarifa zilitoka na.kusambaa kuwa Lema, Sugu na Boniface ndio walohoji swala la Heche katika Mkutano wa Kamati kuu ya Chama Kigoma. Je, Kweli au Uongo?

Kisha nilisema mwanzoni Ufisadi wa Samia unatuhumiwa na watu wa Chadema.na Wanaharakati kweli sii kweli?, hivi mnataka kunambia nikubaliane na Viongozi wa CCM wanaosema hizo tuhuma hazina Ukweli kwa sababu zinatolewa na Chadema na Wanaharakati?

Katika Kisiasa kote duniani, tuhuma zote za kisiasa hutoka upande wa pili hazitoki ndani ya Chama. Aghalabu kusikia mtu wa ndani ya chama akimshutumu kiongozi wake, nimeshuhudia hili Chadema mwaka jana akishutumiwa Mbowe! Leo kwa Heche mnataka itokee vivyo hivyo ndio muamini.

Hata huko nje, Kiongozi anapofuja fedha za Umma, tuhuma hutoka upande wa Upinzani na ndio haswa sababu mojawapo ya kuwa na Vyama vingi. Kuna macho yanakutazama kila.kona na kila upande.

Kinachotakiwa ni majibu sio kukaa kimya ati tuhumanzimeletwa na Ma CCM. Kwani Samia na Abdul wanatuhumiwa na Wanachama wa.CCM? Mauaji ya Oktober 29 mnataka atokee mtu wa CCM kulaani ndio iwe kweli? Haiwezekani watalindana tu, NaChadema inaonekana ni Udaku! Sasa Ukweli utatoka wapi? What's wrong with you my people!

Na kwa.jinsi mnavyotetea hili swala mimi naona kama mnamtetea Heche kama CCM wanavyomtetea Samia na Mwigulu Mchemba bila majibu ya tuhuma tunazosikia. Mind you - Uongo ukisema.sana hugeuka Ukweli.

Tofautisha kati ya matumizi ya michango ya chama, hata CCM wanavyopokea mabilioni kutoka kwa wafanyabiashara hakuwi mjadala lakini linapokuja suala la pesa za walipa kodi na rasilimali za nchi ndipo kunapokuwa na ulazima wa accountability, transparency and answerability.
 
Najaribu kufikiri ni sababu gani Chadema wameshindwa kujibu tuhuma za baadhi Wanachama zinazomkabili kiongozi wao Heche badala yake wanatupiana matusi ya kudhalilishana?

Siku zote Tuhuma huwa hazina Ushahidi zinatakiwa kuchunguzwa tofauti na Mashtaka ambayo kisheria huhitaji Ushahidi. Tatizo nini haswa?

Hapo nyuma kidogo tulishuhudia Heche na Tundu Lissu wakiongoza mashambulizi dhidi ya Mbowe kwa tuhuma kama hizi, kuaminisha Wanachama wa Chadema kwamba Kiongozi wao Mwenyekiti Mbowe alilamba asali, Mbowe alifisadi chama ilihali Mbowe sii mhasibu wala mweka fedha za Chama kama wanavyomtea Heche leo hii.

Chadema wameshindwa kukabiliana na tuhuma hizi badala yake wanachukua mkondo ule ule ambao miaka yote wamekuwa wakiwatuhumu viongozi wa CCM kwa Ufisadi ambao Viongozi wa CVM pia waliendelea kudai hakuna Ushahidi.

Je, tumefikia pahala kila sauti inayokemea Ufisadi na Ubadhilifu lazima mtia tuhuma awe Ushahidi?

b
Tuchunguze vipi jembe letu hili la nguvu!? Zaidi tunahitaji kumpa nguvu ya kutupigania sisi wananchi tuliotawaliwa na mkoloni mweusi.
 
Hili la kupoteza umaarufu lisikupe taabu sana. Subiri tiu uone watakavyopata taabu bila ya wewe na wengineo kuchochea moto kwa sababu zilizo wazi kabisa.

Waacheni CHADEMA wayamalize wenyewe, huko huko ndani ya chama chao. kama kuna mamluki mliowawekea matumaini kukivuruga chama, waacheni wapambane huko huko ndani ya chama; msiwaingizie sumu zenu toka huku nje.

