Kwa wanaosema biashara ya duka haina faida, soma hapa tafadhali

mm nimeifanya 2011..kwakweli faida yake ndg..ss hv ht nipewe5m hii biashara siirudii...sukari mfuko unanengeneka for 2 wks upate 7500😂😂😂sitaki..

ngano faida ilikuwa km 6000 bas uishe ht 2 days😏 unakaa nao week na nusu😑

vinywaji ndo vinabeba duka

Uliweka na friji pia?mpesa haikukupa faida
 
Ni kweli inalipa mkuu biashara hiyo ukiwa serious tuuuu hasa kwwnye vinywaji na vocha hizo za kurusha mkuuu
Ila nifahamishe na hao voda nami niwwke dukani kwangu
 
Kumekuwa na malumbano kuwa biashara ya duka hasa rejareja haina faida....leo nitaleta baadhi ya bidhaa tu kupinga malumbano hayo..(maana ndo ishu nnayoifanya)

Just kabla sijaanza, ukitaka kuona mafanikio ya hii biashara wewe muuzaji uwe mtaji wa kwanza...!! Kichwa chako kiwe mtaji dukani pia mazoea kwenye duka pamoja na mahusiano ya kimapenzi weka pembeni kabisa

1. Soda
Pepsi huuza kreti kwa sasa 9500(soda jumla hua 24 kwenye kreti). Ukiuza jumla utapata 12,000(faida hua ni 2500)
Coca wanauza 10,000(hapa faida 2000). Take away zinauzwa katon 9,000 na znakuwa 12(faida 3,000)

2. Vocha
Hapa nazungumzia za kurusha...za kukwangua sincerely speaking sijawahi kuuza na sitarajii

- Tigo hutoa 6% kama faida kwa kila float utakayonunua(ukinunua float 10,000 unapata 600(hapa bado faida za kwenye vifurushi). Ukiunganisha internet ya buku kwenye float wanakata 900 mteja atakupa 1,000..100 ya kwako

Voda hutoa 8% kila unaponunua float(ukinunua float 10,000 unapewa 800(hapo pia kuna faida ukiunganisha vifurushi)

3. Maji makubwa Uhai
Lita 6 unanunua yakiwa matano kwa 8500 utauza kwa elfu 2 jumla unapata 10,000(1,500 ya kwako)

Lita 12 unanunua kila moja 2500 utauza kwa 3,500(1,000 kila dumu moja ni ya kwako)

4. Viberiti unanunua dazeni 4,500 unapata 9,000(4,500 ya kwako)

5. Pampers unanunua 14,000, zinakuwa 40(kila moja utauza 500. Unapata 20,000....(elfu 6,000 ya kwako)

6. Sabuni ya unga ya kufunga
Utanunua kiroba elfu 31,000. Ukifunga vizuri na kwa kipimo cha 500(faida mpaka 10,000 unapata)

Kuna vingi vya kuweka ila sitamaliza leo. Hapo bado sijataja unga, mchele, sukari, ngano, maharage, omato na vingne kibaaao

Hakuna biashara mbaya, ni wewe mfanyabiashara....!! Msimamo wako na unavyoichukulia biashara yako

Sent using Jamii Forums mobile app
asante sana kwakweli umefanya jambo jema sana naomba twendelee kupeana nondo juu ya biashara hii, ikiwezekana nitakufuata inbox.
 
Watu wanashindwa kuelewa jambo, mafanikio au maendeleo ya biashara huangaliwa kwa hatua ulopiga wew na biashara yako

Kama biashara inakua nawe maisha yanakunyookea then naweza sema inakupeleka kule utakako.

Mimo now nimepanga chumba now nna friji 2, now nna kreti 10 wkat nlkuw na 2 tu...mzigo dukan upo na nnawaza kuongeza zaidi

Kama mtu wasema hii biashara huwezi bas hakuna biashara utakayoweza maana biashara zote znafanana changamoto

Na pia kama wataka kufanya biashara na still unataka anasa kwa kiwango kikubwa unataka kuwa free kuzurura, kutumia hela, utaanguka wew na biashara yako.
 
