Kwa Wizara ya Elimu: Kuhusu cut point za kuingia chuoni kwa waliomaliza Form Six 1980s- 2014

shono

Member
Mar 3, 2024
14
18
Hili suala la cut point za kuingia chuo kikuu zilipandishwa na waziri wa Elimu kipindi hicho (Ndalichako) kiliwaumiza wengi wengi sana hasa watumishi wa umma wenye kutaka kujiendeleza kielimu.

Wiziri alipandisha kwenda cut point 4 Kila chuo badala ya cut point 2 hili suala liliwaumiza vijana wengi wenye ndoto ya kusoma badala yake wapo vijiweni wasijue cha kufanya.. watumishi wa umma wengi wanashindwa kujiendeleza kisa kigezo hicho.

NOTE
Tunaomba iwe kama zamani waliomaliza miaka ya 90s Hadi 2014 washushiwe cut point kama ilivyokuwa zamani kwenye vigezo vya kuingia chuo kikuu.
 
Zamani chuo kikuu ulikuwa unaingia kwa E mbili na sasa hivi unaingia kwa D mbili.

Hivyo katika muongozo wa TCU ebu jaribu kusoma vizuri utaona na wakati Wa kuomba chuo huwa wameweka vigezo ambavyo vinaonesha watu waliomaliza zamani na wa hivi karibuni so fatilia kwanza.
 
Sasa mtu km ww unataka uende chuo kikuu hata ulichoandika hakieleweki. Si lazima usome huko. Ulichoandika kinaitwa cut off points. Inaanzia 13.5, we umepata ngapi.
 
Tusipende kukosoana hapa nilicho maanisha Mimi. Miaka ya nyuma 2014 kurudi nyuma vigezo vilikuwa E+E but ndalichako alivyoungia 2015 akataka D 2 sasa hao waliomaliza hiyo Miaka ya 2014 kurudi nyuma hizi sifa hawana Kwa kuzingazia mwongozo wa TCU.. waziri kama alitaka maboresho angetakiwa azingatie na wale aliowakuta nyuma yake.. Hapa tuna rundo la watu ambao Wana D+ E au wana E+E. Naomba wizara husika waliangalie hili..
NOTE
Makosa mengine ni ya kiundishi tu kama huna Cha kusema Bora kukaa kimya.. nawapazia sauti vijana wanaokosa Fursa wakati wanazo sifa
 
Cut off point ni tofauti kutegemean na ni wa zamani ni wa karibuni?
TCU wanataka uwe na D Mbili wakati 2014 kurudi walikuwa wanaenda na E Mbili na kuendelea...swali langu wizara haioni kama imedhurumu haki ya vijana wengi wa kuanzia 2014 kurudi nyuma
 
Siku hizi hicho
Zamani chuo kikuu ulikuwa unaingia kwa E mbili na sasa hivi unaingia kwa D mbili.

Hivyo katika muongozo wa TCU ebu jaribu kusoma vizuri utaona na wakati Wa kuomba chuo huwa wameweka vigezo ambavyo vinaonesha watu waliomaliza zamani na wa hivi karibuni so fatilia kwanza.
Siku hizi hicho kigezo hakipo kabisa wanataka kuanzia D Mbili na kuendelea kulingana na chuo.. kuanzia waziri ndalichako alivyoungia TCU walibadilisha kigezo Cha watu waliomaliza kabla ya ndalichako
 
Kama unahitaji Sana kuingia chuo Ebu soma foundation course kupitia open university ili upate kigezo cha kusoma degree
 
Kwa sasa E mbili utapata udahili wa diploma mkuu ,labda anza na diploma then uje usome bachelor degree
Hili suala la cut point za kuingia chuo kikuu zilipandishwa na waziri wa Elimu kipindi hicho (Ndalichako) kiliwaumiza wengi wengi sana hasa watumishi wa umma wenye kutaka kujiendeleza kielimu.

Wiziri alipandisha kwenda cut point 4 Kila chuo badala ya cut point 2 hili suala liliwaumiza vijana wengi wenye ndoto ya kusoma badala yake wapo vijiweni wasijue cha kufanya.. watumishi wa umma wengi wanashindwa kujiendeleza kisa kigezo hicho.

NOTE
Tunaomba iwe kama zamani waliomaliza miaka ya 90s Hadi 2014 washushiwe cut point kama ilivyokuwa zamani kwenye vigezo vya kuingia chuo kikuu.
 
Anzia Diploma mkuu. Watoto siku hizi wanapiga ONE kama uchafu halafu wako wengi mno. Hata hizo D mbili ni ngumu kupata UDSM kwenye kozi nyingi. Waziri alikuwa sahihi kupandisha vigezo.
 
Zamani chuo kikuu ulikuwa unaingia kwa E mbili na sasa hivi unaingia kwa D mbili.

Hivyo katika muongozo wa TCU ebu jaribu kusoma vizuri utaona na wakati Wa kuomba chuo huwa wameweka vigezo ambavyo vinaonesha watu waliomaliza zamani na wa hivi karibuni so fatilia kwanza.
Zamani ipi mkuu? Mimi zamani ninayojua chuo kikuu bila point 6 kwa mvulana na 8 kwa msichana huingii. Kumbuka pia wakati huo D na E hazikuwa principal pass.
 
Tusipende kukosoana hapa nilicho maanisha Mimi. Miaka ya nyuma 2014 kurudi nyuma vigezo vilikuwa E+E but ndalichako alivyoungia 2015 akataka D 2 sasa hao waliomaliza hiyo Miaka ya 2014 kurudi nyuma hizi sifa hawana Kwa kuzingazia mwongozo wa TCU.. waziri kama alitaka maboresho angetakiwa azingatie na wale aliowakuta nyuma yake.. Hapa tuna rundo la watu ambao Wana D+ E au wana E+E. Naomba wizara husika waliangalie hili..
NOTE
Makosa mengine ni ya kiundishi tu kama huna Cha kusema Bora kukaa kimya.. nawapazia sauti vijana wanaokosa Fursa wakati wanazo sifa
Kabla ya mwaka 2010, hakuna mtu mwenye D ama E ambaye angepata nafasi ya kwenda chuo kikuu.
 
Zamani ipi mkuu? Mimi zamani ninayojua chuo kikuu bila point 6 kwa mvulana na 8 kwa msichana huingii. Kumbuka pia wakati huo D na E hazikuwa principal pass.
Nilimaliza form six mwaka 2003 na C flat (1, 9) na sikupata Chuo. Rafiki yangu alikua na C D E akaenda kuanzia Diploma Korogwe. Zilikua principal passes ila kupata nafasi ndio ilikua ngumu.
 
Zamani chuo kikuu ulikuwa unaingia kwa E mbili na sasa hivi unaingia kwa D mbili.

Hivyo katika muongozo wa TCU ebu jaribu kusoma vizuri utaona na wakati Wa kuomba chuo huwa wameweka vigezo ambavyo vinaonesha watu waliomaliza zamani na wa hivi karibuni so fatilia kwanza.
Siyo lazima iwe D mbili, yaweza kuwa C moja na E moja unakuwa na sifa ya kudahiliwa chuo kikuu.
Sifa kuu ni mbili;
1. Uwe na principal passes mbili (E, D, C, B au A)
2. Jumla ya points zisipungue 4.0 kwenye hizo principal passes mbili (Yaweza kuwa D mbili au C moja na E moja).
 
Back
Top Bottom