Ni aibu kwa mtu kama wewe kulinganisha shutuma zinazoelekezwa kwa Samia na wenzake kwa uchafu unaofanywa siyo ndani ya chama chao tu, bali kwa taifa zima; halafu ulinganishe na mnayowafanyia CHADEMA, eti ni shutuma tu; huku lengo likiwa ni kukisambaratisha chama.

Huna nia njema katika hayo maswali unayouliza.
Nasema hivi, hakuna kiwango cha Ufosadi katika Ufisadi. Jizi ni jizi tu, tapeli tapeli tu, haijalishi kaiba wapi au kamtapeli nani? Leo kwangu kesho kwako! Kataa wahuni...

Kama Heche amefanya aloyafanya ndani ya Chama, tukamkingia kifua basi ni sawa na Mama anayemlea mwanae muuza ngada kwa sababu kamjengea nyumba! Akili hii mimi sina..Maadam wewe ni Kiongozi wa watu, Ukiharibu nakuwasha haijalishi wee nani. Kumkoma nyani giledi eeeh!

Kama hoja ni U - Chadema, nilitegemea wewe ungenielewa vizuri zaidi tuliko toka kuliko wengine humu. Na kama umesahau mtafute Mwanakijiji au Rev. Kishoka watakukumbusha..
 
Taarifa zilitoka na.kusambaa kuwa Lema, Sugu na Boniface ndio walohoji swala la Heche katika Mkutano wa Kamati kuu ya Chama Kigoma. Je, Kweli au Uongo?
Binafsi sijui na sifanyii kazi habari za kusikika hadi wahusika au viongozi wao watakapo thibitisha
Swali kwako, je, una ushahidi hilo lilitokea? Unaweza kuthibitisha?
Kisha nilisema mwanzoni Ufisadi wa Samia unatuhumiwa na watu wa Chadema.na Wanaharakati kweli sii kweli?, hivi mnataka kunambia nikubaliane na Viongozi wa CCM wanaosema hizo tuhuma hazina Ukweli kwa sababu zinatolewa na Chadema na Wanaharakati?
Hao wanaharakati tuliwataka watoe ushahidi. Kuna ushahidi uliwekwa hadi kupelekea watu kusema ''kuna matumizi mabaya' ya fedha za Umma.

Majuzi CAG alithibitisha Waziri kijana kuwa na pesa za kutisha. Ndio maana tunasema ushahidi wa pesa kuliwa CHADEMA upo wapi? Tofautisha kati ya kutaka ushahidi na kukataa uwepo wake ni mambo tofauti

Pili, Je, anayepaswa kuchunguzwa ni aliyetumia au aliyeidhinisha? Kwanini Heche na si Katibu mkuu.
Mnyika kasema yeye ndiye mwenye dhamana! kwanini isiwe yeye kuchunguzwa bali '' anayekula''
Katika Kisiasa kote duniani, tuhuma zote za kisiasa hutoka upande wa pili hazitoki ndani ya Chama.
Ni kweli ! kuna watu wa CCM wanaweza kuongea ukafikiria. Hivi Selasini, Mchome, Lucas n.k. nao ni wa kusikilizwa?

Mfano, Pole pole alipokuwa anaongea alikuwa anatoa hadi ushahidi. Wote walio ongea CHADEMA wametoa press na kutokemea! hakuna anayeleta ushahidi.

Selasini unayemwamini kasema '' Heche achunguzwe ili CHADEMA iingie katika maridhiano'' Think about that!

Viongozi wengine wanasema ni tone tone! Selasini anasema maridhiano.

Odero anasema Heche hafai katika maridhiano na upuuzi kama huo. Hawa wana credibility gani ya kuaminiwa?
Hata huko nje, Kiongozi anapofuja fedha za Umma, tuhuma hutoka upande wa Upinzani na ndio haswa sababu mojawapo ya kuwa na Vyama vingi. Kuna macho yanakutazama kila.kona na kila upande.
Ushahidi upo wapi? Katika wote walio ongea tupe mmoja tualiyetoa hata ushahidi wa mashaka
Kinachotakiwa ni majibu sio kukaa kimya ati tuhumanzimeletwa na Ma CCM. Kwani Samia na Abdul wanatuhumiwa na Wanachama wa.CCM? Mauaji ya Oktober 29 mnataka atokee mtu wa CCM kulaani ndio iwe kweli? Haiwezekani watalindana tu, NaChadema inaonekana ni Udaku! Sasa Ukweli utatoka wapi? What's wrong with you my people!
What's wrong with you ! October 29 watu wameuawa. Huo ni ushahidi si tuhuma. Tume waliyounda imesema maiti 30 zimepotea! huo ni ushahidi si tuhuma. Kuna watoto wamepigwa risasi zipo picha na tume imesema hivyo. Huo ni ushahidi si tuhuma. Ni tofauti na Katibu wa CHADEMA Kilindi kusema pesa zimeliwa bila kueleza wapi na nani. Tena anasema Heche achunguzwe bila kusema kwa taratibu zipi kikatiba akiwa makamu na si Katibu mkuu

Majibu kayatoa Katibu mkuu Mnyika1 Kwamba ni yeye anayetunza pesa. Kinachotakiwa ni ku prove Mnyika anasema uongo kwa ushahidi na uchunguzi uanzie kwake ili kubaini wahusika. Hilo halifanyiki tunasikia Heche!
Na kwa.jinsi mnavyotetea hili swala mimi naona kama mnamtetea Heche kama CCM wanavyomtetea Samia na Mwigulu Mchemba bila majibu ya tuhuma tunazosikia. Mind you - Uongo ukisema.sana hugeuka Ukweli.
Noo! hatumetetei Heche, tunatetea ukweli. Kwamba, Mtendaji wa Chama ni KM . Kwanini haulizwi anaulizwa Makamu? Pili, kwanini CCM wameshikia bango hili suala kuliko madhila yanayoendelea nchini.

Ipo wapi moral authority ya CCM kukemea ulaji wa pesa tukijua mengi yao yaisyoandikika hapa.

Hivi watu wanaoidhinisha Trilioni moja kununua maandazi, vitumbua, makaimati na visheti Hawa wana moral compass gani ya kukueleza uhalifu
Anyway, mimi nachosema, Chadema wanalamizika kulishughulikia swala hili mapema laa sivyo, mtapoteza Umaarufu wenu Kitaifa. Lema alisema maneno fulani mazito sana! Nataka atokee mtu wa Chadema amjibu Lema.
Upo sahihi walishughulikie kwa taratibu si kwa shinikizo la Selasini aliyeua NCCR kwa kushirikiana na Msajili

Si kwa shinikizo la Msigwa anayeombea mabaya CHADEMA kila siku. Sikwa shinikizo la Lembrus Mchome.
Si kwa shinikizo la watu wanaohongwa ambao video za zipo mitandaoni.

Tuliruhusu uhuni CUF ikafa. Tukachekea uhuni NCCR ikafa , hatujifunzi tu.

Mkandara ukweli ni kwamba CCM wanamtaka ''MBOWE'' wa kukaa naye meza moja mieizi 6 kama ilivyokuwa.

Heche na Lissu ni miiba mikali kwao, watafanya kila liwezekanalo. Watu wametoa pesa kuunda CHAUMMA ili washinde uchaaguzi litawashinda la kuua CHADEMA.
 
Umeniuliza Ushahidi katika tuhuma za Heche, nakujibu hivi Muulize Lema, Sugu au Boniface ukweli utaujua. Achana na hao kina Habib Mchange sijii kina mapandikizi, nenda kwenye Source. Somebody gut to raise up!

Isitoshe sidhani hata wewe una Ushahidi kuhusu Mbowe. CCM inamtaka mtu yeyote mwanasiasa kama ilivyo Chadema na vyama vingine vyote hata wewe Ukitaka kesho watakupa kadi yao.

Kama Chadema iliweza mchukua Lowassa na Sumaye ambao wote waliwahi kuwa Mawaziri Wakuu wa nchi cha kushangaza nini?
 
Najaribu kufikiri ni sababu gani Chadema wameshindwa kujibu tuhuma za baadhi Wanachama zinazomkabili kiongozi wao Heche badala yake wanatupiana matusi ya kudhalilishana?

Siku zote Tuhuma huwa hazina Ushahidi zinatakiwa kuchunguzwa tofauti na Mashtaka ambayo kisheria huhitaji Ushahidi. Tatizo nini haswa?

