Kwanini bidhaa nyingi zinazoagizwa kuja barani Afrika zinatokea China isipokuwa magari ambayo yanatokea Japan?

China brand zao za magari madogo wanatumia wenyewe na kiasi kidogo wana export. Pia China kuna viwanda vya kampuni kama Volvo,Benz,Toyota na Vw wanatengeneza gari ambazo zinatumika China na kuuzwa nje.
Nilikuwa silijui hili. Asante kwa taarifa mkuu...
 
Nimekukubali sana mkuu, uko so hamble...
Mkuu, mimi mtu akinikera sana (matusi/kejeli) ni bora nikamuweka katika IGNORE LIST yangu chaaap kuliko kukaa kutukanana mitandaoni jambo ambalo halina tija yoyote katika maisha yangu.
 
Magari ya China mbona yako mengi pia Mabasi asilimia 90 ni mchina, malori HOWO yamejaa kibao, kuna magreda ya kichina yameingia. Sawa magari madogo ya kichina hakuna ile magari makubwa makubwa yapo kibao

Malori bado mzungu Ana soko
Scania
Mercedes
Soko limehamia kwa maloli ya kichina saivi watu wanakimbilia faw gari lenye nguvu kama trekta na pia spear zake bei cheeeee.hizo scania na benzi ghalinsana kama spear zake
 
Mchina hakuwekeza zaidi uko kwhyo ni sahihi tu Mjapan kuwin soko lake la magari Africa. ...kingine mjapan hua pia alianza kuuza pikipiki zake Honda, Yamaha ambazo ni imara sana sema kwakua upaja wetu mdogo hatuzimudu
Ninazikumbuka sana hizi pikipiki ila kwa hapa bongo zinamilikiwa sana na watoto wa kihindi na kiarabu kule Kariakoo.
 
Jibu ni kwamba, mjapani ndo alianza kuliteka soko la magari used barani Africa. Mchina ameingia kwenye soko la magari hivi karibuni. Soko la japan lina wateja wengi na hii imevutia makampuni mengi kuanzishwa kwa ajili ya kuuza tu magari ya mtumba ya Japana
huko China kwenye bado mjapan anatawala soko hasa kwenye magari madogo.
 
Sidhani kama mchina atatengeneza gari zenye ubora kama mjapan, angalia tu kwenye pikipiki mchina kajaza za kwake za bei nafuu huku akiziondoa pikipiki za mjapan kama Honda, Yamaha ambazo bei yake usipime.
 
Machina mungu was dunia rafiki!
Habari za wakati huu kaka na dada zangu wote wa humu Jamiiforums.

Ndugu zangu watanzania;

Kwanini bidhaa nyingi zinazoagizwa kuja barani Afrika (Tanzania) zinatokea China isipokuwa magari ambayo yanatokea Japan?

View attachment 1634465

Ukiwa upo katika foleni ya magari barabarani, jaribu kufanya tathmini ya haraka haraka kwa kuangalia tu kwa macho kisha utagundua hizi ninachokisema.

Utagundua ya kuwa 98% ya gari zilizopo hapo ni za kutoka Japan (Toyota, Honda, Nissan, Suzuki, Mazda, Mitsubishi, Subaru, Isuzu) lakini bidhaa zingine madukani ni za kutoka nchini China. Why this? What's wrong with chinese automobile industry?

TAKWIMU NDOGO YA BIASHARA BAINA YA CHINA NA AFRIKA KWA MWAKA 2019
=====
According to statistics from the General Administration of Customs of China, in January-June, China’s total import and export volume with Africa was US$101.86 billion, up 2.9% year on year, exceeding the overall growth rate of foreign trade in the same period by 4.9 percentage points.

View attachment 1634490

Among these, China’s exports to Africa were US$52.86 billion, up 5.2% year on year and China’s imports from Africa were US$49.00 billion, up 0.5% year on year; the trade surplus was US$3.86 billion, up 159.0% year on year.

