Kwa wanaume ambao mlikuwa na kazi lakini sasa hamna na wake zenu ndio wanaoendesha familia mliwezaje kutoboa?

Tatizo huwa sio mke, tatizo ni pale atakapoacha kukusikiliza aanze kusikiliza wapambe ndugu jamaa na marafiki.

Ukifanikiwa kumfanya akusikilize wewe na ukakata network zote utajikuta unarudi relini.

Jitahidi basi Hata kubeba zege mkuu maana Kuna raha kuhudumia mke. Hata matatizo ya dunia yalianza siku Eva alipomletea Adam chakula
Hahahahahah Eva alipomlisha Adamu ndio majanga yalianza sio 😂😂😂
 
Kuhusu wanaume pia naanza kuhisi sababu kuna mda atapigiwa simu hata saa saba za usiku na anapokea bila wasiwasi ukimuuliza atakwambia ni workmate wake anamkumbusha kazi za kesho ofisini

Sent from my HUAWEI LUA-U22 using JamiiForums mobile app
Hahahahahahaha da una hali mbaya sana jamaangu 😂!!! Workmate anampigia simu saa 7 za usiku tena
 
Cha ajabu wao ndio wa kwanza kudai haki sawa lakini kiuhalisia hakuna haki sawa mwanaume lazima uwe juu kwa sababu Kama wanatarajia mwanaume uprovide hata Kama hali ya uchumi umeyumba. Huyo mwanamke angekua na busara kidogo katika kuiponya ndoa yenu kupitia shughuli anayoifanya angekutafutia hata mtaji kidogo
 
We jamaa fanya mpango uhame hapo uende mkoa mwingine hata kwa washkaji zako ukapige kazi yoyote itakayokuingizia pesa. Ukipata pesa zigawe, zingine fanya matumizi yako zingine mtumie. Believe me, ukiweza kumtumia pesa hata kama ni kidogo na hazina msaada mkubwa lazima ataanza kukuheshimu. Achana na mawazo ya kugongewa kwa sasa kwani huwezi kuzuia kama ana tabia hizo.

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
 
Hahahaha
Jamaa aliletewa fruits wakati yeye ndiye aliyepewa jukumu la kuongozA jahazi la edeni.

Movie ya mwanadamu ikaanzia hapo. Hahahaha
Dah ila haya maisha bana, tucheke sana ila mzee kufulia kubaya sana yani! Uwe ghafla huna kitu halafu unamiliki mke mara bills umezishindwa kuzilipa aisee ni balaa na nusu! Yani friji lilikuwa linajaa mamisosi panya na mende hawakauki mjengoni ghafla wamehama nyumba inafikia stage una struggle kuweka chakula mezani mnaanza kula michicha na tembele wakati ilikuwa mwendo wa kuku, samaki na nyama!

Yani msione vizee vinakomaa maofisini hata kwa ndumba asikudanganye mtu kuendesha familia kwa hela ya kubahatisha bahatisha mtaani sio swala la masihara kmmmk! Leo una hela kesho huna yani dah...Hela za ghafla zile ukitekenya ef 50 ya haraka huna😎
 
Yaani kama kusali na sali sn ndugu yangu hadi yale maombi ya usiku wa manane nasali, na kufunga lkn naona msala bado upo upande wng

Vipindi vyangu vya Tv zamani vilikuwa ni eatv, wasafi, dizzim, channel 10+, na trace muzik, yaani mda wote ni mangoma tu lkn sasa hivi naangalia vipindi vya akina mwamposa, suguye, Emmanuel tv, na vipindi vingine vya dini ili niwe karibu na mungu

Sent from my HUAWEI LUA-U22 using JamiiForums mobile app
Usichoke kumuomba Mwenyezi Mungu nyakati zote za uhai wako
 
Back
Top Bottom