Hapo nyuma kidogo tulishuhudia Heche na Tundu Lissu wakiongoza mashambulizi dhidi ya Mbowe kwa tuhuma kama hizi, kuaminisha Wanachama wa Chadema kwamba Kiongozi wao Mwenyekiti Mbowe alilamba asali, Mbowe alifisadi chama ilihali Mbowe sii mhasibu wala mweka fedha za Chama kama wanavyomtea Heche leo hii.

Chadema wameshindwa kukabiliana na tuhuma hizi badala yake wanachukua mkondo ule ule ambao miaka yote wamekuwa wakiwatuhumu viongozi wa CCM kwa Ufisadi ambao Viongozi wa CVM pia waliendelea kudai hakuna Ushahidi.

Je, tumefikia pahala kila sauti inayokemea Ufisadi na Ubadhilifu lazima mtia tuhuma awe Ushahidi?

b
Huwezi kuchunguza kitu hakipo
 
Ni kama tumekatwa vichwa CAG anatoa taarifa za ujambazi kila mwaka tupo kimya harafu tujadili pesa za michango ya watu kama ya Haruhi au msiba...
 
Umeniuliza Ushahidi katika tuhuma za Heche, nakujibu hivi Muulize Lema, Sugu au Boniface ukweli utaujua. Achana na hao kina Habib Mchange sijii kina mapandikizi, nenda kwenye Source. Somebody gut to raise up!
Swali ni kwamba una uhakika na ushahidi kwamba Lema, Sugu na Boni walisema hayo?
Tunachotaka ni proof siyo kwenda na habari za kusikia.

Mnyika kasema yeye ndiye anatunza pesa na zipo salama. Iwe kweli au uongo tumesikia kutoka kinywa chake
Habibu Mchange akisema Lema, Boni na Sugu walisema, huo si ukweli achilia mbali credibility yake.

Hata kama walisema, je, walitoa ushahidi? na nani wa kutuhumiwa Katibu mkuu au Heche?
Kwanini wanasema HECHE na si Makamu Mwenyekiti.
Isitoshe sidhani hata wewe una Ushahidi kuhusu Mbowe. CCM inamtaka mtu yeyote mwanasiasa kama ilivyo Chadema na vyama vingine vyote hata wewe Ukitaka kesho watakupa kadi yao.
Ushihidi wa MBOWE upo. Walimtoa magereza wakamkimbiza Ikulu. Kutokea hapo Mbowe akabadilika. Walikaa na Mbowe mwaka wakizungumza mwisho wa siku zero

Mbowe alisema kwa ushahidi kwamba kuna wenzetu walishiriki kuharibu maridhiano! Ushahidi kwamba yeye na CCM walikuwa na mitazamo sawa.

Mkandara, MBOWE alifanya madudu sana! hilo linahitaji ushahidi kweli. Ndiye wanamtaka au photocopy yake
Kama Chadema iliweza mchukua Lowassa na Sumaye ambao wote waliwahi kuwa Mawaziri Wakuu wa nchi cha kushangaza nini?
Ni kweli, na bahati nzuri sisi wengine tulikemea hilo kwa msingi ule ule kwamba EL alikuwa fisadi kwa ushahidi
 
Najaribu kufikiri ni sababu gani Chadema wameshindwa kujibu tuhuma za baadhi Wanachama zinazomkabili kiongozi wao Heche badala yake wanatupiana matusi ya kudhalilishana?

Siku zote Tuhuma huwa hazina Ushahidi zinatakiwa kuchunguzwa tofauti na Mashtaka ambayo kisheria huhitaji Ushahidi. Tatizo nini haswa?

Hapo nyuma kidogo tulishuhudia Heche na Tundu Lissu wakiongoza mashambulizi dhidi ya Mbowe kwa tuhuma kama hizi, kuaminisha Wanachama wa Chadema kwamba Kiongozi wao Mwenyekiti Mbowe alilamba asali, Mbowe alifisadi chama ilihali Mbowe sii mhasibu wala mweka fedha za Chama kama wanavyomtea Heche leo hii.

Chadema wameshindwa kukabiliana na tuhuma hizi badala yake wanachukua mkondo ule ule ambao miaka yote wamekuwa wakiwatuhumu viongozi wa CCM kwa Ufisadi ambao Viongozi wa CVM pia waliendelea kudai hakuna Ushahidi.