In June, China’s total import and export volume with Africa was US$17.09 billion, up 2.3% year on year. Among these, China’s exports to Africa were US$9.29 billion, up 0.3% year on year; China’s imports from Africa were US$7.79 billion, up 4.7% year on year; the trade surplus was US$1.50 billion, down 17.6% year on year.

In January-June, the growth rate of China’s trade with Africa was lower than those with Oceania(6.2%) and Europe(3.9%).
=====

View attachment 1634489

Kwanini magari kutoka China sio bidhaa maarufu hapa Africa (Tanzania) kama bidhaa zingine (domestic products) zilizojaa katika masoko/maduka yetu?

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
[/QUOTE]
 
Sidhani kama mchina atatengeneza gari zenye ubora kama mjapan, angalia tu kwenye pikipiki mchina kajaza za kwake za bei nafuu huku akiziondoa pikipiki za mjapan kama Honda, Yamaha ambazo bei yake usipime.
In Africa, price matters more than the quality
 
Siku sio nyingi mtayaona magari ya Kichina kila mahali barani Afrika ndio wameanza kuya uza kwa speed tofauti na ya Ulaya yao yatakuwa mapya
 
Siku sio nyingi mtayaona magari ya Kichina kila mahali barani Afrika
Kuna baadhi ya wadau humu ndani wanadai ya kwamba gari "second-hand" ya mchina inakuwa imechoka sana kiasi kwamba haifai kuja Afrika tofauti na gari ya mjapan...
 
Mkuu, tumeanza kutumia gari za Japan muda mrefu sana lakini kwanini hakuna "domestic products" zao madukani/masokoni mwetu?
Naona watu wana-hit around the bush na hakuna anayejibu. Ni hivi: China kuna mazingira mazuri ya wazalisha wengi wakubwa wa dunia kuwekeza viwanda vyao. Vitu kama cheap, reliable and high quality labour, Good Government policies vimevutia wawekezaji wengi kujenga viwanda vyao China. Hivyo basi China imekuwa kama ukanda wa kuzalisha bidhaa mkubwa kuliko sehemu nyingi za dunia. Bidhaa za China hazipo Afrika tu ila zipo dunia nzima isipokuwa nchi zilizoendelea zinapelekwa zile za grade nzuri. Kwa hiyo bidhaa nyingi zinatoka China kwa sababu ya cheap price. Ukija kwa upande wa magari, Japan wameanza kuzalisha magari siku nyingi na technolojia yao ni nzuri sana bila kusahau bei. China kwa upande wa magari wameanza kuzalisha kwa wingi siku si nyingi na teknolojia yao bado siyo nzuri hivyo ubora wa magari yao ni hafifu. Kingine: hali ya maisha ya China bado iko chini hivyo magari used yanayopatikana kutoka kwa raia wake hayako kwenye hali nzuri. Kwa kifupi kama ukichunguza utakuta nchi zilizo maarufu kwa kuuza magari used ni zile ziliendelea na raia wake wana uwezo.
 
Kuna baadhi ya wadau humu ndani wanadai ya kwamba gari "second-hand" ya mchina inakuwa imechoka sana kiasi kwamba haifai kuja Afrika tofauti na gari ya mjapan...
Kikawaida kama China ingekuwa nchi iliyoendelea bado watu wangeweza kununua kwa wingi magari used kutoka China kwani wachina wangekuwa wananunua mapya kutoka eg Japan kwa wingi na kuuza ya zamani yakiwa kwenye hali nzuri. Mfano ni nchi za Uarabuni. Hazitengenezi magari lakini bado ni maarufu kwa watu kwenda kununua magari used ambayo mengi yamenunuliwa mapya kutoka nchi nyingine. Lakini hali haiko hivyo kwa upande wa China kwa sababu China nayo ni choka mbaya. Raia wengi hawana uwezo wa kununua magari mapya na kuuza yaliyotumika yakiwa kwenye hali nzuri na kwa bei rahisi kwa wingi.
 
Back
Top Bottom