Dear Ujana

Amani Dimile

JF-Expert Member
Jul 27, 2022
243
395
Dear ujana, simu yako niliiona ikinipigia tangu nilipokuwa na umri wa miaka 17 na nilipokea kwa furaha sana kwa kuwa niliamini tayari nishaanza kupata kibali cha kuingia zile sehemu zinazokataliwa kuingia watu wenye umri chini ya miaka 18.

Dear ujana, nasikitika kusema umeniharibia sana future yangu. Ni afadhali mara mia ningebaki na utoto tu kuliko kupata balehe na kuanza kuelewa mengi juu ya mwili wangu na tamaa za hisia zangu.

Dear ujana, nakulilia wewe kwa kuwa ndie uliyenifanya niishi kwenye maisha ya dhambi huku nikihisi ndio ujanja. Ukapotosha nafsi yangu, nikaamini na enjoy maisha kumbe naharibu future. Nikajihisi najua sana kuliko hata walionileta duniani. Nikawa sishikiki, ukanichukua na kuniingiza kwenye kila aina ya Kasino. Ukanikutanisha na kila aina ya mwanamke, nami nikashindwa kuzuia mkono wangu kufungua zipu mbele ya kila mdada mzuri. Nalia mimi, nakulilia ujana.

Dear ujana, wewe ni mbaya sana nakosa hata maneno ya kukuelezea na ndio maana hata wahenga wakakuita maji ya moto. Wapo wakaka wanaojuta kubalehe kisa wewe, na wapo wadada wanaojuta kuvunja ungo badala ya sahani sababu yako wewe.

Nimlaumu nani, nakulaumu wewe ujana. Angali nilipokuwa mtoto ulimchukua yule dada wa jirani yetu akajinyonga sababu yako. Ulikatisha ndoto za watu wengi, wengine ukawafanya waitwe mama mbele ya vijana ambao mapenzi yao hayakutosha kuwafanya waitwe wake.

Dear ujana, tazama hata Bakari Kipua yule aliyesifika kuwa ni handsome juzi tulimzika kwa maradhi ya ngono yaliyokuwa yakimsumbua sana. Hata Jamila Kidoti, licha ya wazazi wake kupambana kumsomesha ila ukamfanya arudi akiwa na mimba isiyomjua baba.

Dear ujana ndio wewe uliyeharibu kizazi hiki cha Amapiano. Ukaleta misemo yenye ujinga na upumbavu ndani yake. Hivi sasa wavunja ungo wanasema "Mjini msingi kiuno" na wakaka wapata balehe wanasema "atakaejipindua, mpe haki yake" wewe ujana ndio umefanya watu waamini starehe ndio maana halisi ya maisha.

Dear ujana, tazama unavyopoteza watu wa zama hizi. Hivi sasa ngono ndio kipimo cha mapenzi ya dhati, pesa ndio uzuri wa mwanaume, shepu ndio umaridadi wa binti, shisha na pombe ndio kupoa kupunguza stress.
Ni wewe ujana ndie uliyafanya uzuri wa mwanamke utegeme aina ya simu anayotumia, na ndio wewe wewe ujana uliyefanya kupoteza simu kuume zaidi kuliko kupoteza bikra.

Ewe ujana ajabu yako kubwa ni kwamba unafanya watu wengi wakujutie wakiwa tayari washaangamia, tazama nakulilia nikiwa nipo kwenye kitanda cha watu mahututi huku nikihesabu tu sekunde za kumsubiria malaika mtoa roho. Yote ni kwa ajili yako ujana, yote ni kwa ajili yako ujana, Kwa ajili ya ...... ya.... ko.. u u ja ... ujana.

young-african-man-patient-suffering-from-high-fever-having-flu-o-while-lying-with-in-hospital.jpg
 
Ujumbe mzuri Sana ......Ukiwa kijana usipokuwa na control ya matukio yanayotokea utaangamia

View attachment 2755520
 
Back
Top Bottom