Je, tumefikia pahala kila sauti inayokemea Ufisadi na Ubadhilifu lazima mtia tuhuma awe Ushahidi?

Ccm kwa Heche au lissu mtacheza mdundiko sana, hawa watu wamejaa nyoyoni kwa watz , leo hata wakitaka changiwa Bil moja ni faster, so kitendo cha kumuanda ati amekula pesa ,inahusu nini ili hali watz wanasema kama kula acha ale watachanga zingine, hata haibu hamuoni.

Musiba alisha waonya maccm wenzake juu ya vyuma hivi , namna pekee ya ccm kwenda sawa na chadema sasa akili wala sio abavu.

Fanyia kazi madai yao ili wakose hoja
Mfano
Mwachie mwenyekiti wao na viongozi wao mbalimbali mnaowabambikia kesi za ugaidi
2.mchakato wa katiba urudi mezani kupitia rasmu ya Warioba.
3 .uwajibikaji kwa wahusika wote Mo2025

Hizi ndo akili zinatakiwa kufanyika sio kukaa fikiria ati tukibambikia watu kesi, tukateka, tukapoteza, basi tumemaliza ,matokeo watu sasa kila mmoja anaanza kujiona ni mfungwa mtarajiwa wa ugaidi , kupotezwa n.k , hii ni mbaya sasa watu wanaanza kufikia ile hali ya liwalo na liwe, that pamoja na kuteka wanaibuka wengine kibao.

Achaneni na akili za wakina Wasira ati kisa amekaa serikalini sana, je enzi zile na sasa ni sawa, impact yake miaka yote katika taifa ni ipi ,
 
Nakubaliana na wewe kabisa kuhusu shaka juu ya watoa tuhuma. Ila kuna clip moja Heche alitoka akasema anaomba Wanachama wasimchangie, michango yote kuanzia sasa iende Chadema.
Alikuwa na maana gani?
Mkuu,
Heche hakusema hivyo.
Alisema kuna watu wanataka kumchangia yeye. Anawaomba hiyo Michango wachangie chama.
Hilo la wasimchangie Michango yoyote kuanzia sasa ni la kwako umechomekea tu.
 
Nimeuliza swali halijajibiwa mpaka sasa, nasoma michango mingi ipo upande wa kutetea lakini mnaruka HOJA yangu. Narudia mara ya tatu (3)
Taarifa zilitoka na.kusambaa kuwa Lema, Sugu na Boniface ndio walohoji swala la Heche katika Mkutano wa Kamati kuu ya Chama Kigoma. Je, Kweli au Uongo?

Kisha nilisema mwanzoni Ufisadi wa Samia unatuhumiwa na watu wa Chadema.na Wanaharakati kweli sii kweli?, hivi mnataka kunambia nikubaliane na Viongozi wa CCM wanaosema hizo tuhuma hazina Ukweli kwa sababu zinatolewa na Chadema na Wanaharakati?

Katika Kisiasa kote duniani, tuhuma zote za kisiasa hutoka upande wa pili hazitoki ndani ya Chama. Aghalabu kusikia mtu wa ndani ya chama akimshutumu kiongozi wake, nimeshuhudia hili Chadema mwaka jana akishutumiwa Mbowe! Leo kwa Heche mnataka itokee vivyo hivyo ndio muamini.

Hata huko nje, Kiongozi anapofuja fedha za Umma, tuhuma hutoka upande wa Upinzani na ndio haswa sababu mojawapo ya kuwa na Vyama vingi. Kuna macho yanakutazama kila.kona na kila upande.

Kinachotakiwa ni majibu sio kukaa kimya ati tuhumanzimeletwa na Ma CCM. Kwani Samia na Abdul wanatuhumiwa na Wanachama wa.CCM? Mauaji ya Oktober 29 mnataka atokee mtu wa CCM kulaani ndio iwe kweli? Haiwezekani watalindana tu, NaChadema inaonekana ni Udaku! Sasa Ukweli utatoka wapi? What's wrong with you my people!

Na kwa.jinsi mnavyotetea hili swala mimi naona kama mnamtetea Heche kama CCM wanavyomtetea Samia na Mwigulu Mchemba bila majibu ya tuhuma tunazosikia. Mind you - Uongo ukisema.sana hugeuka Ukweli.

Anyway, mimi nachosema, Chadema wanalamizika kulishughulikia swala hili mapema laa sivyo, mtapoteza Umaarufu wenu Kitaifa. Lema alisema maneno fulani mazito sana! Nataka atokee mtu wa Chadema amjibu Lema.
Hao Lema ma wenzake unaowasemea hawajasema hicho.
Lema Alisema taarifa sahihi ya kikao cha Kamati kuu itatolewa na Katibu Mkuu.

Katibu Mkuu Katia maazimio yote ya Kamati kuu. Hilo mnalo likazia misuli halimo na Lema kaunga mkono maazimio ya Kamati kuu.

Sasa hapo mnataka nini? Nyie mnataka kuamini hearsays?
 
Swali ni kwamba una uhakika na ushahidi kwamba Lema, Sugu na Boni walisema hayo?
Tunachotaka ni proof siyo kwenda na habari za kusikia.
Seriously? Unataka sasa mpaka usikie recording ya Lema, Sugu na Boni ndio uamini? Au unataka minutes za kikao husika? Wewe hauoni kukaa kimya kwao kunatia wasiwasi? Na sio wao tu, hakuna hata kiongozi mmoja aliyekuwepo anayekanusha tukio hilo.
Mnyika kasema yeye ndiye anatunza pesa na zipo salama. Iwe kweli au uongo tumesikia kutoka kinywa chake
Habibu Mchange akisema Lema, Boni na Sugu walisema, huo si ukweli achilia mbali credibility yake.
Shutuma sio pesa zilizokuwa kwenye akaunti za Chadema zimeliwa. Shutuma ni kuwa Heche amekuwa hafikishi pesa anazopewa kwa ajili ya Chadema. Shutuma ni kuwa anaziingiza kwenye akaunti yake binafsi. Katika hali hiyo Mnyika anahusika vipi? Au KM anasimamia pia akaunti binafsi ya Heche?

Kinacho shangaza ni kuwa ili kujibu tuhuma hizi ametokeza mfanya biashara mmoja na kusema kuwa ana uhusiano wa kibiashara na Heche na pesa anazompa sio kwa ajili ya matumizi ya Chadema. Amesema pia kuwa huwa anachangia pia CCM. Hili nalo lina shida ethically kwa Heche kama hakuwaambia wenzake kuhusu mahusiano na huyo mfanyabiashara. Aidha, linatia wasiwasi kuwa huyo mfanyabiashara atakuwa na leverage juu yake pale chama chake kitakapo shika dola.
Hata kama walisema, je, walitoa ushahidi? na nani wa kutuhumiwa Katibu mkuu au Heche?
Kwanini wanasema HECHE na si Makamu Mwenyekiti.
Toa mfano wa hicho unachoita kuwa ni ushahidi.

Kwa nini Mnyika ahusishwe wakati katika maelezo yao Katibu Mkuu hakuhusika?

Inawezekana wanasema Heche kwa sababu tuhuma ni kuwa alizihujumu kama Heche na sio kama Mwenyekiti. Wanadai michango hiyo iliingizwa kwenye akaunti ya Heche na sio ya Makamu Mwenyekiti wa Chadema.
Ushihidi wa MBOWE upo. Walimtoa magereza wakamkimbiza Ikulu. Kutokea hapo Mbowe akabadilika. Walikaa na Mbowe mwaka wakizungumza mwisho wa siku zero
I am sorry, but this is pure nonsence. Hakuna ushahidi kuwa Mbowe alipelekwa Ikulu. Mbowe ana usafiri wake na anasema kuwa alialikwa na Rais kwenda Ikulu hivyo akaenda. Hajawahi kuficha kuwa alienda. Amesema pia kuwa aliwapa viongozi wenzake taarifa ya mazungumzo hayo. Hakuna kiongozi aliyesema kuwa hakupata taarifa.

Mbowe hajawahi kuficha kuwa anapendelea zaidi dialogue kuliko confrontation. Hata wakati wa JPM alienda Mwanza kuomba wazungumze. Hapo kosa liko wapi? Mandela aliongea na De Klerk. Martin Luther King Junior aliongea na Lyndon Johnson. Hamas wameongea na Israel wakati watu wao wanafanyiwa unyama. Iran inaongea na USA. Zelensky anataka mazungumzo na Putin. Wote hawa ni wasaliti?

