Kwa wanaosema biashara ya duka haina faida, soma hapa tafadhali

Kumekuwa na malumbano kuwa biashara ya duka hasa rejareja haina faida. Leo nitaleta baadhi ya bidhaa tu kupinga malumbano hayo (maana ndo ishu nnayoifanya)

Just kabla sijaanza, ukitaka kuona mafanikio ya hii biashara wewe muuzaji uwe mtaji wa kwanza. Kichwa chako kiwe mtaji dukani pia mazoea kwenye duka pamoja na mahusiano ya kimapenzi weka pembeni kabisa

1. Soda
Pepsi huuza kreti kwa sasa 9500(soda jumla hua 24 kwenye kreti). Ukiuza jumla utapata 12,000 (faida hua ni 2500)
Coca wanauza 10,000(hapa faida 2000). Take away zinauzwa katon 9,000 na znakuwa 12 (faida 3,000)

2. Vocha
Hapa nazungumzia za kurusha, za kukwangua sincerely speaking sijawahi kuuza na sitarajii.

- Tigo hutoa 6% kama faida kwa kila float utakayonunua (ukinunua float 10,000 unapata 600 (hapa bado faida za kwenye vifurushi). Ukiunganisha internet ya buku kwenye float wanakata 900 mteja atakupa 1,000..100 ya kwako

Voda hutoa 8% kila unaponunua float (ukinunua float 10,000 unapewa 800 (hapo pia kuna faida ukiunganisha vifurushi)

3. Maji makubwa Uhai
Lita 6 unanunua yakiwa matano kwa 8500 utauza kwa elfu 2 jumla unapata 10,000 (1,500 ya kwako)

Lita 12 unanunua kila moja 2500 utauza kwa 3,500 (1,000 kila dumu moja ni ya kwako)

4. Viberiti unanunua dazeni 4,500 unapata 9,000 (4,500 ya kwako)

5. Pampers unanunua 14,000, zinakuwa 40(kila moja utauza 500. Unapata 20,000 (elfu 6,000 ya kwako)

6. Sabuni ya unga ya kufunga
Utanunua kiroba elfu 31,000. Ukifunga vizuri na kwa kipimo cha 500 (faida mpaka 10,000 unapata)

Kuna vingi vya kuweka ila sitamaliza leo. Hapo bado sijataja unga, mchele, sukari, ngano, maharage, omato na vingne kibaaao

Hakuna biashara mbaya, ni wewe mfanyabiashara. Msimamo wako na unavyoichukulia biashara yako

safi sana.
 
Back
Top Bottom