mngony
JF-Expert Member
- Jul 27, 2012
- 5,212
- 6,409
Tunaanza kusikia tuliyokuwa hatuyajui au kuthibitisha yale tuliyokuwa tukidhania, kwa yanayondelea kutamkwa na Sabaya ni wazi hata kitendawili cha waliomshambulia Tundu Lissu na kilichowasukuma kinaweza kutatuliwa.
Sabaya anatamka kabisa kuwa alifika KIA akakutana team ya watu 4 ambao hawezi kuwataja ambao alienda nao kufanya operation aliyopewa na Mamlaka ya uteuzi.
Anaenda mbali kusema operation hiyo baadhi ya watu waliifahamu, inawezekama lengo ni kuhakikisha operation inaenda salama bila kukatizwa hata kama wengine hawajui ni operation gani na mengi aliyoongea.
Nikiangalia naona kabisa kuwa hata suala la Kushambuliwa Lissu, inawezekana pia ilikuwa operation nyingine, ukizingatia kulikuwa na fununu za Bashite kuwepo Dodoma wakati shambulizi linatokea.
Lakini pia wakati shambulizi linatokea inawezekana mamlaka zingine na watu wa makazi hayo( tunaambiwa ni ya viongozi) waliambiwa kuna operation japo hawajui ni aina gani na ndio inaweza kuwa sababu hakukuwa na ulinzi kabisa tofauti na siku zote na hata camera kutolewa?
Kingine kinachoonekana kuna watu wachache sana waliaminiwa na Mamlaka ya uteuzi kuweza kufanya operation za namna hii, ndio maana yule Sabaya alitoka Hai kwenda Arusha kufanya operation, na inawezekana mwingine alitoka Dar kwenda Dodoma.
Tundu Lissu mwenye alisema wakati anashambuliwa Mkuu wa Mkoa wa Dar alikuww Dodoma.
Ninachojiuliza hizi zilikuwa 'Rogue' operation? Inaonekana kuna kikundi cha watu( wasiojulikana) kiliundwa nje ya Taasisi rasmi, ndio maana zimefanya mambo 'kishamba' sana.
Nimpongeze Lissu kwa akili za haraka za kuamua kukilaza kitu yeye na dereva wake na kivuweka mbali viungo muhimu sana vya mwili, kana kwamba alipitia mafunzo, pia faida ya kuwa na tinted hawakuweza kuonwa kuwa wamelala.
NB; Majuma kadhaa kabla ya tukio kulitolewa amri ya kuondoa tinted zote kwenye magari mkoani kwake, baadae nadhani ikawa ngumu huenda operation ilipangwa ifanyike Dar ndio maana Lissu alianza kulalamika kuwa kuna gari zinamfatilia
Je wasiojulikana wanaanza kujulikana?

Tundu Lissu: Siku napigwa risasi Paul Makonda alikuwa Dodoma
Hints: Tundu Lissu anasema kuwa siku aliyopigwa risasi ndio siku Rais Magufuli alikuwa akipokea ripoti ya makinikia. Na masaa mawili kabla ya shambulio lake alitangazia umma kuwa kuna mtu anapiga kelele sana huko nje na katika vita jeshini watu wa namna hiyo ni sawa na wasaliti hivyo kazi huwa...
www.jamiiforums.com