Mmoja wa waliofaidika na hayo mazungumzo ni Lissu. Aidha, mamia ya wafuasi wa Chadema waliondolewa magerezani na kesi zao kufutwa kutokana na hayo mazungumzo. Zuio la mikutano ya hadhara liliondolewa na Chadema walitumia fursa hiyo kikamilifu kwa kufanya mikutano ya hadhara mingi ambayo baadhi ilihutubiwa na Lissu na wenzie.

Mbowe aliendelea kuita maandamano hata pale ambapo hao mashujaa wenu walijificha. Na CCM waliposema kuwa anawachuuza watoto wa wengine, aliongozana na binti yake. Nakumbuka picha ya Hilda akiwa amejificha ili askari wasimuone.

Lissu aliposhambuliwa Mbeya, Mbowe alikimbilia kwenda kusimama nae ingawa alijua thika kuwa angeweza kukamatwa. Na kweli alikamatwa. Mbowe alichangia zaidi ya milioni 200 ili kuwezesha Mkutano Mkuu wa Chama. Lissu alisema yeye sio tajiri hivyo hawezi kuchangia.

Pamoja na kambi ya Lissu kudai kuwa hujuma zitafanyika katika uchaguzi huo, uchaguzi uliendeshwa kwa uwazi ambao ni nadra katika chaguzi tulizo zoea. Na Mbowe aliposhindwa alikubali na kumpongeza Lissu. Katika yote haya huo ushahidi wa kununuliwa na Samia uko wapi? Ni fitna tu.
Mbowe alisema kwa ushahidi kwamba kuna wenzetu walishiriki kuharibu maridhiano! Ushahidi kwamba yeye na CCM walikuwa na mitazamo sawa.
Kwani ni uongo? Kuna ubaya gani katika kutaka mazungumzo na mpinzani wako? Sio upande wa Chadema peke yake ndio kulikuwa na wasiotaka maridhiano, Kinana nae alisema wazi kuwa CCM nako kuna waliokuwa wanapinga mazungumxo hayo. Aidha, hakuna mtu anayeingia katika mazungumzo anaingia ili yashindwe. Lakini akiona mwenzie hana nia njema, anajitoa. Na ndivyo alivyofanya Mbowe. Ni ishara ya maturity.
Mkandara, MBOWE alifanya madudu sana! hilo linahitaji ushahidi kweli.
Hakuna kiongozi asiyefanya madudu. Ni sehemu ya uongozi. Kiongozi anapimwa kwa ujumla wa matendo yake. Ku cherry pick makosa sio kumtendea haki.
Ndiye wanamtaka au photocopy yake
CCM hawajawahi kumtaka Mbowe. Machawa wa CCM walimpigia kampeni za wazi ili Chadema wahisi amenunuliwa na hivyo waamue kumpigia kura mshindani wake. CCM walimtaka Lissu kwa sababu walijua atawapa fursa ya kukibana Chadema na kukitoa kwenye uchaguzi. Na kweli walifanikiwa. Na walijua kuwa pamoja na kelele zao kambi ya Lissu hawana ujasiri wa Mbowe. Mbowe aliita maandamano dhidi ya utawala pamoja na dola kuyakataza. Alifanya mikutano, pamoja na watu wake kuzuiwa na wakati mwingine. Mbowe na wenzake walifanya creative civic disobedience. Wakina Husna walikataa kushusha bendera ya chama chao Chato. Wakina Mwakipesile na wenzake walijigala gala nje ya ubalozi wa Marekani. Mwakipesile alikaa ndani lakini alikataa kuwataja wenzake. Wakina Ruge, Halima na wengine wengi walikaa sana rumande. Sugu alifungwa. Mbowe na wenzake nao walifungwa. Heche alipotoka alisema Mbowe alikataa kutoka jela mpaka wenzake wote wametoka. Tuambie Chadema ya Lissu imeandaa maandamano mangapi?

