Kwanini bidhaa nyingi zinazoagizwa kuja barani Afrika zinatokea China isipokuwa magari ambayo yanatokea Japan?

ooh sasa mtumba wao wanauzia nchi gani?
gari za mchina lifetime ni ndogo yaani ukitumia kwa mdaa flani inakuwa imechoka hafu China ipo kwenye upper middle income ko hakuna restrictions sana kwa muda na Hali ya matumizi ya magari. Tofauti na Japan ipo in first world country ambapo Kuna restrictions za muda na Hali ya kumiliki gari hafu gari za mjapani ni imara Sana .
 
China ni left hand drive kwa hiyo hatiwezi kununua magari used toka huko wakati mjapan tunaendesha upande mmoja. Wabongo hatuna hela za kuweza kununua magari mapya so lazima mjapan abaki na ufalme wake. Hata USA used cars ni cheap kama Japan shida ni left hand drive ndio maana hatuagizi huko.
 
Ninachohisi ni kuwa nani aliyeanza kuendelea kati ya mjapan na mchina. Zamani nchi na alikuwa akitawaliwa na mjapan.
Japan ilishaendelea sana, kuanza na vitu vidogo vya majumbani na hatimae kwenye machine kubwa ikiwamo magari.
Wachina wameanza kuingia miaka si mingi, na kwa hulka yao ya kuagiza vitu, Walianza kujiimarisha kwa bidhaa za ndani, za kielektroniki na umeme n.k. wakawa ni wasambazaji wakubwa si Afrika tu bali hata Marekani.
Magari wameanza kutengeneza, ila kwa soko la Afrika na aina ya uchumi wa watu binafsi, magari ya kijapan ndio tunayamudu kwa upatikanaji wake na vipuri pia. Pengine ni suala la wakati tu, baadae Wachina nao watapata soko la magari madogo Afrika.
 
Kwani kwa ujuavyo wewe, magari makubwa ya mchina yameanza kuwa mengi around miaka mingapi iliyopita mkuu?
Hebu fanya research ya kilocal then uje na majibu. Utakubaliana na alichozungumza mwana jf hapo juu.
Mchina gari kubwa alianza kitambo kuleta hapa Tanzania kama unazikumbuka Jefang zilikuwa zinafanana na Isuzu Tx Injection au Nissan Diesel zile zenye pua ndefu miaka ya 1980-1990. Nyingi kwetu zilikuja tipper na long base kama hiyo pichani.
images.jpeg

Hizi zilianza kupotea baada ya ujio wa Mitsubishi Fuso,Isuzu ftr na forward.

Baada ya hapo mchina ameanza kuleta gari kubwa hapa Tanzania nadhani miaka ya 2005(sina kumbumkumbu sahihi), hao Jiefang sasa wakawa wanaleta gari zao kubwa zinazoitwa FAW tunazoziona mpaka sasa. Saizi kuna Maroli Yao brand tofauti kama FAW,Howo,Beiben,Foton, Shacman,Dongfeng.
 
China brand zao za magari madogo wanatumia wenyewe na kiasi kidogo wana export. Pia China kuna viwanda vya kampuni kama Volvo,Benz,Toyota na Vw wanatengeneza gari ambazo zinatumika China na kuuzwa nje. China gari za kutoka ulaya,Japan na marekani watu wao bado wana agiza.
 
gari za mchina lifetime ni ndogo yaani ukitumia kwa mdaa flani inakuwa imechoka hafu China ipo kwenye upper middle income ko hakuna restrictions sana kwa muda na Hali ya matumizi ya magari. Tofauti na Japan ipo in first world country ambapo Kuna restrictions za muda na Hali ya kumiliki gari hafu gari za mjapani ni imara Sana .
Kweli kuna Zile BJ Jeep za mchina watu waliokuwanazo kuzihudumia vipuri ilikuwa kasheshe ni mwendo wa kuagiza, gari ikianza kuchoka ndio moja Kwa moja.

Kwenye Light truck kuna Zile Catic zipo kama Mitsubishi Canter watu walikuwa wananunua Kwa wachina waliomaliza miradi, kasheshe zilipoanza kuchoka ni mwendo wa kudai vipuri na hazitengamai tena.
 
Kweli kuna Zile BJ Jeep za mchina watu waliokuwanazo kuzihudumia vipuri ilikuwa kasheshe ni mwendo wa kuagiza, gari ikianza kuchoka ndio moja Kwa moja.
Mkuu, ninadhani hata Japan kama wangekuwa hawajateka soko la magari hapa Afrika watu wangekuwa wanaagiza sana vipuri vya gari zao kama magari ya kichina...
 
Jibu ni kwamba, mjapani ndo alianza kuliteka soko la magari used barani Africa. Mchina ameingia kwenye soko la magari hivi karibuni. Soko la japan lina wateja wengi na hii imevutia makampuni mengi kuanzishwa kwa ajili ya kuuza tu magari ya mtumba ya Japana
 
Kwahiyo hapa nimekukera sio?

Sawa kuniweka ignore list nadhani ni uamuzi bora kabisa ukiona nakukera.
Hapana sijakuweka leo, nilikuwekaga tangia mwezi wa saba (July) kwa maana kuna neno baya ulinijibu (Personal Attack) ila sasa silikumbuki.
 
Back
Top Bottom