Kwanini biashara yako haikui? Jifunze Jinsi kampuni hii ilivyokuza mtaji kufikia mabilioni ya pesa

Its Jensen

Member
Mar 30, 2023
14
18
Habari wana jamii forum, ni matumaini yangu mnaendelea salama baada ya mda mrefu kupita bila kushusha thread ya moto....

Leo nimependa kuzungumzia swala zima la mauzo (sales) na jinsi ya kuongeza wateja kwenye biashara, kuna msemo unasema "kufungua biashara na kuuza ni vitu viwili tofauti kabisa" kumekua na ongezeko kubwa la vijana wanaoingia katika biashara kwa lengo la kujipatia kipato kutokana na ukosefu wa ajira.

lakini miongoni mwa vijana wanaoingia kwenye biashara ni asilimia chache sana wanaofanikiwa katika biashara wanazoanzisha, na tatizo kubwa wanalozungumzia ni ukosefu wa wateja........

Kuna msemo hua nasema, kuingia kwenye biashara ni sawa na kuingia vitani, kwenye biashara hakuna urafiki wala undugu, kila mtu yupo kwa ajiri ya kusaka faida. Je, kama tatizo linalosababisha biashara nyingi kufa ni ukosefu wa wateja? je wafanyabiashara waliokwenye biashara zaidi ya miaka kumi wao walifanikiwaje?

Ngoja nikupe story fupi ya kampuni moja ya vinywaji iliyojipatia umaarufu mkubwa kama "Marketing killer" baada ya kuja na mbinu mpya ya kupata wateja na kuongeza mauzo ndani ya mda mfupi. Kampuni ya Redbulls ilianzishwa mwaka 1987, kama kampuni ya kwanza ya vinywaji vya Energy drink, kampuni hii ilipitia changamoto kubwa ya kuuza bidhaa zake sababu kulikua hakuna kampuni yoyote iliyokua ikiuza vinywaji hivyo vya kusisimua
rred.jpg


Baada ya kutafakari kwa mda mrefu ndipo walipokuja na mbinu mbili ambazo waliamini kua lazima zitaleta mapinduzi makubwa katika mauzo yao

Mbinu ya kwanza ilikua ni kuwalenga wanafunzi wa vyuo ambapo walikua wanatoa vinywaji vyao bure kwa wanafunzi na kuwambia vitawasaidia kwenye kipindi cha mitihani yao kufocus usiku kucha bila kusinzia, hii mbinu ilifanikiwa sana kuongeza mauzo hata leo kwa wanafunzi hunywa energy drink sana wakiamini hawatasinzia kwenye mitihani

Mbinu ya pili ilikua ni "Iga ufe au mama mkanye mwanao" hii ilikua mbinu ya kusambaza makopo ya redbulls kwenye madampo yote, kwenye maklabu, kwenye maduka yani ilikua ni vurugu, walisambaza matupu mengi sana mtaani. Unaweza kujiuliza mbinu hii iliwasaidiaje kuongeza mauzo????

Ngoja nikwambie watu wengi hufanya vitu kwa mkumbo(tamaa ya kujaribu) baada ya watu kua wanaona makopo mengi ya redbulls mtaani waliamini kua wenzao au majirani wenzaowatakua wamekunywa hivyo na wao watahijati kujaribu kuonja radha yake, then BOOOM unywaji wa redbulls uliongezeka kwa kasi kubwa sana na kufanya kampuni hio kua ni miongoni kwa kampuni tajiri zaidi duniani

Hivyo wewe kama mfanyabishara wa mtandaoni au wakwaida unatakiwa kubuni mbinu ambayo itawafanya watu wasiokufahamu kua wateja wako, hasa hichi kipindi teknolojia imekua sana, ndio mana hua napenda kuwambia wafanyabiashara wengi saivi hakikisha unatafuta Walengwa au hadhira ya bidhaa au huduma Yako.

Kumbuka,Kujifunza Kulipia matangazo fb na Instagram haiepukiki kama uko Serious na biashara yako Mtandaoni.

Na kama hujui Kulipia Matangazo FB na Instagram wewe bado hujajua utamu wa biashara Mtandaoni. Badoo sana.

Kama hujui Kulipia Matangazo FB na Instagram nimeandaa darasa la watu 20 ambapo ninaoyoonyesha Hatua kwa Hatua jinsi ya Kulipia matangazo fb na Instagram na Kupata Wateja mara 10 ya wale Unaopata kwa sasahivi Tena kwa gharama sawa na BURE Kabisa, sababu najua 90% ya waTanzania hawajua kufanya matangazo kama inavyotakiwa na kuishi kuchoma pesa bila kupata wateja na kusema matangazo ya kulipia hayana faida

PIa nimekuandalia kitabu ambacho kina siri nzito ambazo mwanzilishi wa louis vuitton na Asian Dragon mafia Dan Lok wanazitumia


Utakapo lipia kitabu hiki utapata bonus pia utaungwa kwenye group la mafunzo ya kulipia matangazo kwa utaratibu sahihi, ambapo utaungana na wafanyabiashara wengine na kupatiwa mafunzo yatakayofanyika online kupitia Google meeting ambapo yatakua yamegawanyika sehemu 2, sehemu ya kwanza itakua kwa wale wanaofanya biashara mtandaoni na sehemu ya pili itakua wanaofanya biashara za kawaida

Uwe na siku njema .

View attachment 2644875
 

Attachments

  • jamiiiii.jpg
    jamiiiii.jpg
    48.5 KB · Views: 29
  • Blue Soft Magazine Mockup Pinterest Pin.jpg
    Blue Soft Magazine Mockup Pinterest Pin.jpg
    110.2 KB · Views: 39
nimerudi kuangalia jina la mtoa mada....hii mbinu ya redbull sikuwahi kuiskia.. ila ile ya ukiwa na hoteli au biashara yako kuwapa posho watu maarufu kuja kutumia na kupiga picha na kupost .. kama gadna alivyokuwa anaost anakunywa gugmister mara kwa mara ilinifanya niinunue 80k chupa kubwa bwana weee mixer pariki stanger taste balaa mix sukari nikasema si bure walimpa aipromote kiaina...ila kwa wengine ffresh tu.
 
Back
Top Bottom