Yote hayo mnataka kutuaminisha kuwa CCM walimtaka Mbowe kuliko hao wa sasa ambao wanangoja wapewe kibali ili waandamane na kufanya mikutano ya hadhara! CCM wana mmwagia masifa Mbowe ili asikubalike ndani ya Chadema.

Na kwa kiasi fulani wamefanikiwa maana kuna blind hatred dhidi ya Mbowe kiasi ya watu kukataa kuona ushahidi ulio machoni mwao. CCM wanatazama 2030, na watahakikisha kuwa ifikapo hapo Chadema inakuwa kibogoyo. Unfortunately, watu kama nyie mna wa facilitate kufikia kwenye adhma hiyo.
Ni kweli, na bahati nzuri sisi wengine tulikemea hilo kwa msingi ule ule kwamba EL alikuwa fisadi kwa ushahidi
Hapo ndipo Mbowe alionyesha pragmatism. EL alichangia Chadema kupata wageni wengi. Kura alizopata ziliwapa wabunge wa viti maalum wengi na ruzuku ambayo iliwawezesha kukijenga chama chao. Ile ruzuku na uwepo wa wabunge wao ndio ulionyesha watanzania kuwa kuna alternative to CCM. Ujasiri wao chini ya Mbowe wa kukataa kunyamazishwa ndio umefikisha Chadema hapa ilipo. Viongozi wengi wa Chadema wanakiri kuwa Mbowe ana mchango mkubwa katika uwepo wao kwenye siasa.

Chadema ya Mbowe ilikuwa na wigo kubwa la viongozi mahiri na jasiri kiasi kuwa hata alipokuwa ndani chama chake kiliendelea kuisumbua CCM. Bawacha, Bavicha na Bazecha wote walishiriki kikamilifu na walipewa nafasi za kung'ara chini ya Mbowe. Yote haya yaliwezeshwa kwa kiasi kikubwa na master stroke ya kumtumia Lowassa. Hivi ukimuondoa Heche ni kiongozi gani wa sasa wa Chadema anaweza kuumudu u makamu Mwenyekiti? Sugu? Boni Yai?

Ninachoshangaa ni kuwa hamuonyeshi outrage kwa chama kumkumbatia kiongozi wao ambae aliandika kitabu kukihusisha kilichokuwa chama chake na utekaji na utesaji wa wanachama wake.

Hamuonyeshi outrage kwa kumpokea kiongozi ambae alihamia upande wa pili na kukichafua sana chama chake akiwa amevaa kijani na amebeba picha ya Mwenyekiti wa CCM.

Huu ni unafik mtupu.

Amandla....
 
Swali ni kwamba una uhakika na ushahidi kwamba Lema, Sugu na Boni walisema hayo?
Tunachotaka ni proof siyo kwenda na habari za kusikia.

Mnyika kasema yeye ndiye anatunza pesa na zipo salama. Iwe kweli au uongo tumesikia kutoka kinywa chake
Habibu Mchange akisema Lema, Boni na Sugu walisema, huo si ukweli achilia mbali credibility yake.

Hata kama walisema, je, walitoa ushahidi? na nani wa kutuhumiwa Katibu mkuu au Heche?
Kwanini wanasema HECHE na si Makamu Mwenyekiti.

Ushihidi wa MBOWE upo. Walimtoa magereza wakamkimbiza Ikulu. Kutokea hapo Mbowe akabadilika. Walikaa na Mbowe mwaka wakizungumza mwisho wa siku zero

Mbowe alisema kwa ushahidi kwamba kuna wenzetu walishiriki kuharibu maridhiano! Ushahidi kwamba yeye na CCM walikuwa na mitazamo sawa.

Mkandara, MBOWE alifanya madudu sana! hilo linahitaji ushahidi kweli. Ndiye wanamtaka au photocopy yake

Ni kweli, na bahati nzuri sisi wengine tulikemea hilo kwa msingi ule ule kwamba EL alikuwa fisadi kwa ushahidi
This dude you're busy educating it's sickening because he is deliberately dragging you through the treacherous path, kwao kumuweka Heche kwenye 'defense-mode' wanaamini kuwa wanampunguzia kasi.
Baseless hearsay stories and to make it worse ni pesa za michango ambazo presumably eti watu walizituma kwenye personal account yake, they're just plying dirty politics with no data-based facts.
 
Back
Top Bottom