Uchambuzi maalumu kuhusu sintofahamu katika utoaji wa Mikopo kwa wanafunzi wa Elimu ya Juu

adriz

JF-Expert Member
Sep 2, 2017
10,951
23,093
Habari za muda huu wana Jf .

Mimi kama mdau wa maswala ya elimu hapa Tz hilo suala nimeliona kubwa ,muhimu na linapaswa kupatiwa ufumbuzi.

Nimepitia nyuzi mbalimbali humu ,maoni ya wadau ,wanafunzi na utafiti wangu binafsi nimegundua kuwa kuna malalamiko makubwa katika utoaji mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu wanaoanza masoma haswa kwa mwaka jana na mwaka huu.Nakumbuka mwaka jana wakati bajeti ya fedha zilizotengwa kwa ajili ya mkopo zinatangazwa watu wengi walipongeza serikali na Muheshimiwa Rais Samia Hassan Suluhu kwani likitoka fungu kubwa sana kulinganishwa na miaka ya nyuma na watu wengi walijua wanafunzi akaunti zao zitanenepa.

Ila ajabu baada ya watu kupangiwa kikiwa na malalamiko mengi na ni kweli wanafunzi wengi kwa mara ya kwanza walipewa pesa kiduchu mimi binafsi watu 10 ninawajua wote hawakuvuka asilimia 25% mpaka mtoto wa jirani yangu alinunua Pc kama maandalizi yake kwa ajili ya kusomea chuoni majibu yalivyotoka nilimsikia akitangaza kuuza Pc yake aongezee hela ya ada na akisema huku akisikitika "vibe lote la kwenda chuo limekata". Vilevile ilizoeleka watu wanaosomea kozi za science ,ualimu na nyingine zenye vipaumbele kupata pesa nyingi lakini hali ilibadilika hata wale wa Muhas walipigwa 'Ndoige' wapo waliopata mpaka 25% tofauti na miaka ya nyuma.

Baada ya taarifa hizo ikabini mimi niichunguze kunana halo hii wakati limetoka fungu kubwa kabisa ? nikapata taarifa kuwa mwaka huo(2021) watu wengi walidahiliwa na vyuo hivyo Bodi ikaamua bora kupunja kuliko kujaza wakakosa kwenda chuo watu wengi.
IMG_20221028_171957.jpg

Ukinzani waibuka:
Kutokana na hali hio kukaibuka na maoni tofauti ,kuna watu walidai serikali imekosea kwani kutoa fedha kiduchu bora wangewapa kwa idadi inayoendana kwani kuna watu kwao hizo asilimia ishirini wanaona ni kama kuwatesa wanafunzi ,kutokana na gharama kutoka na mahitaji ya chuo na ada haswa mtu akitokea katika familia duni.
IMG_20221028_172023.jpg


Kwa wengine wanaona mpango huo ni bora kwani itawezesha wanafunzi wengi kusoma hata ikiwa kwa kuongezeka kiasi fulani kuliko kukosa kabisa
IMG_20221028_223955.jpg


Hali ya mwaka mpya wa masomo (2022/2023).


Mwaka huu imetushangaza kidogo watu waliyegemea kutokana na hali ya mwaka jana bajeti ya mwaka huu itakuwa ya kushindo zaidi lakini hali ikawa tofauti imeongezwa lakini wengi wamesema ni kiasi kidogo kilichoongezwa tofauti na nyongeza ya mwaka jana.Vilevile kukaja na Samia Scholarship bilioni kadhaa kwa ajili ya kutoa ufadhili kwa wanafunzi walifanya vizuri masoma ya Sayansi na kuchagua vyuo vya hapa nchini kupata mkopo asilimia 100% ikijumulisha udhamini wa kila kitu.

Baadhi ya wadau walioinga hiki kitu wakaona pesa hiyo itawanufaisha wengi watoto wa marafiki ambao Baba zao wana uwezo wa kuwasomesha maana huwezi kumkuta mwanafunzi wa Kantalamba high school akitoboa katika hiyo list zaidi zmya kuwakuta wa Feza ,Ahmes nk.

Majibu ya mkopo kwa mwaka huu yapo vipi ?

Kwa mwaka huu baadhi ya wanafunzi tayari wameshapangiwa lakini hali ni bado mbaya naona wengi wanalalamika bado hawajapangiwa kwa niliobahatika kuwaona kam watatu hivi kidogo kuna ongezeko tofauti na mwaka jana .

Vilevile sasa hivi sio kama zamani Yatima pamoja na wale wanotoka kaya masikini (Tasaf) kupata pesa nyingi ,kwani karibia watano nikiowaona wote wamepata asilimia 50% na kuna mmoja yupo humu Jf mpaka sasa hajapangiwa na amekata tamaa kabisa.
IMG_20221028_174802.jpg

Huzuni zimetawala.
IMG_20221028_145154.jpg



IMG_20221028_145325.jpg


Je serikali imeansisha mpango gani , vipi na hili limetazamwa ?

Bahati nzuri nilikuwepo katika halfa fupi pamoja na waandishi wa habari makao makuu ya Bodi ya mkopo katika kuzindua mchakato wa uombaji kwa mwaka huu, nilishuduia moja kwa moja Waaziri wa elimu Profesa Adolf Mkenda akitambukisha timu yake ya wataalamu kuchunguza muendendo wa Bodi ya mkopo na mchakato msimu wa utoaji kwa muda wa miaka mitano ili kubaini mapugufu ,vigezo na kama kuna haki na usawa katika utoaji wa Fedha kwa wahusika .

Lakini nimekuta habari katika gazeti la mwanachi ya wiki hii ikisema bodi ya mkopo haitoi ushirikiano kwa timu ya uchunguzi .Sasa hapo lazima tutafakari kwamba labda kuna madudu yanafichwa nyuma ya pazia sasa ni wakati wa kuamka
117c1ac0a1774c40a61a13a115b4a076.jpg


Screenshot_20221028_145056.jpg

HELSB kunani ?
Screenshot_20221028_145035.jpg


Screenshot_20221028_145015.jpg


Maoni yangu binafsi na ushauri:

Kuna mtu aliwahi kuniambia elimu ya Tanzania inakuwa na umbo la pyramid akimaanisha kuwa kukiachiwa upana juu mtabanwa .Hali ya sasa watu wameongezeka darasa la 4 hafeli mtu tena la 7 vile sasa imefikia idadi ya watu kufaulu form 2 na form 4 ni kubwa tofauti na zamani .Mimi Nilifanya uchunguzi shule ya A_level nikiyosoma nimekuta idadi ya waliofaulu kidato cha tano mwaka 2020 na 2021 idadi imeongezeka ndani ya mwaka mmoja kutoka wanafunzi 200 mpaka 500 ,hapo ni ongezeko kubwa sana ndani ya muda mfupi hivyo inatarajiwa hata idadi ya watakaojiunga na vyuo vikuu kuongozeka kwa kiwango kikubwa kila mwaka.

Nikiangalia serikali jitihada kubwa inatumia kuboresha Sekondari na shule za msingi mfano fedha za Vivid na kusahau koboresha miundombinu ya Advance levo na vyouni ili kukabiliana na wimbi la ongezeko la wanafunzi.Ningependa kushauri waongoze nguvu vyuoni na kwenye shule za advance vilevile bila kusahau kufanya maboresho katika suala la utoaji wa mikopo.

#UziTayari
 

Attachments

  • IMG_20221028_174816.jpg
    IMG_20221028_174816.jpg
    35.4 KB · Views: 19
  • IMG_20221028_172130.jpg
    IMG_20221028_172130.jpg
    81.1 KB · Views: 20
Hili Jambo njia Nzuri ya ku-deal nalo ni kuhakikisha Serikali inatenga au kuandaa bajeti kubwa pasipo kuangalia Background ya Familiya ya Mtu

Mfano ugawaji wa mkopo kwa kujuana , kutoangalia wahitaji wanahitaji Nini !!

Angalizo Serikali inabidi kuhakikisha inabiresha Elimu ya chuo kikuu maana huko ndo Taifa linategemea Kupata wataalamu

Imefika hatua hatuoni msomi na hasiyesoma TOFAUTI zao hii Ni kwa ajili ya ugawaji w Degree za chupi , mikopo ya chupi

Naomba niishie hapa hila ongezeni bajeti kubwa ya mikopo ya chuo kikuu na wekeni juhudi kubwa za kuhakikisha Elimu inakuwa bora
 
Ukweli ni kuwa bodi ya mikopo inatakiwa kuvunjwa. wale watu wameoverstay pale wanajiona miungu watu wanafanya kazi kizembe sana. Hawakujua kuwa vyuo vinafunguliwa mwishoni mwa october?
 
Ukweli ni kuwa bodi ya mikopo inatakiwa kuvunjwa. wale watu wameoverstay pale wanajiona miungu watu wanafanya kazi kizembe sana. Hawakujua kuwa vyuo vinafunguliwa mwishoni mwa october?
Kweli kabisa ,kama sio kuvunjwa basi kupigwa msasa wa kutosha kurekebisha mapungufu yanayojitokeza.
 
Updates : Serikali imesikia kilio cha wanafunzi wengi kuhusu kupata Mkopo wenye asilimia chache katika ada ,hali hiyo ilikuwa imefanya wanafunzi wengi wa hali ya chini kuishi katika mazingira magumu .

Sasa katika vyuo vingi idadi kubwa ya wanafunzi wamepata nyongeza katika ada na kufikia 100% katika nyongeza iliyotoka mwaka huu kipindi wapo vyuoni ,na imekuwa ahueni katika masomo yao baada ya serikali kupunguza mzigo mkubwa katika ada.
 
Wakuu nilichukua result slip ya forms six ila Vijana wa boada boda wamepita na mkoba result ikiwa ndani naomba msaada kwa anaejua nianzie wapi
 
Back
Top Bottom