Kwaherini JF

Status
Not open for further replies.
Joanah, nimesikitika sana kusikia changamoto hii, lakini nataka ukumbuke kuwa wewe ni mpiganaji na una nguvu kubwa ndani yako. Katika Jukwaa tumekujua kama mtu wa msimamo, na hata sasa usikate tamaa; kila siku mpya ni ushindi na fursa ya kuishi kwa tabasamu na amani. Sisi kama familia yako ya JF tuko nyuma yako kukushika mkono.
Umbali siyo tatizo, ninakupenda Joanah!..

Sala yangu kwako leo: Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema na faraja, akushushie amani inayopita ufahamu wote wa wanadamu. Akupe nguvu mpya kwenye mwili na roho yako, akuepushe na hofu, na akujaze matumaini makuu. Tunajua hakuna linaloshindikana mbele zake; Mungu akufanyie wepesi na miujiza ya uponyaji, na akuzungushie upendo wake kila sekunde ya maisha yako. Amen."
 

Huu ndo upuuzi wa JF

Ulichoandika hapo natakiwa nikushike matakko huku nikikuaminisha sio?

Fvck off mzee
Lengo la uzi sio kubembeleza mtu aamini
 
Parapanda italia parapandaaa!!

Parapanda italia parapandaaaa!

Waliokwisha takwaswa, watakuwa wamekwisha nyakuliwaaaa, Kwendaa kumlaki Bwana Yesu Mawinguniiii.

Walio okoka watakuwa wamekwisha nyakuliwa, Kwenda kumlaki Bwana Yesu mawinguniiiii.
 
Fanya mpango wa kuniletea Kiko kabla hujaondoka mjukuu πŸ₯² (jokes)

Kwa kweli nimesikitika kusikia habari hizi, nashauri kama Kuna nafasi nenda urudie kupima kufanya ulinganisho wa majibu (Madaktari nao hupitiwa)

Kuugua saratani sio mwisho wa maisha

Ni matumaini yangu yule aliyekuumba, anaweza kukupa miaka mwingine ya kuishi

Kama aliweza kumpa miaka mingine 15 Mfalme Ezekiel hawezi kushindwa kukupa wewe miaka mingine zaidi (2 Wafalme 20:6)

Mungu aendelee kukutunza mjukuu πŸ™πŸ™
 

Mkuu 😭😭
 

Huu ushauri wa kupima tena nipo nao natarajia kufanya vipimo tena ndani ya wiki hii inayoanza

Kimsingi sijui ni how nimepewa majibu hayo, sina maumivu na wala sijisikii kuumwa kabisa lakini taarifa iliyopo ni hiyo
 
Allah atakuafu na utapona, wewe ni Muislamu na usidanganyike ukaenda kwa waliopotea manabii feki n.k.

Jikite kwenye ibada, muombe Mwenyezi Mungu akuondolee maradhi n.k. na acha kumshirikisha kwa chochote
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…