Kama una nia kweli na biashara yako....weka upuuzi pemben...jua unatafta maisha...panga malengo....anza kazi....na uisimamie

Na hakuna kitu kinacholeta raha kama kuinyanyua biashara....hasa hii ya duka

Just kumbuka kuweka akiba au kucheza michezo ya kuchangiana ili kuongeza mtaji lkn pia kwa ajili ya mahitaji yako nje ya duka(ila chagua watu wanaoaminika na unaowaweza)
IMG_20190404_223306.jpeg
IMG_20190106_184046.jpeg
IMG_20190110_134044.jpeg
 
Kama una nia kweli na biashara yako....weka upuuzi pemben...jua unatafta maisha...panga malengo....anza kazi....na uisimamie

Na hakuna kitu kinacholeta raha kama kuinyanyua biashara....hasa hii ya duka

Just kumbuka kuweka akiba au kucheza michezo ya kuchangiana ili kuongeza mtaji lkn pia kwa ajili ya mahitaji yako nje ya duka(ila chagua watu wanaoaminika na unaowaweza)View attachment 1101778View attachment 1101779View attachment 1101780

Hongera sana brad wengine humu wanaishi kwao kula kulala utashangaa wanakuzonga,,piga kaziiii kaka
Mi naonaga wenye hizi biashara wanajenga,wanasomeshaaa na wanaishi vizuri tu
 
Hongera sana brad wengine humu wanaishi kwao kula kulala utashangaa wanakuzonga,,piga kaziiii kaka
Mi naonaga wenye hizi biashara wanajenga,wanasomeshaaa na wanaishi vizuri tu
Mim nmemuona mama alipanga kwa baba...!!alkuwa mama ntilie akafungua duka!!

Now ana duka la jumla

Nmejifunza kupitia hlo na watu wengi niwaonao na biashara zao...!!

Na wengne now wanajifunza kupitia mimi
 
Hiii biashara inafaida na ndio maana tunafanya cha msingi pata eneo zuri hasa lako mwenyewe mara nyingi duka likichanua vizuri wenye maeneo baadhi yao uanza visa wanataka wakutoe nawao wafanye biashara kama ni rahisi hivyo kama sehemu ya kupanga chukua mkataba wa muda mrefu ama panunue,kingine jitahidi kujua maduka yanayouza vitu jumla kwa bei ndogo,nunua vitu kwa carton hii inakuwa na faida zaidi ya dozen kingine usimamizi mzuri kauli njema kwa wateja
 
Hiii biashara inafaida na ndio maana tunafanya cha msingi pata eneo zuri hasa lako mwenyewe mara nyingi duka likichanua vizuri wenye maeneo baadhi yao uanza visa wanataka wakutoe nawao wafanye biashara kama ni rahisi hivyo kama sehemu ya kupanga chukua mkataba wa muda mrefu ama panunue,kingine jitahidi kujua maduka yanayouza vitu jumla kwa bei ndogo,nunua vitu kwa carton hii inakuwa na faida zaidi ya dozen kingine usimamizi mzuri kauli njema kwa wateja
Well brother
 
Hakuna kazi ngumu kama ya duka la reja reja ukitaka kuona faida ya biashara uwe kitega Uchumi kingine usitegemee hapo kwenye hilo duka, alafu uwe unauza mwenyewe kwasababu mfanyakazi akiiba hata 2000 kila siku tuu amekuacha.ni kweli faida ni ndogo ndogo sana unatakiwa kuwa makini sana.
 
Hii biashara miyeyusho Sana , issue ni moja Tu worksmart earn more na hapa ndo akli inatakiwa ufanye kaz ..biashara gani kila sku unakuwa na shati moja limejaa unga ..Mimi hamna wakuu, hii biashara inafaa wazee waliofikia umri wa kufunga mahesabu just wanatafuta hela ya Kula mana washajenga washasomesha na mambo mengi ya msingi wamefanya .... Kijana unatakiwa upige show za kibabe unakunja hata 500000 Kwa wiki siyo mbaya....
Ifikie hatua mazingira yasituendeshe Sana Bali Sisi ndo tuyabadili mazingira yaendane na tunachokitaka ...
 
Back
Top Bottom