Jun 23, 2020
17
7
Ujana : nihatua ya ukuaji anayoipitia mtu baada ya kumaliza hatua ya utoto ili kuelekea utuuzima na uzeeni na hii hatua hutakiwa kuwa Makini na mtulivu wa fikra pamoja na akili nyingi kuliko hatua nyingine yoyote, na hii ndio hatua pekee ya utambulisho halisi wa mtu kifikra, kiutendaji na hata kujua hatima yake ya mbeleni kutokana na vile atakavyo onekana katika maisha ya ujana. Na umri kamili wa maisha ya ujana ni miaka 18- 40 kwa mwanaume , 18-35 hii ni kwa mwanamke inatosha kuishi na kukujua taswira na uwezo wako Kama mwanadam halisi kwenye nguvu ya maamuzi juu ya maisha yake.

Kwa Nini iwe miaka 18-40 kwa mwanaume?

1) Mwanaume huwa anachelewa Sana kutambua mabadiliko ya hatua za ukuaji kuliko mwanamke pia huwa bado Hana changamoto za kumuumiza akili akiwa chini ya umri huo hataivyo ni wachache Sana ambao miili yao inakuwa imekaza kifikra na hata ukakamavu wa mwili kufanya kazi mchanganyiko au ngumu.

2) Kipindi hiiki kwa mwanaume nikizuri kuyapanga maisha yake yeye mwenyewe Kama akiamua kuhusu hatima yake mwenyewe kwasababu huo ndio muda kamili wa kusoma, kufanya kazi , kuwekeza,kujipatia mahitaji yote muhimu Kama chakula, makazi, mavazi pamoja na usalama wa akiba ya afya kwaajili yake mwenyewe na maandalizi ya tegemezi baada ya kuvuka umri huo 18-40

3) Kipindi hiki ndicho kipindi muhimu kujichanganya na watu sahihi wa hatima yako Kama kisiasa, kibiashara, kiimani na nyanja kadha wakadha ili kuonyesha umaridadi wako na kuaminika na jamii inayokuzunguka pia itakupa heshima ya awali kabla ya heshima kubwa itakayokuja baada ya ndotozako kutimiliza

4) Ili ufaidi kuishi maisha ya ujana Hali ukiwa unalenga kwa wakati huohuo kuandaa mazingira ya kuipokea hatua ya utuuzima Basi zingatia kupunguza starehe na anasa ambazo hazitakupa kuaminika na jamii au zitakazokuzuia kuwafikia watu muhimu wa hatima yako, penda kujichanganya na watu waliokutangulia kwenye hatua unayoitazamia kuipitia ili kutimiza ndoto zako, fanya kazi kwa bidii ule vizuri kipindi hiki, uwe na mtu wakukushauri kimipango na hata kitabia, uwe na uhusiano unaokuletea matokeo chanya ili kutimiliza ndoto zako cz mahusiano yasiyo ya kimkakati yamewapekekea vijana wengi kuivuka hii hatua na kushtukia wamevutwa na kundi la watu wazima tafuta msichana utakayempa vigezo na mashart yako atakayekubali kuyatimiza kaanaye umtengeneze akufae kwa hatua ijayo ukigundua hawezi, bado hajajipanga mpe likizo endeleza majukumu ya kimkakati katika hatua yako cz nimuhimu Sana kwako.

Kwanini mwanamke miaka 18-35?

1)Kwa kipindi hiki mwanamke anakuwa kashakomaa kiakili na hata kimaumbile kuikabili hatua ya kuitwa mama napia Kama ni wakusoma kashafika elimu nzuri na kazi anafanya na mahitaji yake yeye Kama yeye kashayawekea njia nzuri , napia ashaandaa mazingira ya kuiendea hatua ya kuitwa mama au mlezi wa familia japo kwa hatua hii Kama mwanamke atakuwa tayari kashafikia malengo yake kwa asilimia 90% Kama alijipanga kujiongeza vizuri toka akiwa na umri wa miaka 18. Na kwa mwanamke ni tofauti Sana mwanamke nirahisi Sana kumshawishi mwanaume na kumbadilishia upepo ila sio rahisi kwa mwanaume kumshawishi mwanamke aliyejipanga na anayejiendesha kimkakati.

2) Kipindi hiki kwa mwanamke anakuwa ameshaanza kuitunza vyema familia yake kutokana Yuko serious na ujana wake autumie kikamilifu na katika swala la uwekezaji Kama atakuwa hajaanza kuwekeza inashauriwa awekeze Sana katika hatifungani au hisa za mabenki na makampuni Kama anauwezo huo au kwa vitu ambavyo havigusiki ili kujilinda na vurugu zozote endapo zitatolea asipate msongo mkubwa wa mawazo na pia Kama mwanamke haishauriwi kutaja Mali zako kipindi Cha mahusiano please zingatia ilo.

Kwa kumalizia pande zote mbili wanaume na wanawake ili msikivuke haraka kipindi Cha ujana bilakufanya maandalizi ya kutosha ya hatua ijayo jitahidi Sana kujizuia na kuwa na kiasi katika kilajambo unalolifanya fanya uku ukijipima je? Jambo hili linaniongezea Kasi ya kutimiliza ndoto zangu na kuishi vyema maisha ya ujana Hali nikijipanga na wakati ujao? Ukiona linachangia kupunguza kwa asilimia kubwa achana nalo . Mwisho kabisa ibada na maombi kilamtu kwa Imani yake itakusaidia kuyalinda yote uyapangayo maana kulogana kupo na kuharibiana kimazingara kupo kwaiyo kilamtu ajilinde kwa Imani yake

By
Sam the bossa
 
Kinachonisikitisha katika wakati huu wa ujana wangu kila demu ninaepishana nae ana chura matata sana, na walivyo na roho nzuri hawakunyimi namba ya simu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom