Wizara ya Elimu acheni kuchezea elimu

WAZO2010

JF-Expert Member
Feb 19, 2021
1,610
3,738
Leo 20/10/22 Naibu Elimu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Technolojia Bw. Omary Kipanga ame tangaza kuwa hivi karibuni serikali ina tarajia kufuta darasa la 7.

Hivyo shule ya msingi ita ishia darasa la 6 tu na hakutakuwa na mtihani wa mwisho. Ila mtihani wa Mwisho utakuwa kidato cha nne. Hii ni kutaka kuburuza Elimu ya Tanzania kama kokoro lenye kubeba kila takataka. Shule ya msingi zamani tulianza na miaka 9 hadi 12. Hivi leo tuna anzisha watoto na umri wa miaka 5 hadi 7. Watoto wana maliza Elimu ya msingi wakiwa wadogo hata uelewa wao umekuwa mbovu. Umri na uwezo wa vichwa vyao haviendani na uzito wa masomo.

Wizara Elimu ili futa mitihani ya kujaza nafasi wazi, kukukotoa na kupata jibu, mkaleta mitihani yote Multiple Choice. Hapa mmeua uwezo wa kufikiri kwa watoto. Wana buni tu Majibu. Una kuta kidato cha kwanza kuna watoto hata 10 darasa 1 hawajui kusoma wala kuandika.

Vilevile, ile program ya Big Results Now, Mfumo wa kupanua goli. Ume haribu Elimu ya Secondary. Kumekuwa na mashindano ya kufaulisha kila mkoa. Hadi mikoa ikiyo kuwa ina kuwa ya mwisho huko Zanzibar, siku hizi ina ongoza kitaifa (siasa)!

Kila shule ni Division One. Watoto ufaulu ni kubwa kuliko kilichopo vichwani mwao. Elimu imekuwa rahisi sanaaa. Nakumbuka Wizara iliwahi kuleta Ujinga wa Kuunganisha Chemistry na Biology, History na Geography, nk. Mara History of Tanzania. Mwingine Tusome Betting!! Mna tuchanganya sana. Baada kila baada ya miaka 5, cheti kipo tofauti!! Homo sexual sasa ina anzia Darasa la 4 hadi form six. Kwa sasa mnafundisha sana kufaulu kuliko Maarifa.

Wakifika vyuoni, watoto ni wa hovyo hovyo. Hawajui kitu. Ndio matokeo ya Supplementary na Disco kuwa nyingi. Hata haya matokeo ya Law School ni madhara ya mfumo mbovu wa Elimu ya awali ya Tanzania (std 1 to Form 6). Hata std 7 wa zamani ana mzidi Graduate wa sasa wa chuo akili na kuishi mtaani.

Angalia hata picha za uchi, video za kufirwa Instagram, Tiktok, Facebook, nk ni za hawa Graduate wa chuo siyo std 7. Watoto wameharibiwa na smartphone from Primary School.

Naungana na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Bw. Antony Mtaka kupinga uharibifu wa Elimu nchini na hawa Viongozi wa wakuu wa serikali ilihali watoto wao husoma South Africa, USA, Kenya, UK, Israel, China, Germany, nk hili tulishuhudia wakati wa Corona wakihaha kurudi Tanzania.

Mapendekezo (Ushauri wa Bure):

1. Mawaziri wasiwe na mamlaka kuhusu mitaala ya Elimu. Hii kazi iachwe kwa Makatibu na Wakurugenzi wa Elimu (Professionals only siyo wana siasa). Na Waziri na Naibu wake wote wawe na Division One au Div 2 na chuo wawe na Upper Second Class au Distinction kuteuliwa. Tuna teuwa watu wa kutoa matamko tu, kumbe tatizo liko vichwani mwao. Elimu ndio Engine ya Nchi. Tusicheze nayo. Leo King Msukuma ana wadharau Ma Prof. wote Bungeni kisa Elimu yetu ni mbovu. Shida ya watendaji wengi Tz ni waoga, wanafiki, kujipendeza, ebu wambieni ukweli Mawaziri hata Rais pia.

2. Darasa la Saba lisifutwe. Ila liboreshwe. Yaani darasa la 7 liwe la kumuandaa mtoto kujiunga Form One. Hapa masomo yote ya anze kufundishwa kwa English. Isipokuwa Kiswahili tu.

3. Ondoeni mambo ya Multiple Choice. Watoto watumie akili zao hasa Hesabu, Sayansi na Maarifa.

5. Punguzeni siasa ktk Elimu. Shule ya Msingi Bakora zirudi na mchakamchaka wa kukimbia. Wizara ya Elimu acheni kuona Walimu kama ni Wakosefu Muda wote. Mna watia Walimu woga. TCU acha kuingilia vyuo. Acha watoto watandikwe SUPP na DISCO akili zikae sawa. Wata soma tu.

6. JKT iwe lazima na kwa wote.

7. Tuanze kubadili mfumo wa Walio feli kuwa Walimu. Hao waende Jeshi, Polisi, wajisiriamali, nk ila Division One na Division Two ndio wawe Walimu.

8. UMISETA na UMITASHUMITA tutenge shule maalum za kuchukua washindi wa timu nzima za mipira, riadha, kuruka, mikuki, kuogelea, disco, nk walelewe katika shule zao maalum huku wakiendelea na masomo mengine. Tume kuwa tuna wapoteza njiani hawa vijana kama Taifa kwani hatuna muendelezo wa Vipaji.

9. Elimu iwe ya Vitendo zaidi kuliko nadharia. Hapa Serikali iwe tiyari kutoa pesa za kutosha. Practical from std One to University. Pamoja na tafiti kwa vyuo vikuu. Huu ni uwekezaji. Tuwekeze kwenye Elimu kuliko kuwekeza kwenye siasa za hovyo.

10. Tusipende kusikiliza kila ushauri wa Wazungu. Wazungu lengo lao ni kuhakikisha sisi Wa Africa tuna bakia shamba la raw material na market place kwao. Wengi ni wanafiki tu. Mf. Mradi wa Bomba la Mafuta kutoka Uganda kwenda Tanga wana pinga kwa maslahi ya Biashara zao.

11. Mwisho, naomba Wizara ya Elimu mkae chini mpate mfumo sahihi wa Elimu ya Tanzania, kuanzia Darasa la kwanza hadi chuo kikuu hata kwa ku copy na ku paste huko Europe, siyo matamko ya kila mwaka. Mara Biology na Chemistry.
Mungu Ibariki Tanzania
 
Nyie mliosoma zamani mbona hamna impact yoyote katika Maisha mmekuwa mafisadi tu na kuajiriwa kwa wahindi huku mkinyonywa

Elimu sio kujibu mtihani Bali ni kuwa innovative na ku-Apply katika real life situation.
Ww unadhani Nchi hii ina ongozwa na nani hadi hapa ilipo? Ikiachiwa nyie si itakuwa nyuma ya Burundi.

Just appreciate their efforts, and Add a block!
 
Bila shaka wewe utakuwa mmiliki wa Shule binafsi ya Msingi, mmeifanya mitihani ya darasa la 7 kama kivutio cha kupiga mamilioni yetu ya ada.
Sina shule. Ila ni Mtanzania. Hapa ndio tatizo la Elimu yetu. Mada ni kuboresha Elimu. Ila mawazo yanayo tolewa hapa. Daah
 
Kwanza elimu iwe mwisho darasa la 3. Sio mtu anasoma mpaka anazeeka anarud home anaanza 0 kutafuta mtaji na kupata uzoefu wa ujasiliamari wakati huo wenzake aliowaacha darasa la 7 wameanza kutusua au kuona mwanga wa maisha.
 
Suala la kuanzia darasa la kwanza hadi form 4 hakuna mtiani wa mchujo napinga kwa miguu na mikono yote.....

Hivi hawa wanafunzi wasiyojua kusoma na kuandika wataenda kuchujiwa wapi??
 
Ulaya watu wanamaliza wadogo sana na wala hamna shida
Msipende kabisa kujilinganisha na Ulaya, hamtaweza. Si umesikia leo waziri mkuu wa Uingereza amejiuzulu mwenyewe? Kabla yake kuna mawaziri wawili pia wamejiuluzu, haya niambie kwa mara ya mwisho kusikia Waziri au Waziri mkuu kujiuzulu huku bongo??
 
Umesahau lugha ya kufundishia

Tukubaliane lugha ya kufundishia ni tatizo.

Tuchague lugha Moja ya kufundishia kama ni kiswahili au kiingereza kuanzia msingi hadi chuo kikuu.

Kama kiswahili hakijitoshelezi kwenye misamiati basi twende na kiingereza Wala tusione aibu katika hili.

Na pia tukubaliane kuboresha maslahi ya walimu Ili kuwamotisha kufanya kazi kwa kujituma. Ikiwa pamoja na kiwango Cha elimu zao kupandishwa kwa maana ha kwamba walimo wote wa msingi waanzie kuwa diploma ya elimu.

Tatizo ni kwamba tuna wanasiasa Kariba ya mzee makamba ambao wanataka tuwashukuru kwa mbishe zao mbovu mbovu wanazozipiga zinazoligharimu Taifa hili na bado wanataka wapewe CREDIT geeeez!!!

Hio ni shida.
 
Back
Top Bottom